Ijue Historia ya Umiliki wa Vitalu – Machimbo ya Tanzanite Mererani

Belinda Habibu

Mererani ni jina la kata ya Wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara, Tanzania, kwa sasa eneo hili limepewa hadhi ya kuwa mji mdogo,na kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002 ina wakazi wapatao 48,027 waishio humo.

Ni sehemu pekee ambako madini ya Tanzanite huchimbwa duniani, na kiistoria yaligunduliwa karne ya 20 (1960s) na wachimbaji wadogo ndio waliopewa hati za mwanzo za kuchimba ambazo zilidumu hadi mwaka 1971, Serikali ilipotaifisha eneo hilo na kulikabidhi shirika la maendeleo la taifa (NDC).

Ilipofika mwaka 1972 NDC ilikabidhi eneo hilo kwa STAMICO ambao waliendelea na utafiti,wakati huo eneo lilikuwa na ukubwa wa nusu kipenyo cha maili kumi(10).

Mnamo mwaka 1985 eneo hili lilipimwa na kupunguzwa hadi kufikia km za mraba 8.5, na kugawanywa katika vitalu vine yaani kitalu A,B,C NA D,ambapo kilikabidhiwa kwa TANZANIA GEMSTONE INDUSTRY(TGI) kulilinda ili lisifanyiwe uchimbaji haramu.

TGI ilitoa mchango kwa wananchi wa maeneo hayo kwa kuchekecha mchanga wenye madini na kuuza kwake.

Mwaka 1989 Serikali iligawa vitalu vyote vinne kwa makampuni yafuatayo,Kitalu A(Kilimanjaro mining),Kitalu B (Building Utilities),Kitalu C (Magezi and Company) na Kitalu D( Mfahamiko).

Mnamo mwaka 1993 Serikali iliwaondoa umiliki wa kitalu D,AREMA Enterprises na kuwamilikisha wanachama wa AREMA mmoja mmoja kwa eneo lake.

Mwaka 1998 Serikali iliwaongezea wachimbaji wadogo eneo kwa kuwapa kitalu B, July 15 1998, Mh.rais wa awamu ya tatu Mh. Benjamini Mkapa aliwapa ahadi wachimbaji wadogo wadogo ya kuwaongezea kitalu A na C ambapo hawajapewa bado.

Habari yote hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Marema ( chama cha wachimbaji wadogo wa tanzanite Mererani kwa kamati ya Mh. Bomani, ukurasa wa 1-2.

1 Comment
  • Je nafasi za kazi kwa wachimbaji wadogo kwann wananyanyaswa kwa kufukuzwa kazi je ni kwamba hawana mkataba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *