Wahariri nchini wametakiwa kuwa makini na kazi zao ili kuepusha kuipotosha jamii na kupigania maendeleo.
Maoni hayo yametolewa muda huu na baadhi ya wahariri hao Jijini Dar es Salaam walipokuwa wakichangia katika mada kuhusu uwajibikaji wa vyombo vya habari Tanzania kwenye kongamano la wadau wa habari lililoandaliwa na Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF).
Akizingumza kuhusu uwajibikaji huo, Mhariri wa gazeti la Kiingereza la Guardian, Richard Mgamba, amesema idadi kubwa ya wahariri nchini hivi sasa wameacha kuwajibika kwa wananchi zaidi ya kuangalia zaidi kutengeneza faida.
Mgamba amesema makosa makubwa yanayotokea sasa katika vyombo vya habari, hasa magazeti yanadhihirisha wazi kuwa wahariri ama wameshindwa kuwajibika au hawana uwezo mkubwa wa kuongoza magazeti.
Amesema mifano hai kuhusu hilo inaweza kuonekana wazi katika mifano ya hivi karibuni ambapo vyombo kadhaa viliandika juu ya kujiuzulu kwa waziri mmoja, lakini haikuwa kweli na kesho yake halikuomba samahani.
“Mbali na tukio hilo, pia gazeti hilo hilo lililoandika kujiuzulu kwa waziri, likaandika tena kwamba Baraza la Mawaziri limewakaanga baadhi ya mawaziri jana, lakini ukweli ni kwamba hakukuwa na kikao cha baraza hilo,” hii ni kuonesha kuwa hakuna uwajibikaji na uongo ndiyo unaotawala kwa sasa.
Mchangiaji mmoja amesema gazeti la Kiingereza la Daily News limeonekana kuwa shabiki mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ba limeshindwa kutoa nafasi sawa kwa vyama vingine vya siasa.
“Tumeona mara nyingi, vyombo vya serikali vikiwaadhibu viongozi wake (wahariri au wakurugenzi) wanapoonekana kuwa upande wa wananchi,” amesema mchangiaji huyo. Katika siku za hivi karibuni, Mkurugrnzi wa TBCI, Tido Mhando alikatishwa ghafla mkataba wake kwa kile kinachoonekana kuwapa nafasi kubwa vyama vya upinzani wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopita.”
Mchangiaji mmoja alisema kuwa wahariri na waandishi wote wa Tanzania wanakula rushwa, amedai kuwa ukiona makala ndefu kwenye magazeti, lazima itakuwa imelipiwa kwa maana kwamba mwandishi na hata mhariri wake watakuwa wamechukua rushwa.
“Mimi siamini kabisa vyombo vya habari Tanzania, kwa kuwa wote wanapokea bahasha ili habari zao zitangazwe au kuandikwa, siamini kabisa,” ameongeza.
Wahariri nchini wametakiwa kuwa makini na kazi zao ili kuepusha kuipotosha jamii na kupigania maendeleo.
Maoni hayo yametolewa muda huu na baadhi ya wahariri hao Jijini Dar es Salaam walipokuwa wakichangia katika mada kuhusu uwajibikaji wa vyombo vya habari Tanzania kwenye kongamano la wadau wa habari lililoandaliwa na Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF).
Akizingumza kuhusu uwajibikaji huo, Mhariri wa gazeti la Kiingereza la Guardian, Richard Mgamba, amesema idadi kubwa ya wahariri nchini hivi sasa wameacha kuwajibika kwa wananchi zaidi ya kuangalia zaidi kutengeneza faida.
Mgamba amesema makosa makubwa yanayotokea sasa katika vyombo vya habari, hasa magazeti yanadhihirisha wazi kuwa wahariri ama wameshindwa kuwajibika auhawana uwezo mkubwa wa kuongoza magazeti.
Amesema mifano hai kuhusu hilo inaweza kuonekana wazi katika mifano ya hivi karibuni ambapo vyombo kadhaa viliandika juu ya kujiuzulu kwa waziri mmoja, lakini haikuwa kweli na kesho yake halikuomba samahani.
“Mbali na tukio hilo, pia gazeti hilo hilo lililoandika kujiuzulu kwa waziri, likaandika tena kwamba Baraza la Mawaziri limewakaanga baadhi ya mawaziri jana, lakini ukweli ni kwamba hakukuwa na kikao cha baraza hilo,” hii ni kuonesha kuwa hakuna uwajibikaji na uongo ndiyo unaotawala kwa sasa.
Mchangiaji mmoja amesema gazeti la Kiingereza la Daily News limeonekana kuwa shabiki mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ba limeshindwa kutoa nafasi sawa kwa vyama vingine vya siasa.
“Tumeona mara nyingi, vyombo vya serikali vikiwaadhibu viongozi wake (wahariri au wakurugenzi) wanapoonekana kuwa upande wa wananchi,” amesema mchangiaji huyo. Katika siku za hivi karibuni, Mkurugrnzi wa TBCI, Tido Mhando alikatishwa ghafla mkataba wake kwa kile kinachoonekana kuwapa nafasi kubwa vyama vya upinzani wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopita.
Hapa na mimi niseme jambo.Wakati wa mazishi ya raia wetu Watanzania waliouwawa na Polisi kinyama ktk maandamano ya CHADEMA yalipomalizika gazeti la Habarileo liliripoti kuwa familia ya marehemu mmojawapo kati ya wawili alikuwa akiitwa Ismail Omari ati ndugu hawakutaka maiti huyo akaagwe ktk uwanja wa NMC unga ltd,baada ya habari hiyo kutoka ndugu hao wakalishukia gazeti la Habarileo kuwa limepotosha uma.Sasa hapo ni nani aliwatuma Habarileo?,au ni mafisadi wa ccm ili chadema ionekane iliwalazimisha hao ndugu kufanya kile hawakukitaka