Ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imepata ajali wakati ikitaka kuruka katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma na abiria wote 38 waliokuwamo kunusurika.
Ndege hiyo ambayo imekuwa ikifanya safari kati ya Kigoma, Mwanza na Dar es Salaam, imetumbukia katika dimbwi la maji lililotokana na mvua zilizoanza kunyesha mkoani humo.
http://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/247602-abiria-air-tanzania-wanusurika-kifo.html
wizara ya uchukuzi iache ubabaishaji ni muda mwafaka wa kununua ndege za kisasa kama wenzetu wakenya
Pole kwa wote waliokuwemo katika ndege hiyo.
Nawapa pole wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo. Hata hivyo serikali yetu inatakiwa kuuwekea lami uwanja huo sasa, na watafute ndege nyingine za kuhudumia njia hiyo. Kisingizio cha kukosekana fedha hakikubaliki kwani kuna matumizi mengi yasiyo na maana.
pole yao kwa kunusurika ndugu zanguni