Gumzo Mitaani

Jamii Africa
Tanil Somaiya

tanil-somaiya

Ilikuwa ni siku ya Desemba 9, 2010. Tanzania ilikuwa inasherehekea miaka 49 ya Uhuru wa taifa. Baada ya kukagua gwaride Uwanja wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete alifanya dhifa ya kitaifa Ikulu na kualika viongozi wa serikali, mabalozi, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakuu.

Waalikwa wote, walikuwa wanaingia Ikulu kupitia mlango wa nyuma ulio karibu na bahari upande wa ferry. Lango kuu la kuingia Ikulu lilikuwa halitumiki kwa wageni siku hiyo na lilitumiwa na Rais na viongozi wengine wakuu. Magari yote, ikiwemo ya mawaziri na mabalozi yalipaki nje ya Ikulu kwenye uwanja mkubwa ulio karibu na ferry na wageni waalikwa waliingia kwa mguu kwenye viwanja vya Ikulu.

Mmoja wa wageni waalikwa mashuhuri wa Kikwete alikuwa ni Tanil Somaiya, mmiliki wa Shivacom Group of Companies.

Wakati mawaziri na mabalozi waliambiwa na maafisa usalama Ikulu watumie mlango wa nyuma wa kuingia Ikulu na kutembea mpaka kwenye gardens ambako sherehe ilifanyika, Tanil alipewa heshima ya kipekee na kuruhusiwa kutumia main entrance gate.

Tanil aliingia Ikulu na gari la kifahari jekundu (a red FERRARI) na kuipaki gari hiyo kwenye mlango mkuu wa kuingia IKULU ambako huwa gari la Rais ndipo linapaki.

Aliiacha FERRARI hiyo hapo kwenye lango la kuingia Ikulu kwa zaidi ya masaa mawili huku akijimwaga kwenye dhifa.

Mawaziri, mabalozi na vigogo wengine walibaki wamepigwa na butwaa iwaje wageni wote waambiwe waingie Ikulu kupitia mlango wa nyuma kwa mguu na kuacha magari yao nje halafu mfanyabiashara huyu apite main gate na kuweka gari lake kwenye main entrance ya lango kuu la kuingia Ikulu.

Tanil ni rafiki wa karibu na business partner wa Shailesh Vithlani, mfanyabiashara ambaye amekimbia nchi kutokana na kashfa ya rada.

Tanil, ambaye ametajwa kwenye WikiLeaks kuhusu rada, amehusishwa pamoja na Vithlani kwenye kashfa ya rada, military trucks, military choppers, Gulfstream presidential jet na scandal nyingine.

Inaeleweka kuwa Tanil alimchangia pesa nyingi sana Kikwete kwenye uchaguzi wa Rais uliopita na pia alitoa helikopta zake zitumike kwenye kampeni ya CCM, lakini hii ndivyo Ikulu ya Mwalimu Julius Nyerere inavyodharauliwa siku hizi?

Kwa kutumia main entrance na kupaki gari lake mbele ya lango kuu la Ikulu, Tanil alikuwa anataka kuwaonesha wageni wote kuwa yeye yuko karibu sana na Rais wa nchi na Ikulu ni kama nyumbani kwake.

Mbaya zaidi, kufuru hii ilifanywa siku ambayo Tanzania inaadhimisha uhuru wake. Kuna uhuru kamili kweli kama watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wanafanya kufuru namna hii mpaka IKULU?

Unatarajia kweli Edward Hoseah wa PCCB anaweza kuondokana na uoga wa kumkamata Tanil kwa ufisadi wa rada wakati Rais wa nchi ni besti wake na Ikulu ni kama playground yake?

1 Comment
  • TEH TEH TEH,HII HABARI KWELI INASISIMUA NA INATISHIA AMANI YA TANZANIA,YAANI NI KAMA NAANGALIA MOVIE VILE,SASA HAPA MKIDODOSA SANA MTAAMBIWA PARKING ZILIKUWA ZIMEISHA JAMAA AKAAMUA KUTINGA MLANGO WA MBELE,TEH TEH TEH

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *