Siku moja nilikuwa nabadilishana mawazo na vijana wenzangu kupitia email yangu, Je kwa siku wanatumia saa ngapi kufikiri? lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza na kusema kuwa angalau kwa mwezi mmoja ana muda wa kukaa chini na kutafakari mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika maisha yao au kwa lugha nyingine mambo yanatokea kwa lolote liwe tu (haphazardly), nilisikitika sana. Nikawa najiuliza sasa je, kama vijana wa sasa wengi tumekosa muda wa kutafakari angalau nusu saa kwa siku je, tunajitakia nini katika maendeleo yetu? sana sana ya kiuchumi ya sasa na ya muda mrefu baadae na yale ya kijamii katika kuyatatua?
Fikiria matajiri duniani kama Bill Gates kwa muda mrefu anatumia muda wa mwenzi mmoja kwenda katika kisiwa na kufikiri ni jinsi gani aendeleze biashara yake. Nilishawahi kuandika makala juu ya kutofikiri leo umempa mtu nafasi akufikirie na kisha kukutawala pasipo wewe kujua. Ndugu yangu binadamu wote ni sawa ila tunafanyaje ili kuutimiza huu usawa? Asilimia 3% ya watu dunia wana malengo (plan) na wameyaandika na asilimia 97% hawana malengo maishani mwao kwa lolote tu lile likitokea nao humo humo yaani kwao kufanikiwa ni bahati. Hii ni kutokana na kukosa muda wa kufikri ili wajikomboe. Sababu hii inasabisha asilimia kubwa sana utaona inatawaliwa na watu wachache sana.
Askofu mkuu wa kanisa la Living faith dunian kutoka Nigeria anasema anatumia muda wake mwingi kufikiri kuliko kusoma biblia na vitabu vingine na kweli ni mmoja wa watu wenye mafanikio sana hapa kwetu Afrika kiuchumi. Waafrika wengi wanapenda kufanikiwa lakini hawana hata sekunde moja ya kutafakari ni kwa njia gani atafikia hayo mafanikio. Kuna mambo mbalimbali niliwahi kujifunza kwa wanazuoni mbalimbali mmoja wapo ni Dr John Maxwell katika kitabu chake cha “Thinking for Change”. Kuna jinsi mbali mbali za kufikiri ambazo zina tija kama ukiwa makini:
1. Kufikiri kwa zingatio moja (ondoa mambo mengine yote); Uwezo wa kufikiri kwa kuondoa mambo yanayochanganya kwenye akili yako.
2. Kufikiri kwa ubunifu; uwezo wa kuvunja sanduku la mipaka yako na kugundua mawazo mapya kabisa.
3. Kufikiri kimkakati; Uwezo wa kutekeleza msisimuko wako na kutumaini kupata ufumbuzi kwa yasiyowezekana
4. Kufikiri kwa uhalisi; uwezo wa kujenga msingi imara juu ya kuweza kufikiri kwa uhakika
5. Kufikiri kiuwezekano; uwezo wa kuelekeza msisimko wako na kutumaini kupata ufumbuzi kwa yasiyo wezekana.
6. Kufikiri kwa kukosoa; uwezo wa kukataa mipaka ya wazo lililozoeleka ili kupata matokeo yasiyoya kawaida
7. Kufikiri kwa pamoja; uwezo wa kuhusisha mawazo ya wengine ili kupata matokeo unganishi
8. Kufikiri kusipo kwa ubinafsi; uwezo wa kuwafikiria wengine na safari yao ili kufanikisha ushirikiano
Mtu anayefikiri ana faida kubwa sana; kwanza huokoa muda mwingi wa ufanyaji jambo kwa kuwa hutumia kanuni ya 20/80 huwa na kujiamini ya kutosha ambapo ni jambo la msingi kuwavutia wengi jambo unalolifanya maana huko ni kurupuka. Ni rahisi sana kuanza kufikiria, anza sasa kupanga muda ambao kila siku utapenda kuwa peke yako na hali ya utulivu ukitafakari muda mzuri. Mara nyingi ni asubuhi alfajiri, usiku sana pale ambapo hakuna usufumbufu.
Watu wanasema mtu asiyekuwa na taarifa (habari) hana tofauti na mnyama anayetembea barabarani lolote lile laweza kumtokea aendako kwa kuwa hana taarifa. Mimi nasema ukiwa haufikirii ni kumpa tikeki mtu anayefikiria kukutawala. Anza sasa kuweka ratiba ya kufikiri kwa siku, sana sana usiku au asubuhi na uufanye moyo wako uwe unatamani kujua mengi mazuri.
Kuna faida nyingi za kufikiri ikiwepo kuongeza thamani ya jambo unalolifanya na pia kuwavutia watu jambo unalolifanya. Anza sasa! anza leo. Maendeleo ya shughuli zetu yanatokana na sisi tunavyofikiria na maendelo ya nchi tulionayo leo hii ni kutokana viongozi wetu walivyofikiria, je, walikuwa makini au walikopi kutoka kwa wengine? unaweza amua leo ukawa kati ya kundi dogo la watu duniani wanafikiria ili usitawaliwe na wengine na uwe na maendeleo, maana ‘blue print’ yako inatokana na wewe unajituma vipi kufikiri.
Mwandishi Deogratius Kilawe ni mfanyabiashara wa Dar es Salaam na mshauri binafsi wa masuala ya biashara.
Anapatikana kwa simu 0717109362
Email: [email protected]
lets now tz,act internationaly
Uko sahihi kaka, lakini bado kuna changamoto nyingi sana, ili ufikiri unahitaji kuwa na wazo, na mara zote wazo jipya lenye chachu ya kufikiri hutokana na taarifa mpya ambazo zimetokea kukuintrest, akili ya binadamu hufanya kazi kwa biddi sana katika mawazo ambayo hayamuumizi mwanafikra.
Sasa jaribu ku-picture maisha harisi na ya ukweli ya mtz wa sasa lets say kwa mfanyakazi ambaye anaamka saa 11 alfajiri ili awahi daladala kumfikisha kazini na kisha kurudi nyumbani saa nne usiku kutokana na foleni, sasa huyu mtu kwa vyovyote atajisikia vizuri kama akistay away from thinking kwa sababu kwake hilo ni maumivu, atahitaji kupumzika ili kesho awahi tena kazini na hayo ndio maisha ya watanzania wafanyakazi na kwa wafanyabiashara nao ndio hivyohivyo hawana chance ya kufikiri sababu sio wazalishaji, wenyewe ni ma-gobetweener kati ya products za nje na wateja wa ndani, kwa hiyo nao wako hivyo fikra zao zimetawaliwa na producer wao ni kununua tu, wakati mwingine huwa nahisi kwamba anyway kila mtu ana akili but u need to be rich to think.
Thanks
Umetoa mfano kwa watu wanaoishi katika miji mikubwa; unawafikiriaje watu walioko vijijini ambao wakiamka asubuhi hawana hata la kufanya zaidi ya kuzurula? Kunya mapombe ya kienyeji n.k.
kaka Deo ahsante sana kwa mawazo yako! Lakini unaweza kufikiri kufanya jambo fulani – mfumo wa kiutawala ukakurudisha nyuma.
Kuna jamaa yangu alikuwa na uwezo wa kutengeneza mizani na kuiuza, ilikuwa inafanya kazi vizuri tu, lakini alikamatwa na kufunguliwa kesi eti hana kibali. Huo ni mfano mmoja tu, yapo mengi ambayo mfumo wetu wa serikali unatufanya tushindwe kufikia malengo yetu!
ni kweli ndugu umesema kweli