Songea: Dawa za binadamu zasafirishwa kwa Pikipiki kutokana na ubovu wa barabara

Mariam Mkumbaru

Ubovu wa barabra katika Kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Wilaya ya Songea  katika Mkoa wa Ruvuma, unachangia usafirishaji wa madawa ya binadamu kwa kutumia pikipiki ya kukodi.

Usafirishaji wa madawa mbalimbali ya binadamu hufanyika kila mwezi baada ya madawa hayo kuisha katika zahanati hiyo.

Nikiwa katika msafara wa kuelekea kijijini Ifinga  ambako ni zaidi ya kilometa 48 kutoka barabara kuu ya kwenda Songea, pamoja na mwenyeji wangu Mganga wa zahanati ya Ifinga Tobias Millinga, huku tukiwa tumebeba madawa ya matumizi ya binadamu katika pikipiki tuliokodi.

“Nimezoeya kusafirisha madawa kwa njia ya pikipiki kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na husafiri kwa saa 4 hadi 5 kufika Ifinga, husafirishaji wa madawa haya sio salama kwa sababu muda mwengine dripu zinapasuka na kulowesha baadhi ya madawa ya vidonge, nikifika kijijini huishia kuyatupa madawa yaliyoharibika kwa kulewa,”alisema Mganga Millinga.

pikipiki-kazi

Pikipiki kukodi kutoka Kijiji cha Madaba hadi Ifinga ni Tsh.30,000, pesa ambayo napewa kusafirishia madawa hayo, kuna wakati sipewi pesa ya kusafirisha madawa, huwa natumia pesa yangu mwenyewe kitu ambacho kinachangia maisha ya familia yangu kuwa magumu.

Millinga alisema kuwa hata upatikanaji wa dawa hizo ni tatizo kubwa sana, huchukua siku 4 hadi 7 nikisubiri kupewa dawa hizo na Katibu wa Jimbo Mama Lugongo ambaye ndiye anasimamia zahanati mbalimbali Songea.

“Nashindwa kutoa taalifa mapema ya kuniandalia madawa kwa sababu Kijiji cha Ifinga hakuna mawasilino ya simu, madawa yakiisha inanibidi kupanda roli au kukodi pikipiki mpaka Madaba kisha napanda gali mpaka Songea mjini, unatumia muda mwingi kusubiri kupatiwa madawa na wakati mwengine huwa naishiwa pesa ya chakula na pesa ya kulala nyumba za wageni,”alisema Millinga

Madawa hayo yakifika katika kijiji cha Ifinga huwa yanauzwa kwa wanakijiji mbalimbali, kitu ambacho kinachangia vifo vya makusudi kwa watoto wa chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee, kwa kushindwa kulipia pesa ya matibabu katika zahanati hiyo.

“Tunashukuru  kwa  kuwepo  kwa  zahanati  hii lakini  pesa  tunayotozwa ukiumwa  ni nyingi  sana  kama  mtoto  anaumwa  maralia  akiwekewa  dripu  yenye  Kwinini  ni Tshs. 8000 kwa mtoto wa chini ya umri wa miaka mitano,” alisema John Ndunguru.

Hali halisi ya kipato cha mwanakijiji wa Ifinga ni Tshs. 500 kwa siku pesa hiyo haipati mpaka apike pombe za nafaka kama mpunga, mahindi, ndizi, mtama na ulezi, akiuza ndio anauhakika wa kupa kiasi hicho cha pesa.

Mtoto akiumwa maralia inakuwa  tatizo kubwa kumpeleka katika zahanati hiyo ya Mission kwa sababu ya ghalama zake kuwa juu, tunamchemshia mti wa mwarobaini na kunywesha ilia pone.

safar-pikipiki

“Hapa nilipo naumwa nimefanyiwa upasuaji wa henia  toka mwezi Agosti dawa nilizokuwa nazo zimekwisha nimefika katika zahanati hii kununua   dawa na nimetembea kwa saa 4 kutoka jitongoji cha ruhuji kuwa ajili ya dawa, upasuaji huu nimelipia Tshs. 100,000 wakati daftari la kutibiwa     bure ninalo ambalo limegongwa mhuri,”alisema mzee Rwanda ambaye anamiaka 68 kwa sasa.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songea Dokta Daniel Masawe, alikili kuwepo na tatizo la watoto, wazee na wamama wajawazito kutozwa pesa za matibabu wakifika katika zahanati hiyo, tatizo kubwa ya kulipia huduma ni zahanati hiyo kuwepo chini ya uwongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea.

“Tumepata malalamiko katika zahanati mbalimbali ambazo ziko chini ya Kanisa Katoliki wanakijiji kulipishwa pesa za matibabu, tumeanza kulifanyia kazi suala hilo kwa kuandika mkataba  maalumu wa makubaliano kati ya serikali na uwongozi wa Kanisa juu ya utaratibu wa kutoa huduma sawasawa na zahanati za serikali, mkataba huo ukikamilika huduma kwa jamii itakuwa bure,” alisema Dokta Masawe.

Kwa sasa zaidi ya zahanati 14  na Hospitali moja ya Peremiho ziko chini ya Kanisa Katoliki, zahanati hizo ni Ifinga, Mkongotema, Mpitimbi, Morogoro, Mhalula, Chipole, Liganga, Jkt Mlali, Mtangimbole, Mahanje, mpangindo, ndongosi Matimila, zimejengwa sehemu ambazo serikali wameshindwa kujenga zahanati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *