Hapa ni Ikulu ya Rais wa Msumbiji

Albano Midelo

Hapa ni mahali ambapo ni muhimu katika historia ya nchi ya Msumbiji.Eneo hili linaitwa Congresso lililopo katika mkoa wa Niassa ,ambako ulifanyika mkutano wa pili wa harakati za ukombozi nchini Msumbiji mwaka 1968 ambao ulifanikiwa nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1975.Nyumba hii ndiyo mahali ambako Rais wa Msumbiji akifika analala yaani Ikulu ambayo imejengwa katika mazingira ya asili.Hapa pia ni nyumba ambayo imejengwa katika eneo la Congresso mkoa wa Niassa nchini Msumbiji .Nyumba hii ni kwa ajili ya kulala mawaziri wanapotembelea eneo hilo la kihistoria na makumbusho ya Taifa ya nchi hiyo.Pia kuna nyumba za kulala wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi hiyo wanaotembelea kuona makumbusho ya nchi hiyo.Gharama ya kulala kwa siku moja ni shilingi 25,000.

6 Comments
  • hii inaonyesha jinsi gani hao wenzentu wapo makini katika kuhifadhi mambo ya kale hivyo naomba nasisi watanzania tuwaige hao wenzetu

  • tutaweza wapi ndugu yangu mana uzungu tutamwachia nani? ila inapendeza, natamani iwe hivyo hapa kwetu.ukiheshimu utam,aduni wako wengine watauheshimu pia, na hakuna kitu kizuri kama kuthamini chako, wa TZ porojo nyingi, kuiga tunaweza sana hadi wenye navyo wnaonekana cha mtoto!

  • ikopoa ikulu na inafaa kutunzwa na maraisi wa ikulu za nchi nyingine zina faa kuwa za kihistoria kama hiyo………good one MSUMBIJI

  • Jamani wa Tanzania ebu tujifunze kutoka kwa wenzetu hawa wa Msumbiji; hakika huu ni mfano mzuri wa kuigwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *