Mvua Kubwa kuendelea kunyesha Dar hadi Jumamosi; hali kuzidi kuwa mbaya!

Jamii Africa

Mvua kubwa ambayo imeanza kunyesha siku ya Jumatatu Jijini Dar itaendelea kunyesha ikiambatana na ngurumo na radi kubwa hadi usiku wa Jumamosi kuamkia Krismasi siku ya Jumapili. Mvua hiyo kubwa ambayo tayari imesababisha mafuriko sehemu mbalimbali za jiji la Dar pamoja na kusababisha maafa inatarajiwa kuendelea kuja na madhara makubwa kwa maisha ya watu, vitu na miundombinu. Utabiri wa hali ya hewa unaonesha kuwa Joto litaendelea kuwa kubwa wakati huu wa mvua huu na hivyo kufanya hali kuwa tata na tete zaidi kwa watu, wanyama na mazao.

Tayari taarifa za watu kupoteza maisha zimepatikana huku watu wengi wakijikuta hawana makazi kutokana na mvua hizi na kwa kadiri zinavyoendelea ndivyo ambavyo zinazidi kusababisha madhara. Jiji la Dar-es-Salaam ambalo ndilo jiji kubwa nchini halina mfumo mzuri wa kuzuia majanga au uokoaji kulinganisha na idadi ya watu wake na hivyo kutegemea sana vyombo vya Kijeshi ambavyo taarifa zinadokeza tayari vimeanza kazi za uokoaji.

Ushauri ambao unatolewa kwa wananchi ni kuwa kama hauna sababu ya kwenda katikati ya Jiji au mahali pengine ni bora utulie nyumbani ili kupunguza msongamano na vile vile kusaidia hali ya uokoaji kwani ukiondoa watu ambao tayari wanashida ya makazi watu kadhaa wamesharipotiwa kujikuta wakikwama kwenye magari yao barabarani wengi wao wakitumaini labda mvua itaachia baada ya muda wakati mvua hii ni ya kudumu kwa karibu siku tano mfululizo.

 

Hali ya Utabiri wa Hali ya hewa uko hivi:

 

Dar es Salaam, TZ Forecast – 12/21/2011 1:29 am [ °F / °C ]
Wed Thu Fri Sat Sun

T-storms
Hi 31°
Lo 25°

T-storms
Hi 30°
Lo 26°

T-storms
Hi 31°
Lo 25°

T-storms
Hi 31°
Lo 23°

Partly Cloudy
Hi 33°
Lo 22°
 Currently Almanac
observed at HTKI
NA
NA° at
00:00
Apparent NA°
Dew Point NA°
Humidity NA%
Wind NA/NA
Visibility NA
Barometer NA
Sunrise 6:08 am
Sunset 6:33 pm
Avg. Hi 30.0°
Avg. Lo 24.0°
Yesterday Hi NA°
Yesterday Lo NA°
Kutoka Kwiqast.comNa. M. M. Mwanakijiji

 

 

 

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *