“Kweli utu umekwisha na kilichobakia sasa ni unyama. Tazama wanavyosomba vitu kwenye duka langu na kutokomea navyo. Nakimbiamoto, lakini watu hawa wanaojifanya wasamaria badala ya kunisaidia kunusuru mali yangu wao wameamua kuchukua vyote,” anasema Bi. Sitikege, kama alivyojitambulisha kwa jina moja, huku akiwa amechanganyikiwa.
Na lazima achanganyikiwe kwa sababukatika majira haya ya saa 4:30 Ijumaa asubuhi, wafanyabiashara wote katika soko la SIDO Mwanjelwa, jijini Mbeya walikuwa wamechanganyikiwa kufuatia moto uliozuka na kuteketeza sehemu kubwa ya soko hilo, huku wengi wao wakipoteza mali nyingiama kwa kuteketea kwa moto au kwa kuporwa na watu waliojifanya wasamaria wema.
Bi Sitikege, ambaye ni mmoja wawafanyabiashara wa soko hili, akiwa anauza vifaa vya elektroniki kama redio na antenna za luninga kwenye duka lililoandikwa SIMSUNG, aliendelea kulalama bila kuwa tayari kupigwa picha; “Nimepoteza kila kitu, watu wamevamia duka langu,badala ya kuokoa mali wameamua kujisombea vitu vyote duka limebaki jeupe.”
Mama huyo ambaye alionekana kushikwana fadhaa, alishindwa kuuzuia umati wa ‘wasamaria wema’ waliovamia dukani kwake mara baada ya jengo moja ambalo lina mashine za kukamulia mafuta ya alizetikushika moto ambayo iliteketeza sehemu kubwa ya katikati ya soko hilo.
Soko hilo lilijengwa na manispaa kama mbadala kufuatia kuungua kwa soko la Mwanjelwa Desemba 2006 ambalo bado linaendelea kujengwa, na kwa kiasi kikubwa, soko hili la muda limekuwa ndilo kiini cha uchumi wa jiji la Mbeya.
“Tunashindwa kuelewa nini chanzo,ingawa wanasema kulikuwa na hitilafu ya umeme. Lakini swali la kujiuliza nikwamba, hivi kweli hatuna uwezo wa kukabiliana na majanga kama haya ama tunasubiri yatokee ndipo tuanze kuhangaika? Kwa nini tuna kawaida ya kukonyeza gizani?” alihoji Bwana Rashid Sanga, mmoja wa wananchi waliofika kwenye eneo latukio kutoa msaada.
Moto huo ulianza saa 9:30 asubuhi nachanzo chake kinadaiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyoanzia katika mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti na kuanza kusambaa katika fremu za maduka mengine. Mali za mamilioni ya fedha zinadaiwakutekea kwa moto na nyingi kuhamishwa na ‘wasamaria wema’ ambao mara nyingihuombea majanga kama hayo yawapate wenzao ndipo nao wajipatie mali kwa njia yawizi.
Hii ndiyo hali halisi iliyokuwepokwenye tukio hilo;
Habari hii imeandikwa na Daniel Mbega, Mbeya
Kwa miaka ya karibuni, baadhi ya watu wamekuwa na tabia za kushangilia wengine wanapopatwa na matatizo; iwe ni ajali barabarani, majanga kama moto na kadhalika. Furaha yaokubwa ni kwamba, watajinufaisha kwa kuwapora waliopatwa na tatizo kwa kigezo cha kuwasaidia. Wanasahau kwamba hata wao wanaweza kukutwa na matatizo kama hayo na endapo watafanyiwa hivyo ni wazi hawatafurahia. Sijui tatizo ni umaskini au ni unyama tu kiasikwamba hawana utu tena. Sijui tufanyeje ili kuondokana na hali hii.
ni aibu,utu umekwisha.
Tanzania ikitaka kujenga soko jipya nikwanini la zima sokoliunguzwe au liungue kwanzandip walijenge ndio utamadun wetu au ndio mipango ya kurudishana nyuma kimaendeleo? angalia historia ya masoka yote yaliyo karabatiwa au kujengwa upia lazim y kumbwe nazaruba ya moto mfana Songea sokokuu, Arusha Soko la kilombero namengineo hiv kwel wajasiriamali wanao jitafutia kwanjia ya kudunduliza wata fikia malengo kweli?.