MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amevunja sekretarieti ya chama hicho inayoongozwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, hatua inayoelezwa kufuatiwa na maamuzi mazito zaidi.
Uamuzi huo wa Kikwete umefanyika usiku huu, huku hali ikiendelea kuwa tete mjini Dodoma kunakofanyika vikao vya chama hicho vilivyotanguliwa na sekretarieti na baadae Kamati Kuu.
Kwa mujibu wa habari hizo, Kikwete toka jana ameonekana kuwa mkali na ambaye amekua akitembea na ajenda mkononi huku wasaidizi wake wengine wakiwa hawaelewi undani wa ajenda yake ya mageuzi mazito ndani ya CCM.
Moto ulianza kuwashwa katika kikao cha Kamati Kuu ambako zile tetesi kwamba kuna mkakati wa kumuondoa Kikwete zilipodhihiri kuwa kweli ilipoibuka ndani ya Kamati Kuu hoja ya “kutenganisha kofia za Urais na Uenyekiti”
Taarifa ambazo ziliifikia mtandao wa Jamiiforums.com zilieleza kwamba Kikwete alipoona hoja hiyo imetajwa ndipo alipobaini kuwa “sasa mafisadi wamepania kumng’oa”.
Katika kamati kuu hoja ilikua ni nini kifanyike kuwadhibiti watuhumiwa wa ufisadi na pia kuhusu hatima ya Makamba.
Kwa mujibu wa Jamiiforums.com Kikwete anayo ripoti ya kitaalamu ikielezea sababu za yeye kupata asilimia 60 katika uchaguzi wa mwaka 2010 na kwamba ilipendekeza kuwa mafisadi watoswe.
Imeelezwa kwamba mjadala wa vikao vya Dodoma utazingatia hotuba ya Kikwete katika sherehe za CCM Februari 5, 2011.
Katika hotuba hiyo Kikwete alisema;
“Hatuwezi kuacha jukumu la kugharamia uendeshaji wa Chama chetu mikononi mwa wafadhili matajiri. Tunahatarisha uhuru wa Chama chetu.
“Chama cha Mapinduzi kiige tabia ya nyoka ya kila baada ya muda fulani hujivua gamba lake na kupata jipya.
“Hatuna budi kufanya hivyo na kufanya hivyo sasa. Wakati wa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa vya tathmini tutalijadili pia suala zima la mageuzi katika Chama.
“Nitapenda tuelewane juu ya namna tutakavyotekeleza agenda hii muhimu kwa uhai na maendeleo ya Chama chetu. Hili ndugu zangu haliepukiki.
“Lazima tukihuishe ili kukiongezea mvuto mbele ya watu. Tuutazame muundo wetu kama unakidhi haja.
“Tuwatazame viongozi watendaji kama wanakidhi haja na kama siyo mzigo unaokipaka matope Chama chetu. Wale tunaoweza kuachana nao sasa tuachane nao kwa maslahi mapana ya Chama chetu.”
Tuombe na kusali kwa Mungu huyu kiongozi wetu afunguke macho aoene kuwa kazungukwa na wapambe nuksi.
Uongozi wa vitendo utakiokoa chama na kurudisha heshima ya rais…watendaji,kama ilivyo nyumbani,wangeleta uvundo zaidi ikiwa wangeachwa bila kukemewa….amka na ongeza bidii za kiutendaji kiongozi wangu wa nchi.
analiona sana bt ndohvo hawez fanya lolote
wishful thinking. La kuvunda halina ubani
Nionavyo mimi hatua ya kuvunja secretaria na kuwatosa baadhi ya makada itaongeza mpasuku katika chama na hiyo ndio itakuwa shangwe kwa wapinzani.
Kweli ndugu yetu ameanza kujifunika shuka wkt kumekucha!!
kwa kimombo tunasema “knee jerk reaction”. Anafunga zizi wakati mbuzi wote wamekwisha toroka! Dear Me! Too little too late.
Now it is the time when people gets confused 🙂 lets wait and see kiini macho
so he think he has find a solution, but am telling you it is another illusion
Mr Kikwete it is too late to catch the bus. Mbona mafisadi wa Richmond na walafi katika TRA hujawasafisha? Hawa watendaji wa TRA wanaifanya hata bandari zetu na vituo vya TRA za mipakani tuzione kama simba mwenye njaa. CCM isitupake chozi la tope hamna jipya.
nikweli yakuvunda haina ubani vasco da gama atulie afanye kazi
Be carefull with ur decision Mr. President! (kikulacho ki nguoni mwako). Anyway goodluck, and watch out ur steps!
Good day!
Mwenyekiti wa ccm awe wakusubutu akifanya hivyo anaweza kunusuru chama lakini nionavyo mimi kwa macho na masikio yangu na jinsi wazee wengi wanao nizunguka hapa kwetu kijijini MKONKO WENGI WAMESITA NAKUJIVUA GAMBA mzee wa kwanza ccm ya NYERERE haipo tena wa tatu wazee wanapuuzwa Hivyo mwenyekiti wa ccm anakazi sana
Mhe,mzee mkubwa,inafaa tujue kwanza kabla ya yote kuwa ,hilo gamba mnalojivua mlilivaavaaje?kina nani walihusika?isije ikawa na top layer mlishiriki, ndio tuone namna ya kujivua, tena namna bora ya kujivua sio NAPEISM,huyo dogo sio muafaka kabisa,nae gamba tu,maana haitakua mujarabu kuwafanya wenzenu kama ishara ya de barking, wakati mlikivalisha chama wote, ee BOYS 2MEN. tatizo lingine mzee mkubwa hampendi kusikiliza wadau,japo wa mchangani,timu nzuri ipo, likini mnapenda sana kutumia ma risevu, MAXIMOISM kumtumia mapunda badala ya kaseja, yale yale kumpeleka MAGUFULI kwenye samaki badala ya uwaziri mkuu,unatarajia nini mzee mkubwa, UBABAISHAJI tu. sijui mnaogopa nini kumpa rungu huyo bwana maana ndio njia pekee ya kujivua gamba UNAPE ni USANII tu