Soko letu limekuwa likiwanufaisha zaidi wageni na wananchi wa nchi jirani ambao hulitumia kikamilifu kujinufaisha na wazalendo wengi kutoelewa nini kinachoendelea. Kwa wale waliokwisha jitosa, huwezi amaini jinsi wanavonufaika na kuwekeza zaidi na zaidi.
Leo kidogo tutupe jicho kwenye hii sekta ya hisa… Si sekta ngeni sana ila kwa hapa nchini wananchi wengi hawajaigundua na kushiriki kikamilifu kama nchi jirani na Tanzania. Wenzetu Kenya wamejitahidi kwenye ushiriki wa soko lao la Hisa la Nairobi (Nairobi Stock Exchange). Na kwa Afrika Mashariki, hili Soko la Hisa la Nairobi ndilo soko kubwa kuliko yote.
Soko letu la hisa la Dar es Salaam (DSE) japo kila siku limekumbatia usemi ni soko geni nchini, lina zaidi ya miaka 15 tangu lianze kufanya biashara mwaka 1998 mwezi wa Aprili. Kwa muda wote huu wa miaka 15 soko limekuwa halina ukuaji wa kuridhisha wala kuvutia. Mpaka leo 2013 kampuni zilizojisajili ni 17 tu, (Soma hapa zaidi http://www.dse.co.tz/main/index.php?page=5) Idadi ya wananci wanaoshiriki kuuza na kununua hisa bado ni ndogo sana na uelewa wa jamii juu ya hili soko ni mdogo sana!
Pamoja na changamoto zake, hili soko lina faida kubwa kwa wale walioligundua na wanaoendelea kulitumia. Kuna mjasiriamali mmoja, yeye alinunua hisa za Twiga mwishoni mwa miaka ya 90 au mwanzoni mwa miaka ya 2000 zikiwa zinauzwa kati ya 200-300 kwa kipande. Leo hii kipande hicho hicho cha Twiga Cement kinauzwa kati ya 2500-2006 kiasi cha miaka 13 tu mbele.
Mdau huyu wa soko hilo anakiri kama angejua ukuaji ni wa kiasi hiki basi angenunua zaidi ya hizo alizonunuaga. Na ameendelea kuongeza vipande vyake kila awezapo. Anadai yeye hupenda kuwekeza kwenye hisa sababu hakuna usumbufu wa uendeshaji . Ukishanunua hisa unakaa na kungoja zipande ama zishuke ili na wewe uuze za kwako. Anakiri kuwa soko hili limemnufaisha sana na anawashauri wengine wajiunge nalo wapate kunufaika pia.
Wengi wetu wenye mitaji midogo midogo tunaweza kunufaika kwa kujiunga na hili soko la hisa la Dar es Salaam na kununua vipande kwa pesa tuliyonayo. Vipande vingi vimeonesha kupanda thamani yake ikiwemo hisa za makampuni ya bia (TBL na SBL), Saruji (Twiga na Simba ) na Bank kama NMB. Kama mwekezaji mzalendo, ukijitosa ukanunua hisa zako za 2,000,000 leo, baada ya miaka 4 unaweza kuziuza hata kwa faida kubwa tu bila kuteseka na usumbufu wa uendeshaji kama zilivyo biashara nyingine.
Upande wa pili soko hili la hisa pia lina magumu yake kama kupotea kwa mtaji wako kutokana na kushuka kwa thamani ya vipande. Hili kwa mfano, limewaathiri wawekezaji walionunua hisa za CRDB na TOL ambazo zimekuwa zikikumbwa na kushuka kwa thamani mara kwa mara. Muhimu ni kuwa makini tu kwa kuchagua vyema ni hisa zipi ununue na kampuni ipi uwekeze.
Soko letu limekuwa likiwanufaisha zaidi wageni na wananchi wa nchi jirani ambao hulitumia kikamilifu kujinufaisha na wazalendo wengi kutoelewa nini kinachoendelea. Kwa wale waliokwisha jitosa, huwezi amaini jinsi wanavonufaika na kuwekeza zaidi na zaidi.
Huu ni wito wangu kwenu wazalendo wenzangu, mkajiunge na soko la hisa la Dar es Salaam na kufaidi matunda yake!
Changamoto yako kwa watanzania kushiriki katika soko la hisa ni nzuri. Ni kweli kabisa ushiriki wao una faida kubwa bila kuvuja jasho jingi la uendeshaji na ufuatiliaji. Lakini ni wazi kwamba ukiritimba uliojengwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa soko hilo, unachangia ushiriki mdogo wa wananchi katika soko hilo.
Hivi kuna sababu gani mpaka leo hii, miaka 15 toka soko lianzishwe tun- kampuni za madalali tano tu (stockbrokers). Je madalali hawa, wana mtandao wa kufika nchi nzima? Mtu wa Shinyanga au Katavi, akitaka kununua hisa katika soko hilo analazimika kuwatafuta madalali hao watano tu ambao ofisi zao hazijatapakaa nchi nzima.
Ushauri wangu, ni bora tuachane na ukiritimba katika uendeshaji wa soko. Zisajiliwe kampuni nyingi zaidi za madalali. Ikibidi yawekwe masharti mahususi kwamba vipaumbele vya usajili wa madalali vitatolewa kwa wale watakao operate kwenye mikoa ambayo haina huduma yao. Tjifunze kwa jirani zetu- Kenya na Uganda…..Mabenki yenye mitandao nchi nzima yamesajiliwa kuuza hisa za soko la hisa….kwanini sisi hatufanyi hivyo? NMB, NBC,CRDB,Postal Bank,Exim Bank zikiruhusiwa kuuza hisa, maeneo mengi ya nchi yetu yatapata huduma hiyo. Hivi kama leo hii Halmashauri ya Bukoba inatumia mtandao wa benki ya Posta kuuza viwanja vyake, na wanafanikiwa….iweje soko la hisa washindwe kutumia mtandao wa aina hiyo?
Lakini lingine, soko la hisa wafikirie matumizi ya teknolojia katika kurahisisha kazi zao. Hivi leo hii kama makampuni ya huduma mbalimbali kama umeme, maji nk wanatumia teknolojia ya Mpesa, airtel money na tigo pesa kulipia huduma zao, iweje soko la hisa washindwe kutumia platform hiyo kuwafikia wananchi wengi zaidi?
Mimi ninadhani uongozi wa soko la hisa una weakness ya kuwa na innovation ya kuboresha utendaji wao. Waende jirani pale Kenya wala sio Wall Street, wakajifunze.
Pole na kazi. Nikiwa mfanyakazi wa kipato cha kawaida, ningependa kupata maelekezo – ni wapi au nimuone nani ambaye atanipa maelezo ya jinsi ya kujiunga na soko la hisa?