Polisi watembeza kipigo Dodoma; nyumba za bomolewa

Jamii Africa

Kuna vurugu zinaendelea kati ya polisi na wananchi huko Dodoma baada ya jeshi la polisi kufika katika eneo la kijiji cha Chadengwa katika kusimamia utekelezaji wa kampeni ya bomoa bomoa. Kwa mujibu wa habari kutoka Dodoma wananchi wa eneo hilo walikuwa na kesi mahakamani ambayo ilizuia nyumba zao kubomolewa lakini mapema asubuyi magreda ya kubomoa yalifika eneo hilo nakuanza kazi hiyo ya kubomoa bomoa.

 

Hata hivyo haieleweki kwa kina mazingira ya ubomoaji huo kwani wananchi walicharuka na kuanza kupambana na polisi. Kuna taarifa kuwa wapo watu waliojeruhiwa na wengine kufa japo taarifa hizo bado hazijathibitishwa hadi hivi sasa. Tutaendelea kufuatilia na kuwajuza.

1 Comment
  • Bomoabomoa kama hii ilifanyika Dar maeneo ya Tabata. Kwa kiasi fulani mazingira yanafanana japo kwa kesi ya tabata walifika Mahakama KUU na hii ya wananchi wa NJEDENGWA hapa Dodoma ilifika mahakama ya ardhi na kwamba tayari waathirika walikuwa wamekata rufaa. Iweje wabomolewe kinyama namna hii na serikali ikae kimya? kama ubomoaji wa Tbata Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala alisimamishwa kazi na waathirika walipewa viwnja, iweje ubomoaji huu wa NJEDENGWA mkurugenzi wa Manispaa ya Dododma bado anakula kuku na serikali imekuwa bubu?

    Na je hawa wananchi wa Dododma si watanzania? Au wananchi ni wakazi wa Dar tu na wengine wanyama?

    Kuna nini katika hili? nani anataka kutuchafulia Dododma yetu?

    Wabunge mpo wapi kuishinikiza serikali kuunda tume? Au ni kwa vile ninyi hamna maslahi na jambo hili?

    Waandishi mpo wapi kuandika habari za kina na za kiuchunguzi juu ya hili? Au nanyi ni bensera fuata upepo? Nadhani ingetokea wanakoishi watanzania huko DAR mngeandika. Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma mko wapi? Au ninyi mnasubiri mialiko yenye mshiko na mnuso tu? KaMA NDIVYO, HIZI HABARI ZENYE MNUKO WA RISASI , DAMU NA RUSHWA ZITAANDIKWA NA AKINA NANI?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *