Mchungaji asomewa mashitaka hospitalini

Jamii Africa

MCHUNGAJI Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo(DRC) Jean Felix Bamana (45) amesomewa mashitaka akiwa kitandani katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi mjini Moshi, akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha binadamu.

Mchungaji Bamana ambaye ni mlemavu wa miguu, aliibua mvutano mkubwa ndani ya Jeshi la Polisi na serikali, alikamatiwa jijini Dar es Salaam akiwa na watoto wawili ndugu ambao aliondoka nao mjini Moshi, kwa ahadi ya kwenda kuwatafutia shule.

Alisomewa mashitaka hospitalini baada ya kugoma kupelekwa mahakamani tangu jumatatu wiki hii akidai ni mgonjwa huku askari wanaomlinda wakilalamika kuwa anafanya mchezo wa kuigiza.

Mshitakiwa huyo alisomewa mashitaka mawili ambayo yanaangukia kwenye sheria ya usafirishaji binadamu namba 6 ya mwaka 2008,mashitaka ambayo hayana dhamana hivyo kupelekwa rumande katika gereza kuu la mkoa wa Kilimanjaro la Karanga.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya,Naomi Mwerinde,mshitakiwa huyo anadaiwa kuwa mnamo Februari 18 mwaka huu huko Masama wilaya ya Hai,alimsafrisha(Jina tunalo) kwenda Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na wakili wa serikali,Stella Majaliwa,mshitakiwa huyo pia anashitakiwa kwa kumsafrisha (jina tunalo) kutoka Masama wilaya ya Hai Kwenda Jijini Dar es salaam kosa ambalo lilitendekea .

Baada ya kusomewa mashitaka hayo mshitakiwa alikana na iliamuliwa apelekwe katika mahabusu ya gereza la Karanga na hadi waandishi wanatoka katika wadi namba moja ambako mashitaka hayo yalisomwa,alikuwa bado hajaondolewa.

Kesi hyo imeahirishwa hadi machi 27 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa kutokana na upelekezi wa shauri hilo la jinai namba 13 la mwaka huu kutokamilika.

Kabla mahakama haijamalikiza kazi katika Hospital hiyo,mshitikiwa alilalamika kutokuwapo na huduma za vyoo vinavyokidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu ndnai ya wadi hiyo na hata alipokuwa akitaka kituo kikuu cha polisi mjini moshi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusomewa mashitaka hayo,mchungaji Bamana anayehudumu katika kanisa la Mikocheni B Assembles of God,aliwataka waandishi wa habari kuwasilisha kilio chake kwa mamlaka zinazohusika ili tatizo hilo la kutokuwapo na vyoo vya kukaa katika wadi hiyo liweze kutafutiwa ufumbuzi.

5 Comments
  • Inasikitisha lakini habari hii mbona haina ukweli kwa sehemu? Muandishi huyu amefanya uchunguzi kabla hajaandika alichokiandika? Mchungaji huyu SIO wa Mikocheni B ninawafahamu wachungaji wa Mikocheni B huyu sijawahi kumuona na wala Mik. B hakuna Mchungaji mlemavu.

    Mchungaji huyu alifika hapa nchini kama sikosei mwezi wa pili nahakuhubiri kanisa moja, alikuwa akizunguka makanisa mbalimbali jijini dar hadi huko moshi na arusha, imekuwaje kawa Mchungaji wa Mikocheni B?? Mama Rwakatare hana Mchungaji wa aina hii kuweni wa kweli msimpake mtu matope pasipo sababu.

    Mojawapo wa maadili ya uandishi wa habari ni kuhakikisha unachokiandika umekifanyia utafiti na kujiridhisha sio kuandika habari za uzushi tu, hii inaonyesha ni jinsi gani muandishi huyu hajazingatia maadili ya kazi yake bali amelipua tu!

  • Wee usiwashutumu Waandishi wa Habari bila kuwa na Data, ni mara chache sana Waandishi wanaoandika Habari bila kuwa na Data na hao sijui kama wapo.

    Ukweli ni kwamba sio watu wote wanaofanya Makosa wangependa waandikwe habari zao za kweli, hapo ndipo ugomvi unapoanza na kuwashambulia Waandishi wa Habari.

    Wee ungekuwa mtafiti kidogo na kama unafuatilia mahubiri ya Dr.Lwakatare katika TV ya Chanel Ten ungemuona Mchungaji huyo wa DRC, mimi mwenyewe nilikuwa navutiwa sana na Mahubiri yake wakati akihubiri lazima nimtazame. Swala hapa sio kumhukumu kama kweli amekosa. Mahakama itaamua, lakini ukweli ni kwamba anahubiri Mikocheni B. Ukikanusha hilo mbele ya jamii unaofahamu ukweli huo na wewe utaonekana una jambo nyuma yake. Mwombe Msamaha mwandishi aliyeandika habari hiyo kuhusu kumwona Mchungaji huyo Mikocheni B.

     

    • Bado nasimamia ninachokiamini kwamba Mchungaji huyu sio wa Mikocheni B; unaposema anahudumu/kuhubiri Mikocheni B ina maana ni mtu ambaye yuko hapo siku zote. Ningemuheshimu muandishi kama angebalance story angeuliza na upande wa pili ambao ni Uongozi wa Mikocheni B ili kujua ukweli kama Mchungaji huyo ni mmoja kati ya wachungaji wa Mikochini B au lah!

      Mungu ndiye hakimu wa kweli atahukumu sawasawa na mapenzi yake na palipo na Ukweli Uongo hujitenga.

       

  • Inabidi nchi iwe makini na watu kama hao wapo wengi sana wanaingia nchini kwa kigezo cha kwamba wahubiri kumbe wana yao mambo. Watakuja hadi magaidi sasa

  • Sikiliza Gladys huyo Felix alikamatiwa akiwa visiting mchungaji wa kanisa la mikocheni b. msaidieni kiongozi wenu maana nae kashfa zimezidi kumuabdama! Aagh!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *