Wakulima waomba kujengewa maghala ya kisasa

Editha Karlo

WANAKIJIJI wa kijiji cha Lusesa katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma wanaiomba serekali iwasaidia kuwajengea maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao yao baada ya kuvuna ikiwa sambamba na kuwapatia elimu ya kutumia maghala hayo.

Uchunguzi nilioufanya kijijini hapo wa kutaka kujua ni njia zipi wakulima wanazozitumia katika kuhifadhi mazao yao baada ya kuvuna niliweza kugundua njia za kienyeji mbalimbali wanazotumia wakulima hao katika kuhifadhi mazao yao ambazo njia hizo hazina tija yoyote kwao kwani zime kuwa zikiwapatia hasara.
Baadhi ya wakulima kijijini hapo waliongea na mwandishi wa habari hii walisema kuwa asilimia 99 ya wakazi wa kijiji hicho wanategemea  kilimo katika kuendesha maisha yao  lakini pamoja nakuwa wanalima sana lakini wamekuwa hawanufaiki na kilimo hicho kwani wanaishia kupata hasara tu baada ya kuvuna mazao yao kwasababu ya kutumia njia za kienyeji wanapo hifhadhi mazao yao.

Moja ya njia ya kienyeji wanayotumia wanakijiji wa Lusesa katika kuhifadhi mazao yao

Mussa Ndamuhoza ni mkulima wa mahindi na mihogo kijijini hapo yeye anasema kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi katika kuandaa mashamba msimu unafika na gharama kubwa za kununua mbegu na mbolea lakini anapo vuna mazao yake na kuyapeleka nyumbani mengi uharibika kwakuwa njia anazotumia kuhifadhi mazao hayo ni za kienyeji.

“Kwakweli serekali ingetujengea maghala ya kijiji ya kuhifadhia mazao yetu baada ya kuyavuna ili tuweze kuhifadhi mahali salama na ikifika msimu tuuze kwa bei nzuri na yakiwa na hali nzuri serekali isikie kilio chetu hiki” alisema mkulima huyo.

Ndamuhoza alisema kuwa wanakijiji wengi kijiji hapo maisha yao yote wamekuwa wakiyaendesha kwa kutegemea kilimo kwani ndo mkombozi wao,lakini kilimo hicho kimekuwa hakiwa komboi kama wao wanavotegemea kwani wamekuwa wakipata harasa ya kuharibikiwa na mazao au kuozewa kutokana na njia za kienyeji wanazo zitumia katika kuhifadhi mazao hayo baada ya kuyavuna.

Mkulima huyo aliiomba serekali kupitia Wizara ya kilimo na ushirika kutenga fedha kwenye halmashauri yao za kujengea maghala ya kijiji ya kuhifadhia chakula ikiwani sambamba na kuwa tuma wataalamu wa kilimo kwenda kutoa elimu juu ya kutumi njia za kisasa za kuhifadhi mazao yao ili kuepukana na hasara wanayoipata baada ya kuvuna.

Mtendaji wa kijiji cha Lusesa Sadoki Tozwa alikiri kuwa ni kweli wakulima wa kijijini hapo wamekuwa wakitumia njia za kienyeji sana katika kuhifadhi mazao baada ya kuyavuna na kujikuta wakipata hasara karibu kila msimu wa mavuno unapofika kwani mazao yao mengi yamekuwa yakioza na kuwaharibikia manyumbani kabla hata hawajaya peleka sokoni.

Mtendaji huyo alisema kuwa  kijiji chake kina jumla ya wananchi 110,207 ambao asilimia 99 wanaendesha maisha yao ya kila siku kwa kutumia kilimo na kijijini hapo kuna ghala moja tu la kuhifadhia chakula  ambalo bado halijaanza kutumika  kutokana na wingi wa wanakijiji hao najinsi wanavo lima sana chakula kila msimu  ghala hilo moja haliwezi kutoshi kuhifadhia chakula kwa wakulima wote.

Sadoki aliiomba serekali kutuma wataalamu wake wa kilimo kwenda kijijini hapo na kutoa elimu ya kuhifadhi mazao baada ya kuvuna kwani wakulima wengi hawazijui njia za kisasa za kuhifadhi mazao yao baada ya kuyavuna ikiwa ni sambamba na kuwajengea maghala

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *