Picha mbili zinauonesha mto Songwe ambao unaanzia kwenye milima ya Umalila mkoani Mbeya na kumwaga maji yake ziwa Rukwa kupitia Bonde la Songwe Chunya Mbeya.
Mto huo ambao ndiyo pekee unaomwaga maji yake ziwa Rukwa upo katika hatari ya kukauka na kupotea kutokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na idadi kubwa ya mifugo kwenye Bonde la Songwe.
Mifugo hiyo ambayo ina kunywa maji kwenye mto huo imesababisha mto huo kujaa mchanga na udongo na kusababisha makorongo makubwa kutokana na mmomonyoko wa udongo wakati wa mvua.
Picha ya tatu inaonesha athari za momonyoko wa udongo kuelekea mto Songwe ambazo zinasababisha makorongo