WENZANGU wa MAJI YA CHAI- wazee wa kumiliki viumbe na vyombo vya angani, wajomba zangu KIKATITI wana wa visima na mwaka , wakubwa wa KINGORI wale watu jasiri sana waliopambania ardhi yao ,LEGURUKI wazee wa Kukarabati nyakati, NGARENANYUKI wamiliki wa maji wa karne hii,NGWARANGA wasiookotwa na maneno mboga… , NKORUA kikosi cha kupambana na haramia wa mashambani, MBUGUNI wazee wa Vito nyepesi ila gharama (Zairwaa), SINGISI wenye vijiji vya haki,AKERI watu wasiobahatisha na hali za Milima,KIKWE watu watulivu wa kuaminiwa washikao dini ,SONGORO yenye wazee warefu wenye kuona mbali na karibu, na maeneo mengine ya..USA.. Mji uliopendwa na Benjamin Franklin kabla ya sehemu ya mji huo haijatokomea ardhini 1863..
Kwa Muda wa wiki Tatu, sehemu kubwa ya mji wetu huu, ARUMERU MASHARIKI umegubikwa ugeni wa makundi ya watu wa aina na rangi tofauti. na Haijawahi kutokea Hivi kwenye Historia ya Mji huu. Hii yote ni kwa sababu ya turufu tuliyoishika mkononi na wageni hawa wanataka tuicheze
jumapili ya tarehe moja. si kucheza turufu hii kunakoleta maana ila wapi pa kuicheza. wageni hawa wametuomba, wametubembeleza, wametulazimisha na wengine kutushurutisha tuicheze kwa faida ya kundi lao..
Ni wazi yako mabaya na mazuri ya ugeni mzito huu.. miongoni mwao ni matusi.. Tumetukanywa, tumechambwa, tumedhalilishwa .. ingawa wao wanasema walikuwa wanatukanana wao kwa wao lakini Tusi kamtukane aliyekutusi sasa tusi unatukana mbele ya asiyekutukana si kutukanywa huko?, akina mama.. mimba zimefanywa katuni kwanye majukwaa na wageni hawa. Tumesikia, tumevumilia na sasa tunahesabu madakika.. wanasema ni kampeni za Kisiasa.. si hivyo hata kidogo, ingelikuwa ni kisiasa ndani ya jimbo letu si wangetuachia wenyewe tufanye tujuacho, kwani watu wetu hawana midomo? kwanini waje kutusemea wao.. ok basi bora wangetusemea lakini si kututusi, nasi ni raia halali wa Jamhuri tunaohitaji kuheshiwa sisi na familia zetu na si kutukanywa!!
Mbali na Mabaya Tunakiri kuna neema kiasi imetokea, mara tatu au nne vijana wetu wa bodaboda wamejaziwa mafuta kwenye tukutuku zao na kupewa cash ya siku Tsh20,000. kinabibi, babu, na wazee wengi wamepewa viruzuku .. ukipata Tsh20,000 unakunywa pombe za kienyeji karibia mwezi mzima ukitunza bajeti yako..pia kuna watu wamepata nguo mpya za kutokea zenye rangu ya migomba na t-shirt rangi ya ndizi zilizoiva, ambazo ni za kutokea siku za sherehe au kwendea kwenye nyumba za ibaada.
Hatukusimuliwa kadhia iliyotupata, Tumeona, tumeshuhudia na tuna kila sababu sasa wana Arumeru ya kufanya, kufanya jambo, jambo moja, jambo moja Tu, Sababu ya kufanya jambo Hilo ..TUNAYO, Nguvu ya kufanya ….TUNAYO na Nia ya kufanya Vilevile ..TUNAYO.. TUTAFANYA..Tunataka Dunia Ijue, Viongozi wa Nchi hii wajue, na Raia wazalendo wa Kweli wa nchi hii wajue kwamba Ingawa sisi ni maskini wa kipato, lakini hatuko tayari KUDANGANYWA TENA.. IMETOSHA!!..
Tumebakiwa Na Dakika.. Tumeahidi kutoa mshtuko.. Kwamba hata Kama kutakuwa Na uchakachuaji .. Haitawezekana.. Tunayo fimbo mkononi.. Tutawachapa..watachapika.. Arumeru si mji wa mabwege wanaoburuzwa Kwa nguvu za shilingi.. Tuliahidi kuzivaa nguo zao.. Tumezivaa.. Tuliahidi kutokataa pesa Yao of which ni Yetu waliyotunyang’anya, Na tumezipokea, kanga zimevaliwa, malori tumeyapanda sana Na radhim matusi tumeyabeba hapanashaka.. Lakini kichapo tutakitoa.. Kesho Nyangumi atapatiwa dozi yake stahili Na Ujinga nchini UTAKOMA.. Kijana wetu, ingaIwa Meru ni sehemu ya nyumbani kwako, Na ingawa Makazi yako ya Kudumu ni Mbezi DSM, sisi hatuna Ubaya Na wewe.. Tutaendelea kukukaribisha Hapa kwetu Kama mtalii.. Tumeishi Na Nyamgumi miaka 50 sasa, amepiga kelele kwamba yeye ni zaidi ya fahari wote wa Baharini.. Kumbe amekuwa akitudanganya maskini sisi, ametunyang’anya hata kile tulichopewa Na Mola kama tunu ya zawadi yetu.. Katuhadaa, katudhalilisha Na kudiriki kututukana wazi wazi.. Tunasema lazima AADHIBIWE.. Kama hutaki tumuadhibu Basi tutakuadhibu na wewe pia..
Kutoka Jamiiforums.com
http://www.jamiiforums.com/chaguzi-ndogo/242150-rai-ya-salma2015-kwetu-wana-arumeru.html