Nachingwea: Ardhi yatumika kama Ubao wa kufundishia

Mariam Mkumbaru

Ukosefu wa vibao vya kujifundishia inawalazimu wanafunzi wa awali kuandika katika ardhi, kitu ambacho kinachangia ugumu wa mwanafunzi kuelewa kwa haraka na uwezekano wa kupata magonjwa kama mafua na nyungunyungu.

Hali hiyo imejitokeza katika shule ya msingi ya Kiegei iliyopo katika Kijiji cha Kiegei Kata ya Kiegei Wilaya ya Nanchingwea Mkoa wa Lindi, kwa wanafunzi wa awali kuandika kwenye ardhi.

vibao-ardhi

“Tuna vibao vya kujifunza 20 tu, na kwa sasa tuna wanafunzi 60 ukilinganisha na vibao tulivyonavyo hivitoshi kwa wanafunzi wote kujifunzia kuandika, ukimpa mmoja wengine wanalia inabidi niviwekee tuu na wote kujifunza chini ya ardhi,” alisema Mwalimu Hamza.

Kwa sasa shule haina pesa ya kununua vibao vingine vya kusomea kwa wanafunzi hao wa awali, inawalazimu kusoma kwa kuandika kwenye ardhi mpaka watakapo elewa jinsi ya kuandika ndio wataandika katika madaftari.

“Shule haina pesa ya kununua vibao vya kufundishia watoto, kutokana na ugumu wa maisha kwa huku kijijini na pesa ya korosho hatujalipwa mpaka sasa, pesa ya kula kwa siku ni shida sana tutaweza kupata pesa ya kununua kibao cha kusomea mwanafunzi,” alisema Mchekenje Mwalimu Mkuu  wa shule hiyo.

mwalimu-ubao

Kwa upande wa watoto wanaonekana kuchoka  na wengine kuchubuka vidole, kwa kuandika katika ardhi kwa muda wa saa mbili hadi tatu kitu ambacho kitachangia kutokwenda kwa watoto shuleni hapo kwa kukimbia zoezi hilo la kujifunza kuandika.

Jamadini Mkumbila ni Mjumbe wa Kamati ya Wazazi katika shule ya Msingi Kiegei alisema, kuwa kweli watoto wanajifunza kuandika kwenye ardhi kwa kukosa vibao na kamati ya wazazi ya shule haina pesa ya kununua vibao vya kujifunzia.

Ghalama ya mwanafunzi mmoja wa shule ya awali kwa mwaka ni Tshs. 6000, kutokana na hali halisi ya kipato kwa wakazi wa Kiegei kutolipwa pesa ya korosho, walizokopesha mwaka jana mwezi Oktoba mpaka sasa wanafunzi bado hawajalipa ada ya shule ya awali.

“Tungelipwa pesa zetu za korosho tungelipa ada ya mtoto lakini kwa kutokana na ukata inakuwa ngumu kulipa pesa hiyo kwa sasa ili walimu wanunue vibao vya kujifunzia shuleni,” alisema Musa Mputo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *