RIDHIWANI Kikwete mtoto wa Rais Jakaya Kikwete ametajwa kuingilia na kuamua kuendesha siasa za Mkoa wa Arusha kwa kutumia ‘rimote Control’ akiwa jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano wa leo uliofanyika katikati ya Jiji la Arusha na kuhudhuriwa na vijana wengi, Ridhiwani ametajwa kuwashika baadhi ya viongozi wa UVCCM wilaya ya Arusha na kuwaweka kwenye himaya yake.
Akizungumza baada ya kuhitimisha kazi ya ufunguzi wa mashina ya CCM zaidi ya 100 katika maeneo mablimbali ya jimbo la Arusha, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha James Millya alimrushia kombora hilo Ridhiwani mbele ya halaiki ya watu mjini hapa.
Huku akionyesha kuzungumza kwa hasira Millya aliyeshiriki zoezi hilo akiwa na baadhi ya viongozi wa Umoja huo wa kitaifa, akiwamo Beno Malisa Makamu Mwenyekiti alisema, wanachama wa CCM mkoa wa Arusha na maeneo mengine nchini walimchagua baba yake Ridhiwani kuwa kiongozi wao na si mtoto wake.
“Huyu mtoto anataka kuongoza siasa za Arusha akiwa Dar es Salaam, hivi mbona sisi hatuingilii siasa za Bagamoyo, sasa tumtaka abakie na Bagamoyo yake na atuachie Arusha yetu. Anajifanya anajua sana, tunachojua sisi tumemchagua baba yake kuwa kiongozi wa taifa haiwezekani na mtoto wake aongoze Arusha,” alisema Milya huku akishangiliwa na ummati mkubwa wa watu.
Naye Malisa akizungumza katika mkutano huo wa hadhara alisema, yeye binafsi ameshuhudia jinsi viongozi wa uuma waliochaguliwa kuwatumikia wananchi wakijitahidi kuzuia kazi ya kufungua mashina ya CCM.
“Tumewajua wote waliopambana ili kutuzuia tusiimarishe Chama chetu, jamani hivi haya mambo ya urais wa 2015 yanatoka wapi wakati sisi tupo kwenye kuimarisha Chama. Mimi ni shahidi leo wametutumia mpaka sms kututishia tusifanye hii kazi, jamani viongozi wanaacha kufanya kazi ya kuhakikisha vijana wanaonbdokana na ukali wa maisha wanahangaika kuzuia kazi ya kufungua mashina.
Malisa alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa muda wa kufanya mambo kwa kutumia busara sasa umepitiwa na wakati.
Baadhi ya viongozi wa UVCCM waliokuwa katika shughuli hiyo ya kuzindua mashina ni pamoja na Mbunge wa Vijana Catherine Magige, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro Godling Moshi, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Morogoro, wajumbve wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Arusha, na viongozi wengine.
Utata wa kufunguliwa kwa mashina hayo uliibuka jana baada ya kambi ya Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha God Mwalusamba kutangaza kuwa haikuwa na taarifa ya ziara hiyo ya uzinduzi wa mashina.
Tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2010 Mwalumba alikuwa kambi ya Dk. Batilda Burian lakini mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo alihamia kambi ya Mary Chatanda Katibu wa CCM Mkao wa Arusha.
kazi kweli kweli kwani hawa watu hawaoni hali ya siasa ilivyongumu, kiasi cha kuwashukuru hata hao wanaojitahidi kukusanya watu. nadhani tusipige kelele tusubiri 2015 watu watasoma no.
Ifikie atua watoto wa vigogo waachane na siasa vinginevo watanyang’anywa hata vile ambavyo tayari walichuma kialali,kwa hakika wana macho lakini hawaoni dalili hizi za siasa za kileo!!!!!!!!!!!
kweli huo ndio wakati wa uvccm kujivua gamba haliyo sema millya na Beno ni dalili tosha kwamba wamechoshwa na siasa za kikwele na bado wapo wengi tu wameshoshwa
huyu mtoto wa presidee anataka kututawala kimabavu nini atuachie A town yetu tuna viongozi wa kutosha hakuna katiba inasema baba anaweza kusaidiana na mwanae kuongoza nchi
oooh! hata wao kwa wao huyu mtoto wa presidee atuachie A town yetu tuna viongozi wa kutosha,isitoshe hakuna katiba inasema baba na mwana wanweza kushirikiana kuongoza nchi
wavuane tu magamba
nahisi libya ikifika tanzania ama baghdad itapohamia bongo bagamoyo itakuwa sirte
ahaa
wang’oane meno wenyewe,, ukweli utabakia palepale “TUMEICHOKA CCM”.
Kama hali ikiendelea hivi yaani watoto wa Viongozi kuchukua hatamu kimtindo huo, huko tuendako kutatimka vumbi.
Ifikie hatua chama chetu kisome nyakati,watoto wa viongozi wasiwe na nguvu yoyote katika chama!uvccm inapaswa kuwa makini na hali hii kabla mambo hayajaharibika,mambo haya ndo yanawapa nguvu wapinzani!!!!!
Ndugu bora usiende , maana matapeli wengi sana Mjini hapa wasije kukufanyia kitu mbaya bure
Huyo ambaye amefikia hatua ya kuwafatilia watu wa kawaida kupitia wapambe wengi wenye njaa eti hao wenzetu yaani ni ccm na ni waislamu.
Nani kampa mamlaka ya kufuatilia maisha ya watu wengine?
believe me.kazi ya kuondoa mafisadi ni ngumu.tuungane bila kujali itikadi zetu tuwamalize na kuwafilisi.am telling you mafisadi hawaiathiri ccm tu watapenya hadi upinzani.penye rupia tupaangalie sana
Hii biashara ya wanasiasa ya kutufanya sisi kama maandazi hatutaki hata kidogo, wanatuletea ule usemi usemao “tembo wakigomba nyasi ndio zinazopata shida” hapa ukiangalia hawa mayanki wote katika hili bifu la kisiasa ni kwamba wanarimotiwa tu sisi tunabaki tukishabikia tu hawa mafisadi waliowatuma………Lamaana ni kwamba nchi hii imeishauzwa ukweli ndiyo huo sasa tufikirie jinsi ya kujitoa muhanga kuirudisha mikononi mwetu kidiplomasia tu!
CCM waachen waendelee kuvuana magamba, sumu hatawatoka,2015 wataisoma namba kwenye masanduku ya kura
Jamani, Ridhiwani iangalie familia ya Gadafi iliko leo hii. Jishughulishe na mambo yako binafsi. Walibya walipewa kila kitu na Gadafi bure lakini leo wamemuua kama mbwa mwizi uchunguzi ukionyesha kilichowaudhi watu wa Libya ni familia ya Gadafi kuifanya Libya ni nchi yao na wao ndio wenye haki ya kutawala. Soma alama za nyakati ukutani ili usitibue watz waliokwisha choshwa na utawala wa nchi hii.
Si jk aliwapasha lakini kwamba urais ni suala familia. Kwani yaelekea hamkumwelewa. Haya ni mambo ya BMW hayo
nyinyi mayanki, tunamtaka malema wetu wa tz afanye kama kule bondeni, msikubali kuwa ngazi za kuwapandisha wale wanaowania unyerere 2015