Zaidi ya Wanafunzi 890 na walimu 13 wanatumia matundu 16 ya vyoo, shule ya msingi Mwadui DDC, katika kijiji cha Mwadui Lohumbo.
Shule hiyo kongwe yenye miaka 68 ni miongoni mwa shule zinazozunguka mgodi wa almasi wa Williamson Diamond,wilayani Kishapu,mkoani Shinyanga.
Kaimu mwalimu mkuu wa shule hiyo Magreth John,alisema wanamatundu 16 tu,ili yatosheleze yanahitajika mengine zaidi matundu 20.
Mwalimu Magreth amesema pamoja na tatizo hilo pia wanakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa,kwa sasa vipo 9,ambayo yana mrundikano wa wanafunzi wengi na kuathiri uwelewa wao.
“Darasa la pili linawanafunzi 139,la tatu 141,la nne 82,la tano149,la sita 79 na darasa la saba 85.” Alisema.
Ameongeza darasa la kwanza wapo 129 na lengo lilikuwa kuandikisha wanafunzi 145,na kwa upande wa chekechea wako wanafunzi 183.
Alisema ili kuwe na usikivu na wanafunzi waelewe wanahitajika wawe wanafunzi 45,hata mwalimu ataweza kuwasaidia wale wasioelewa mapema.
Mwalimu Magreth alisema wanaupungufu wa nyumba za walimu 11 kwani kwa sasa zipo mbili tu na zimechakaa maana za zamani mno toka enzi ya mkoloni.
Hata hivyo amesema hawana pato kama shule la kuwawezesha kupunguza changamoto hizo ingawa wanapata sh.milioni tatu kwa matumizi mbalimbali ya shule kutoka serikalini,na hazitoshelezi kuweza kutumika katika ujenzi wa madarasa hata vyoo.
Akizungumzia suala la mimba mashuleni,alisema sio sana kutokea katika shule hiyo, ingawa mwaka 2008 alikuwepo mwanafunzi mmoja wa darasa la tano na mwaka 2012 alikuwepo wa darasa la saba.
“Huyu wa darasa la saba hatukufahamu alifanya mtihani,na siku tulipowapima wenzake,yeye alikuwa mgonjwa nyumbani,lakini alifaulu na amejifungua yuko nyumbani hasomi ila nilimtembelea anasema anataka kwenda shule”alisema mwalimu huyo.
Sera ya Elimu ya mwaka 2010 inasema Sera za Elimu na Mafunzo zilijikita zaidi katika kuelekeza uongezaji wa idadi ya wanafunzi shuleni na vyuoni kwa usawa na kukuza ubora wa elimu na mafunzo.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX