WAKULIMA wa zao la Tangawizi katika kijiji cha Munzeze kilichopo katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba serekali kuwasaidia kuwapatia pembejeo za kilimo za kisasa kwa mkopo wa bei nafuu ili kuondokana na kilimo cha jembe la mkono wacholima sasa.
Wakizungumza nami kijiji hapo baadhi ya wakulima hao wa zao hilo la Tangawizi walisema kuwa tangawizi ni zao lisilo na gharama katika kuanzia hatua ya kuandaa shamba hadi kufikia kuivuna kwa zao hilo limekuwa likistawi mahali popote penye maji ya kutosha bila ya matatizo hata usipoweka mbolea.
Mkulima wa zao la tangawizi katika kijiji cha Lusesa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma; akiichambua tangawizi yake shambani baada ya kuivuna
Philibeth Ndayasunse ni mkulima wa zao hilo la tangawizi kijiji hapo kwa miaka miwili mpaka sasa yeye alisema kuwa tangawizi ni zao ambalo wanalilima bila ya kutumia gharama kubwa tatizo lao ni wanalima kwa kutumia jembe la mkono hulazimika kulima eneo dogo kwa muda mrefu tofauti na kutumia trekta au power tiller ambazo zinalima eneo kubwa kwa muda mfupi.
“Najua wengi wamezowea kuona tangawizi ikilimwa Tanga, Zanzibar na maeneo mengine; hata sisi huku Kigoma tunalima zao hili tunaomba serekali yetu itukumbuke na sisi wakulima wa zao hili la tangawizi huku munzeze kwa kutupatia mikopo ya pembejeo kwa bei nafuu ili tutoke kwenye kilimo hiki cha jembe la mkono tulime kilimo cha kisasa” alisema mkulima huyo.
Ndayasunse alisema kuwa zao la tangawizi linafaida kubwa ukilima robo heka kama hazijaharibika sana unaweza kuvuna hata gunia kumi ambapo wao wanauza kwa bei ya jumla kilo moja shilingi 1000 kwa bei ya jumla na kwa bei ya rejareja kilo moja ni shilingi 2000 nasoko lao kubwa lipo kigoma mjini na mwanza.
Mkulima huyo aliiomba serekali kuwasaidia wakulima wa zao hilo kijjini hapo pembejeo za kisasa kwa mkopo nafuu kama vile trekta, powertiller kwani hicho ndo kilio chao ili waweze kulima zaidi tangawizi na pia kutoka kwenye jembe la mkono ambalo tija yake ni ndogo sana pia walihitaji zaidi wataalamu wa zao hilo ili waweze kuwapa ujuzi zaidi wa kulima zao hilo la tangawizi.
Ni kweli lakini kichwa cha habari kinazungumzia pembejeo ilhali wakulima wanahitaji zana za kisasa za kilimo,pembejeo ni mbolea, madawa na mbegu. Nakubaliana kabisa kuwa hizo zana za kisasa ni mhimu vilevile na elimu ya uzalishaji sina uhakika sana kama wakulima wetu hao wana uwezo na kanuni bora za kilimo