Jinsi Wakili Mwalle alivyohamisha mabilioni

Jamii Africa
medium mwalle

medium mwalle
HATIMAYE imebainika jinsi Wakili maarufu mjini hapa Mediaum Mwalle alivyokuwa akihamisha mabilioni kwenye akaunti mbalimbali zinazodaiwa kufikia Sh. Bilioni 18.

Kupitia hati ya Mashitaka alityosomewa jana hospitalini hapo na Mwendesha Mashitaka Frederick Manyanda imebainika kuwa mtuhumiwa huyo aliyesomewa mashitaka 13, ambapo kosa la kwanza hadi la tatu ambalo ni la kughushi anadaiwa kulitenda Januari 6 Mwaka 2010 na Januari 13.

Alidai kuwa mtuhumiwa katika kughushi huko alifanikiwa kuhamisha kiasi cha fedha kwenye Kampuni kadhaa kwa siku tofauti ambazo ni Oliva Green, Nyamao Mbeche Hollo, Gregg Motachwa, Ogembo Meetchel, John H. Adam na Mosoto  O.Haye.

Alidai kuwa kosa la tatu hadi la 13 ni la kuhujumu uchumi ambalo alifanya Februari 16 mwaka jana, ambapo alihamisha fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.9   kutoka kampuni ya Ogembo Chacha na Gregg Motachwa Mwita.

Hati hiyo ya Mashitaka imeendelea kudai kuwa kosa la Nne ambalo mtuhumiwa anadaiwa kulitenda Machi 5 Mwaka 2010 na kufanikiwa kuhamisha Dola za Marekani 200,000.

Kosa la tano katika hati hiyo linatajwa kutendeka Machi 30, Mwaka 2010 ambapo mtuhumiwa aanadaiwa kufanikiwa kuhamisha Dola za Marekani 159,500. Huku kosa la Sita likidaiwa kutendeka Septemba 27 Mwaka 2010 na kufanikiwa kuhamisha Dola za Marekani 5,500.

Hati hiyo ya Mashitaka ambayo ilibadilishwa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi kukataa kuipokea awali imelitaja kosa la Saba kuwa linadaiwa kutendeka Novemba 2 Mwaka 2010  na mtuhumiwa anadaiwa kufanikiwa kuhamisha Dola  1,246,624.84.

Kosa la Nane katika hati hiyo ya mashitaka linadaiwa kutendeka  Desemba 21 Mwaka 2010  na mtuhumiwa huyo alifanikiwa kuhamisha Dola za Marekani 416,000.02. Kosa la Tisa katika masitaka hayo linadaiwa kufanyika  Desemba 24 Mwaka 2010 na alifanikiwa kuhamisha Dola za Marekani 521,000.

Hati hiyo iliyosomwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali Manyanda hospitalini alipokuwa amelazwa mtuhumiwa yalieleza pia kuhusu kosa la 10 ambalo linadaiwa kutendeka Januari 7 mwaka huu ambapo Mwalle anadaiwa kufanikiwa kuhamisha Dola za Marekani  808,000.02.

Kuhusu kosa la 11 linadaiwa kutendeka Februari 9 Mwaka huu na wakili huyo alidaiwa kuhamisha Dola za Marekani 527,000.02. Huku Julai 13 Mwaka huu mtuhumiwa alidaiwa kuhamisha  Sh 330,000,000 ikiwa ni kosa la 12 .

Hata hivyo mashitaka hayo yaliyosomwa jana ambapo mtuhumiwa huyo alikana masiataka yote na kupitia kwa wakili anayemtetea Loom Ojare aliiomba Mahakama impatiea mali zake zilizokuwa zinashikiliwa na polisi.

Ajare alidai hospitalini hapo kuwa gari la kifahari la mtuhuniwa aina ya BMW halikuwa limeoredheshwa kwenye hati ya mashitaka pamoja na simu za mtuhumiwa hivyo aliomba vitu hivyo virejeshwe. Hata hivyo Mahakama iliamuru vitu hivyo virejeshwe kama ilivyoombwa.

Mwalle alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashiotaka 13 mbele ya Hakimu Mfawidhi Charles Magessa ambapo mashitaka hayo hayakupokelewa kutokana na kukosewa namna ya kuandaliwa.

Kutokana na makosa hayo upande wa Mashitaka ulilazimika kuandaa hati mpya ya mashitaka kwa ajili ya kuisoma ambapo, mara baada ya kukamilika mtuhumiwa alisomewa akiwa amelazwa katika Hospitali kutokana na afya yake kuwa na mgogoro.

Hadi jana mtuhumiwa huyo alikuwa bado amelazwa katika Hospitali hiyo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa afya yake ilikuwa bado haijaimarika.

5 Comments
  • UTAWALA BORA NDIO NJIA PEKEE KUELEKEA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA JAMII YOYOTE ILE. HIVYO JAMII KWA MAANA YA WATAWALA NA WATAWALIWA AU VIONGOZI NA WANAOONGOZWA WANA JUKUMU LA KUHAKIKISHA KUWA WANASIMAMIA SIO TU KWA MANENO BALI KWA VITENDO MISING YA UTAWALA BORA. KWA KITENDO ALICHOFANYA WAKILI HUYO KAMA ITATHIBITIKA NI KWELI BASI ANAPASWA KUPEWA ADHABU KALI. HII ITAKUWA NI FUNDISHO KUBWA KWA WOTE AMBAO WANA AMINI KWA UBINAFSI WAO KWAMBA MALI ZA WATANZANIA HAZINA MWENYEWE NA HIVYO WAPATAPO DHAMANA YA KUSIMAMIA HUZANI NI KWAMBA WAMEMILIKISHWA.

    NI WAKATI WA KUONYESHA VITENDO ZAIDI KWA WOTE WANOKIUKA MISINGI YA MAADILI KATIKA KAZI NA TAALUMA ZAO. TUNATEGEMEA WANASHERIA KUWA WALINZI NA WATETEZI WAKUBWA WA HAKI NA MASLAHI YA WATANZANIA LAKINI KWA ALICHOKIFANYA MHESHIMIWA MWALE NI KUKIUKA KWANZA MAADILI YA TAALUMA YAKE NA PILI MISINGI YA UTUMISHI BORA. LAKINA TWAWEZA KUJIULIZA NI KWANINI MATUKIO YA UFISADI HAYPUNGUI NA HATA KUKOMA PAMOJA NA KWAMBA MEDI NA MAMLAKA ZINAZOZOHUSIKA NA KUPAMBANA NA RUSHWA ZINAPIKGA KELELE KILA IITWAYO LEO? NI WATUHUMIWA WANGAPI WALIOHUJUMU MALI ZA UMA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA IKIWAMO KIFUNGO NA KUREJESHA MALI WALIZOIBA?

    JE HII YAWEZA KUWA NI SABABU YA KUDHOOFU KWA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA VILE JAMI HAINA CHA KUJIFUNZA JUU YA MADHARA YA RUSHWA HASA KWA MPOKEAJI NA MTOAJI KWANI KILA MTU HUONA KELELE HIZO NI KAMA CHACHU NA KAULI MBIU KATIKA KUHAMASISHA ZAIDI RUSHWA NA KUWAKUMBUSHA WALE AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE HAWAJAFIKIRIA KUZIPAMBAMBAJA FEDHA ZA UMMA? JE MENO YA TKUKURU YAMEOZA KWA SABABU YA KULA PEREMENDE ZA MAFISADI AU WATU WAMEPOTEZA UZALENDO NA HRUMA KWA WATANZANIA WA HALI YA CHINI?

  • Ni uporomokaji wa maadili katika nchi tangu viongozi hadi wanataaluma. Mwalle asingepaswa kuwa mwizi aliekubuhu kiasi hicho. Abebe mzigo wake huo yeye mwenyewe tu.

  • Mwalle ni kama kumbi kumbi Tanzania wapo watu zaidi ya mwalle wameiba mabillion kwa matrillion lakini hakuna hatua yeyote kwani rushwa kubwa (grand corruption) wakubwa wengi tu wanahusika,wapo watu wanamiliki mali nyingi mno visivyo halali na haviendani na kipato chao.

    Tiba ni elimu ya dini na uzalendo viwekwe kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo na yawe yalizima kwa kila mtu kusoma ili watu wawe na hofu ya MUNGU,sambamba na kuwekwa sheria kali mno,lakin kubwa ufuatiliaji na utendaji wa haki,kweli kwa usawa kwa watu wote.

    Mwalle kaiga toka kwa viongoz wetu wa tz teana ambao hawaja fungwa wengi tu.

  • Tazameni kesi ya ICC inayohusu viongozi wa Kenya zinavyoendeshwa je wtz tuna chochote tunachokjifunza? Downs,

  • NADHANI WAKILI MWALLE NI MTANDAO NA WALA SI MTU MMOJA . NAMWOMBEA KWA MUNGU AFYA YAKE IIMARIKE ILIATOE USHIRIKIANO JUU YA KESI YAKE. HII ITASAIDIA KUJUA NI AKNA NANI ALIKUWA ANASHIRIKIANA NAO. INASEMEKANA NI RAFIKI NA WAKILI WA MWAKILISHI MOMOJA WA MANANCHI KATIKA JIMBO MOJA LA KASKAZNI MWA NCHI HII

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *