Matokeo Yacheleweshwa; CCM yaanza kuiacha CDM nyuma kidogo; Shingo kwa shingo

Jamii Africa

Matokeo ya Uchaguzi mdogo wa Igunga yameanza kutiririka kwa taratibu sana kuliko ilivyotarajiwa huku vyama vya CHADEMA na CCM vikionekana kuchuana vikali sana. Hadi majira ya saa nne usiku huu ambao ndio muda uliotarajiwa kuwa na matokeo hakukuwa na masanduku yote yaliyokuwa yamerudishwa kwenye makao makuu ya Jimbo ambayo ni makao makuu ya Halmshauri ya Igunga.

Kucheleweshwa huku kwa matokeo kumeanza kuwajaza watu wasiwasi hasa kutokana na kukosekana na maelezo ya kueleweka ya nini kinaendelea. Hata hivyo baadhi ya maafisa wanaelezea ucheleweshaji huo unatokana na mvua kubwa iliyonyesha baadhi ya maeneo na hivyo kusababisha ugumu wa mawasiliano.

Kuna vituo 427 huko Igunga vyenye kata 27 na hadi mida hii matukio yaliyo na uhakika sana ni ile ya kata moja tu. Kuna uwezekano matokeo kamili hayatopatikana hadi majira ya kuanzia saa tisa au saa kumi alfajiri.

Matokeo ambayo tunayasikia hadi hivi sasa kwenye kata 18 hivi CCM inaongoza kwa kura 18,000 na CDM 15,000.

Tutaendelea kuwahabarisha matokeo ya uchaguzi huo.

Tofauti ya kura zinavyoendelea hadi hivi sasa chama chochote kati ya CCM na CDM chaweza kushinda kwani hakuna tofauti kubwa sana ya kura. Ikumbukwe kuwa kuna vituo vipatavyo 427 na vilivyoripoti bado ni vichache sana.

Hadi hivi sasa inaonekana Chama cha Mapinduzi kimefanya vizuri zaidi kwenye maeneo ya ngome yake hususan Kata ya Nkinga, Nguvu Moja na Itumba.

Hata hivyo tunapata taarifa kuwa mitandao yote ya Internet haifunguki huko Igunga na hivyo kufanya kazi ya kupasha habari kuwa ni ngumu sana.

UPDATE:

WAKATI matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa wakati wowote, Chama cha Mapinduzi (CCM) kinazidi kukibana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuanza kupata kura nyingi maeneo ya vijijini.

 

Hata hivyo hadi hivi sasa, taarifa zinazopatikana kupitia mtandao wa www.jamiiforums.com zinaeleza kwamba, ni vigumu kwa sasa kusema moja kwa moja nani ni mshindi japo inaonekana kwamba CCM wanaweza kushinda.

 

“Dalili ngumu kusema moja kwa moja maana Igunga mjini Chadema wanaongoza kwa zaidi ya nusu mfano vituo vya mwanzo Chadema walikuwa na kura 104 na CCM 78.

Hata hivyo maeneo mengi na wanaopoongoza Chadema na CCM pia wamepata kura za kutosha kuongeza idadi wakati maeneo ambayo CCM wanaongoza wanakuwa wamewaacha Chadema kwa kura nyingi,” anaeleza mtoa taarifa wa Jamiiforums.

 

Mashabiki wa chadema Igunga mjini walianza kushangilia wakataka matokeo yatangazwe wakiamini kwamba matokeo ya mjini ndio ya jimbo zima na baada ya matokeo ya maeneo mengine kufika mjini, vijana wa Chadema waliozingira eneo la kutangaziwa matokeo (Halmashauri) wakapoa….

 

Kwa mfano Nkinga ambako ni ngome ya Chadema CCM imepata kura 1479 na Chadema 1087, na kata ya Itumba nyumbani kwa Dk Kafumu Chadema wamepata 560 na CCM 1078 na Itobo CCM 730 na Chadema 362.

 

Kata ya Igurubi kwenye Waislamu wengi, mchuano ulitarajiwa kuwa kati ya CCM na CUF japo inaonekana kwamba Chadema sasa wamepata kura nyingi isivyotarajiwa kutokana na kuanguka vibaya kwa CUF kwa kuonekana hawajulikani ni wapinzani ama chama tawala.

 

Kata ya Igurubi, alikabidhiwa Mbunge wa Tabora Mjini, Ismael Aden Rage, ambako aliweka kambi huko.

 

Matokeo ya awali yanamuweka pabaya Mwenyekikiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba ambaye anatokea mkoani Tabora kwa kuzidiwa vibaya na Chadema.

 

 

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *