“Ngono ni chemchemi ya ujana”. Anasema hivyo mwanasaikolojia wa Uingereza, ambaye anadai kwamba watu ambao huushughulisha mwili huonekana miaka mitano mpaka saba wadogo kuliko wale ambao hawafanyi hivyo.
"Ujumbe wangu ni kwamba kufanya ngono ni vizuri," Dk. David Weeks aliiambia Jumuia ya Saikolojia Uingereza.
Mkuu wa zamani wa saikolojia ya wazee katika Hospital ya Edinburgh, Uingereza – Weeks alisema alitumia muongo akitafiti maisha binafsi ya maelfu ya wanaume na wanawake wa umri wote.
Weeks aligundua kuwa furaha ya kujamiana ni "kitu muhimu" katika kuhifadhi ujana. Jinsi gani? Kujamiana hutoa homoni ya ukuaji wa binadamu, ambayo husaidia kutunza ngozi, hivyo kupunguza uwezekano wa ngozi kusinyaa (kuwa na makunyanzi).
Kujamiana pia hutoa ‘endorphins’ ambazo ni kemikali inayofanya mwili kujisikia vizuri; na dawa za asili za kutuliza maumivu ambazo hupunguza wasiwasi na hufanya iwe rahisi kusinzia, Weeks aliongeza. Kemikali hizo hufanyizwa kwenye ubongo na mfumo wa fahamu kiujumla.
Kujamiana kunaongeza mzunguko wa damu, ambayo ni nzuri kwa moyo na hufanya ngozi kuwa na muonekano mzuri na wenye afya, daktari mzuri.
Anaeleza kuwa kujamiana hufanya mwili kuchoma mafuta na kutoa kemikali zingine zinazoimarisha mfumo wa kinga, alisema.
Weeks, ambaye yeye mwenyewe ana muonekano wa kijana ingawa ana umri wa miaka 59, alisema kufanya ngono ni vizuri kwa watu wazima.
"Ni dhahiri kuwa ngono si burudani maalumu kwa vijana tu na haiwezi kuwa hivyo," alisema na kuongeza; "kuridhika kimapenzi ni sababu kubwa ya ubora wa maisha."
Chapisho la hivi karibuni kutoka http://www.mensJournal.com lilisema kuwa kufikia mshindo ni chemchem ya ujana.
Ugonjwa wa moyo, kansa na sababu kadhaa za mazingira, huchangia vifo kwa wanaume wengi, ila kufanya ngono husaidia kupunguza vifo hivyo. Na wanasayansi wengi wanaamini kwamba kufanya ngono zaidi kunarefusha maisha.
Kwa mujibu wa Michael Roizen, daktari mwenye umri wa miaka 62 ambaye ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wellness katika Kliniki ya Cleveland, Marekani, anadai mtu ambaye anafikia mishindo 350 kwa mwaka ana uwezo wa kuishi miaka minnne au zaidi kuliko wengine. Na zaidi ya ziada miaka hiyo minne, Roizen anasema, wanaume hujisikia wadogo miaka minane kuliko rika lao la sasa.
Alipoulizwa kama kuna idadi mahsusi ya mishindo kwa mtu wa kawaida, Roizen anadai kwamba mishindo 700 kwa mwaka inaweza kuongeza hadi miaka minane kwa maisha yako.
Kuna baadhi ya ushahidi kuunga madai ya Roizen. Utafiti uliofanywa Sweden miaka ya 80 uligundua kuwa wazee wenye miaka 70 ambao walifikia miaka 75 walikuwa bado wanafanya ngono, na utafiti wa Chuo Kikuu cha Duke iliyofuata watu 252 wenye zaidi ya miaka 25, ulihitimisha kwamba wingi wa kushiriki ngono ni kiashiria muhimu cha maisha marefu.
Katika utafiti mwingine katika Wales, Uingereza, wanasayansi waliwahoji wanaume karibu 1,000 katika vijiji sita vidogo kuhusu mara ngapi wanashiriki ngono na kutuma rekodi za vifo vyao kwa wanasayansi ili waweze kurekodi urefu wa maisha yao.
Miaka kumi baadaye, walikuta kwamba wanaume ambao walifikia mshindo mara mbili au zaidi kwa wiki walifariki zaidi kuliko wale wemgine ambao hawakufanya ngono kabisa au kufanya mara moja kwa kipindi hicho.
Watafiti wanaeleza zaidi kuwa; "hughuli ya kujamiana au kufanya ngono, kuna faida ya kinga kwenye afya za wanaume.