CHADEMA yajiachilia mikononi mwa Serikali

Jamii Africa

Freeman MboweChama cha Demokrasia na Maendeleo kimekubali kimsingi kuitegemea serikali ilete mabadiliko ya mswada wa Sheria ya kusimamia mchakato wa Katiba Mpya. Hii ni kufuatia mazungumzo ya siku mbili yaliyohusisha chama hicho na Rais Kikwete Ikulu Jijini Dar-es-Salaam. CHADEMA ilipeleka mapendekezo kwa Rais Kikwete ambayo yalikuwa yanaonesha upungufu mkubwa wa sheria hii matarajio yake ikiwa ni kuweza kumshawishi Rais Kikwete kutosaini sheria hiyo jinsi ilivyo hivi sasa.

Hata hivyo, inaonekana msimamo wa serikali uko pale pale ambapo mabadiliko yoyote yatatakiwa yaletwe Bungeni na hivyo CHADEMA wanatarajia kuona sheria itabadilishwa katika Bunge lijalo la Januari. Hata hivyo haieleweki kama Rais akishapitisha sheria hiyo ataendelea kuteua Tume au atasubiri mabadiliko kwanza. Endapo Rais atateua tume baada ya kupitisha sheria na kabla ya mabadiliko haijaeleweka kama CHADEMA bado watakuwa na imani na serikali.

Ifuatayo ni sehemu ya matangazo ya BBC ambapo Mwandishi wa BBC Eric David Nampesya amezungumza na Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe kuhusiana na yale yaliyokubaliwa.

Na. M. M. Mwanakijiji

SIKILIZA BBC – BONYEZA HAPA

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *