JE UNAHIFAHAMU WILAYA YA KISARAWE

Belinda Habibu

Wilaya ya Kisarawe ina jumla ya wakazi 95,614 wanawake wakiwa 47,271 na wanaume ni 48,343,kwa mujibu wa sense ya mwaka 2002 ya watu na makazi.
Ongezeko la watu kwa mwaka ni sawa na asilimia 2.1,na kila kaya ina watu wasiozidi wanne,kufikia mwaka 2013 makisio ya watu ni 116,067 wanawake wakiwa 57384 na wanaume 58,683.
Pamoja na ongezeko hilo kipato cha wakazi wake bado ni kidogo kiasi cha sh. 500000/= kwa mwaka na kinachopatikana kutokana na biashara ndogo ndogo,mazao ya misitu (mkaa,asali) na korosho.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hii, Yona Maki alisema pamoja na wakazi wake kufanya shughuli hizo,wapo wawekezaji wakubwa waliowekeza kama katika kiwanda cha simenti cha Kazimzumbwi,mashamba makubwa (Jetropha).
Ameongeza zao la jetropha likiimarishwa litaletea halmashauri hii pato kubwa kwani matumizi yake ni pamoja na utoaji wa mafuta kwaajili ya magari.
Mkurugenzi huyo ameongeza pamoja na mambo mengine pia pato linalopatikana la halmashauri kwa mwaka kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato, asilimia 10 limetengwa kwa kuwawezesha wanawake na vijana wanaojishughulisha na kazi za ujasiliamali.
Alisema lakini ni lazima wawe wamejiunga katika kundi la watu 15 ama 20, watawezeshwa mtaji kutokana na fungu hilo.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

1 Comment
  • Wilaya ya Kisarawe ina jumla ya wakazi 101,598 wanawake wakiwa 50,967 na wanaume ni 50,631 ,kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012 ya watu na makazi.

    Vyanzo vya mapato kwa wakazi ni;  Mkaa, Korosho, Mohogo, Nazi, Magafu, Matunda (Nanasi, Tikiti), Asali, na biashara ndogo ndogo.

    Kisarawe kuna kiwanda kimoja cha saruji (cement) kilichopo Kazimzumbwi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *