Jinsi ya kujua kama Uzito wako unaendana na Kimo chako kiafya

Dr. Joachim Mabula

BMI hupatikana kwa kugawanya Uzito (Weight in Kg) kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in M) au Uzito (Weight in Kg) gawanya kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in Cm). Jibu utakalopata, zidisha kwa 10,000 au Uzito (Weight in Lb) gawanya kwa (Kimo Mara Kimo) (Kimo/Height in In) na Jibu utakalopata zidisha kwa 703.

Body Mass Index (BMI) ni njia nzuri na kuangalia kama Uzito wako upo katika afya njema.

Kwa watu wazima, BMI ni Kipimo cha kujua kama Uzito wako unaendana ka kimo chako.

Kwa watoto wa Umri wa Miaka miwili na zaidi, BMI Centile hutumika. Hiki ni Kipimo cha kujua kama Uzito wa Mtoto unaendana Na Kimo, Umri na Jinsia.

BMI hupatikana kwa kugawanya Uzito (Weight in Kg) kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in M) au Uzito (Weight in Kg) gawanya kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in Cm). Jibu utakalopata, zidisha kwa 10,000 au Uzito (Weight in Lb) gawanya kwa (Kimo Mara Kimo) (Kimo/Height in In) na Jibu utakalopata zidisha kwa 703.

Ukiwa na BMI inayozidi mipaka, upo katika hatari zaidi ya Matatizo ya kiafya kama Kisukari aina ya Pili (Type II Diabetes), Ugonjwa wa Moyo (Heart Disease) na Saratani (Kansa) za aina tofauti tofauti.

Baadhi ya watu wazima wana maumbo makubwa yanayoweza kusababisha BMI iwe juu zaidi ya mipaka; Mfano wachezaji wa Rugby ambao wanaweza kuwa na Uzito uliozidi sana (Obese BMI) ingawa wana miili midogo. Hata hivyo, hii haitaweza kutumika kwa watu wote.

BMI KWA WATU WAZIMA (BMI FOR ADULTS):

BMI inazingatia kuwa watu wako na maumbo na ukubwa tofauti tofauti. Ndio maana mipaka (Range) ya BMI inaonyesha ni ya afya njema kwa watu wazima wa kila kimo.

BMI zaidi ya mipaka ya Afya Njema, huonyesha kwamba una Uzito unaozidi kimo chako.

Mipaka ifuatayo hutumika kwa watu wazima tu:

BMI chini ya 18.5: Huonyesha kwamba upo chini ya Uzito (Underweight).

BMI kati ya 18.5 na 24.9: Huonyesha mipaka ya afya njema. Huonyesha kuwa uzito wako unaendana na kimo chako kiafya.

BMI kati ya 25.0 na 29.9: Huonyesha kuwa hali imezidi mipaka ya kawaida, hali inayomaanisha Uzito wako umezidi kawaida (Overweight). Pia inamaanisha kuwa wewe ni mzito zaidi kuliko mtu mwenye afya njema wa kimo chako.

Uzito uliopita kawaida unakuweka katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo, kupooza (Stroke) na kisukari aina ya pili (Type II Diabetes).

BMI ya 30 na zaidi: Inachanganuliwa kama uzito kupita kiasi (Obese). Kuwa na Uzito kupita kiasi (Obese) kunakuweka katika hatari zaidi ya Matatizo ya Kiafya kama Ugonjwa wa Moyo, Kupooza (Stroke) na Kisukari aina ya Pili (Type 2 Diabetes).

Kupunguza Uzito kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuleta kuimarika kwa afya, kuondoa maumivu ya mgongo na viungo.

uzito

Funguo kubwa za kupunguza uzito ni kupunguza vyakula vya wanga (Meals with Calories) na kufanya mazoezi ya mwili.

Kiwango cha Mazoezi ya Mwili huendana na umri. Watu wazima wa kati ya Umri wa Miaka 18 hadi 64 wanapaswa kufanya mazoezi kwa angalau dakika 150, Mazoezi kama kutembea kwa haraka na kuendesha baiskeli.

Kwa watu wazima wenye Uzito uliozidi kiasi, wanapaswa kufanya zaidi ya kutembea kwa haraka na kuendesha baiskeli.

CHATI YA KIMO NA UZITO (HEIGHT AND WEIGHT CHART)

Unaweza pia kutumia chati ya kimo na uzito ili kuweza kujua kama uzito wako unaendana na kimo chako kiafya. Chati ya kimo na uzito ni chati flani inayowekwa ukutani inakuwa urefu na uzito na hivyo mtu akipima uzito analinganisha na kwenye chati.

bmi

BMI KWA WATOTO (BMI FOR CHILDREN)

Kukokotoa BMI kwa mtoto, wataalamu wa afya huangalia uzito wa mtoto kwa kimo, umri na jinsia. Matokeo yake huitwa ‘BMI Centile’. BMI Centile ni njia nzuri kwa wataalamu wa afya kutambua kama mtoto ana uzito mzuri kiafya na kujua kama mtoto anakua kama inavyotegemewa.

BMI Centile hupatikana baada ya kupata jibu kwenye BMI ya kawaida na kulilinganisha kwenye chati ya BMI ya mtoto wako kulingana na jinsia yake; iwe ya kike au ya kiume, kuna chati yake maalumu. Unaweza kuwa umeshawahi fanya hivyo kwenye kadi ya makuzi ya mtoto wako.

Baada ya kukokotoa BMI Centile, Mtoto huanguka kwenye moja kati ya makundi manne:-

Chini ya Uzito (Under Weight): Chini ya BMI Centile ya Pili (Below 2nd BMI Centile).

Uzito mzuri kiafya (Healthy Weight): Kati ya BMI Centile ya Pili na ya Tisini (Between the 2nd & 90th BMI Centile).

Uzito Kuzidi (Overweight): Kati ya BMI Centile ya Tisini na Moja na Tisini na Saba(Between 91th to 97th BMI Centile).

Uzito kuzidi kiasi (Very Overweight/Obese): BMI Centile ikiwa ya Tisini na Nane na zaidi.

Kama mtoto wako ana Uzito uliozidi kiasi (Obese) atakuwa katika hatari ya kubwa ya kuugua sana kipindi chake cha utoto hata katika maisha ya baadaye.

Endelea Kufuatana nami kwa Makala zijazo, Nitakuelekeza jinsi ya kupunguza Uzito na uwe na afya njema kwa Ujenzi wa Taifa letu.

9 Comments
  • Ila tukumbuke milo tulayo, kwetu huwa kinyume, wanga huzidi vitamini, wakati vitamini hujakiwa kuzidi wanga.

    Je, uasili hautuathiri? Hususani turukiangalia tamaduni za wengine kwa unusunusu, mfano, uasili wa mtu mweusi ni kula kwa mikono, ila tumerukia tamaduni za wenzetu tukidai ndio ukisasa. Ila kwa kweli ni madhara na ushamba zaidi, badala ya kutumia desert spoons kulia deserts, tumetumia aina hiyo ya kijiko kulia milo mikuu, na bado tu, itambidi kushika paja la kuku kwa mikono kisha kurudia kijiko na kuendelea kula, wakati alitakiwa kuwa na umma na kisu kujihudumia huduma hii ya mlo kwa ujanja wa damaduni ya wenzetu!

    Ndivyo ilivyo kwa vyote tushikavyo kwa utamaduni nusu nusu, miziki pia vivyo hivyo, hatujui kiimbwacho ila kujifanya wajanja tuishia kuzipiga studioni na kusababisha maadili potofu mitaani. Haya sasa ni uzito, milo na life styles. Tamaduni ya majani (mboga) machace wanga kibao, tembea basi kama asili ya mwafrika, bado una gari, elevator na mistarehe kibao, calories zitapoteaje? Iga basi hata kufanya zoezi kama tamaduni za unaoiga!

  • mi nimekuelewa sana na ntajitaidi kuwaelimisha jamii inayonzunguka umuhimu wa kuwa na uzito usiozidi uwiano wa kimo.

  • Hello Dr. Joachim Mabula,

    Asante kwa article nzuri inayotupa furusa ya kujifunza umuhimu wa kujua uzito kulingana na kimo. Endelea kuelimisha jamii yetu.

    Irene A.

  • Ahsante sana Dr. Kwa maelezo yako ,nimefurahishwa sana na nimejifunza kitu hususani umuhimu wa mazoezi ya viungo kwa afya.

  • Ahsante sana Dr. Kwa maelezo yako ,nimefurahishwa sana na nimejifunza kitu hususani umuhimu wa mazoezi ya viungo kwa afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *