Wagonjwa wanaolazwa katika kituo cha afya cha Kinesi kilichopo kata ya Nyamunga wiayani Rotya, wako hatarini kuambukizwa malaria, kuytokama na kukosekana kwa vyandarua katika wodi mbili, zilizopo katika kituo hicho.
Hayo yameelezwa na muuguzi mkunga wa kituo hicho Nyakibore Bulenga, anasema vyandarua vilivyopo katika wodi ya akinamama na wanaume ni vidogo ikilinganishwa na ukubwa wa vitanda vilivyopo kwenye wodi hizo.
Muuguzi wa kituo cha Kinesi Nyakibore Bulenga, akionyesha chandarua
Anasema vyandarua hivyo huishia katikati ya kitanda na kumfanya mgonjwa aliyelazwa kuumwa na mmbu na kuwa katika hatari ya kuambukizwa malaria.
“Kama unavyoona tuko karibu na ziwa kwa hiyo mmbu ni wengi, hii inatupa hofu kuhusu usalama wa wagonjwa wetu”.
Martha Mpandujii muuguzi katika kituo hicho anasema bado hawajatoa taarifa utawala kuhusu suala hilo, kutokana na matatizo mengi yanayokabili kituo hicho, kama kukosa umeme, maji na vifaa tiba.
Anasema kama kituo wameona kwanza washughulikie matatizo hayo na baadae suala la kukosekana kwa vyandarua vinavyokidhi litafuata.
Kituo hicho cha Kinesi kinahudumia vijiji vya Ruhu, Nyihara, Kinyamisana, Bitilio, Barack na Kibui.
dada hiyo ni wilaya ya Rorya.