Takribani wakazi 40 wa kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Wilaya ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma, wanaotumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, (ARVs) wanalazimika kutembea siku nne kufuata dawa hizo.
Licha ya kutembea umbali huo lakini dawa hizo wanazopatiwa zimebainika kuwa ni bandia, Hospitali ya Peramiho ndio waliokamata madawa hayo bandia ya kupunguza makali ya ugonjwa huo maarufu kama ARVs.
Nilipo ongea naye mmoja wa watumia wa dawa hizo, Partina John alisema kuwa natembea siku nne kwenda kituo cha afya madaba ambapo ni zaidi ya kilometa 87 kutoka katika kijiji cha Ifinga hadi katika kituo cha Afya Madaba.
Partina anaishi na virusi vya UKIMWI kwa miaka minne ila mumewe Dominic Haule hana maambukizi; ana watoto wawili nao hawana maambukizi na kwa sasa ni mjamzito
“Nikitoka Ifinga saa 12 asubuhi nafika katika kijiji cha Lunyanya naomba hifadhi nalala asubuhi na mapema naanza safari ya kwenda Madaba kituo cha afya nafika saa 8 mchana, nachukua dawa na kupimwa na lala kesho yake naanza safari ya kurudi ifinga nikifika lunyanya na lala na asubuhi naanza tena safari hadi ifinga”. Alisema Patrina ambaye anatumia dawa kwa miaka 4 sasa.
Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Songea Dokta Daniel Masawe akizungumzia juu ya kuyembea kwa kilometa 87 wa waathirika hao, wanalitambua tatizo hilo na sio kwa kijiji cha Ifinga tu, vijiji vingi vya Songea waathirika wanatembea umbali unaofanana na huo.
Dokta Masawe alisema kuwa, licha ya umbali huo lakini tumekamata madawa mbandia ya kupunguza makali ya ugonjwa huo na kupelekea kupunguza imani kwa waathirika wengi wanaotumia dawa hizo.
“Tumekamata mabox mbalimbali yakiwa yamewekwa madawa bandia ya kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI (ARVs) tumeyateketeza kwa kushirikiana na Hospitali ya Peramiho kabla hayaja wafikia watumiaji,” alisema Dokta Masawe.
Wilaya ya Songea ina vituo 12 vya kutoa dawa za kupunguza makali UKIMWI (ARVs) kati ya hivyo vituo vitatu bado havijasajiliwa. Kitengo cha kupunguza makali ya UKIMWI kwa songea, kinakabiliwa na changamoto ya kuwa na gali moja, inakuwa vigumu kuviratibu vituo vyote na kupeleka dawa kwa wakati.
Kwa sasa anashindwa kwenda mwenyewe kufuata dawa kwa sababu ni mjamzito na anamtuma mumewe kwenda kuchukua dawa hizo, hiyo inachangia kurudisha nyuma afya yake kutokana na kushindwa kupimwa afya yake na kujua kama dawa zinamsaidia au ana tatizo.
Aliomba serikali kuwasogezea dawa hizo kwa karibu ili kuweza kupunguza kutembea kwa muda mrefu kufuata dawa hizo, wanapita porini kuna wanyama wakali na wanadhoofu afya zao kwa kukosa lishe bora akiwa njiani.
Kwa sasa dawa hizo wanawatuma waume zao kwenda kuchukua katika kituo cha afya cha Madaba, na hutumia kwa miezi miwili, zinapokwisha wanawatuma tena waume zao kitu ambacho kinasababisha kutokupimwa afya kwa kutokwenda muaathirika mwenyewe.
Kwa sasa kijiji cha Ifinga kina zaidi ya watu 60 kati ya hao 40 wanatumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI na 20 bado hawajaanza kuchukua dawa hizo, kwa mujibu wa sense ya mwaka huu kijiji hicho kina zaidi ya wakazi 3,220.
Diwani wa Kata hiyo Logatus Kianjali alisema kuwa tayali wamepeleka malalamiko hayo katika kitengo cha UKIMWI ili kuweza kuleta dawa hizo katika zahanati ya mission ili kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa wagonjwa hao.
Kimsingi serikali ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha kuwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi zinapatikana, lakini kinachoonekana ni kuwa haijaweka utaratibu mzuri wa kuzifikisha kila mahali na vijijini ndiko kwenye tatizo kubwa la upatikanaji wa dawa hizo, hapo ndipo uwajibikaji mbaya unapoonekana.