Mto Kiwila wasababisha majonzi Kyela

Stella Mwaikusa

Wananchi wa vijiji vya Lema, Busoka na masoko vilivyopo kata ya Busale wilaya ya  Kyela, wamelalamikia kukosekana kwa daraja  la kuwawezesha kuvuka toka ng’ambo ya  kijiji kimoja na kingine, kutokana kuwepo kwa mahitaji ya msingi katika vijiji hivyo na vijiji vya ng’ambo ya mto  Kiwila vijiji vya kapeta na Mwalisi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanakijiji hao wanasema kukosekana kwa daraja la mto Kiwila, ni tatizo kubwa kwao, kwani wamekuwa wakipoteza ndugu zao ambao wakiwa katika hali ya kuvuka wanajikuta wakichukuliwa na maji.

kiwila-mto

Kaisi Anyigulile mkazi wa kijiji cha Masoko anasema mwaka 2007 walimpoteza kijana mwenzao Obeth Asubisye, ambaye alikuwa akiendesha mtumbwi kuelekea kijiji cha Mwalisi ambapo mtumbwi aliokuwa akiutumia ukazama na kumfanya ashindwe kufanya chochote na kupoteza maisha..

Anasema haikushia hapo kwani mwaka 2010,  Anyelwisye Cheyo mkazi wa kijiji cha Mwalisi naye alizama na mtumbwi akiwa anatokea kijiji cha Lema ambako kulikuwa na mnada, lakini hakufika nyumbani kwani maisha yake yaliishia mto Kiwila.

“Ilikuwa ni huzuni kubwa kwani watu wa vijiji vinne tulisaidiana kumtafuta na hatimaye akapatikana baada ya siku tano” anaeleza Kaisi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kitongoji  cha Mwati, kilichopo katika kijiji cha Masoko  Ally Mwafyela, anathibisha kuwepo kwa vifo vinavyotokana na maji ya mto Kiwila, anasema wanasubiri ahadi ya mbunge wao ya kujengewa daraja iliyotolewa mwaka 2010.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *