Mwanza: Mwanafunzi Kidato cha Sita atumbukia chooni na kufa!

Sitta Tumma

MIEZI michache baada ya wanafunzi wa Shule ya Sengerema Sekondari iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, kufanya maandamano kisha kuharibu baadhi ya mali za shule hiyo, wakidai kujengewa vyoo shuleni hapo, mwanafunzi mmoja Yunis Kajiti anayesoma kidato cha sita amefariki dunia baada ya kutumbukia chooni shuleni hapo.

Tukio hilo limetokea leo alfajiri, baada ya mwanafunzi huyo aliyekuwa anatajarajia kumaliza mtihani wake wa mwisho hii leo, alipotoka kwenye bweni kisha kwenda kwenye choo cha shule hiyo, ambapo inadaiwa akiwa anajisaidia ghafla mbao za choo hicho zilivunjika kisha kutumbukia ndani kwenye vinyesi.
  
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Saanane John aliiambia FikraPevu kwamba: "Alfajiri hiyo kuna mwanafunzi mwenzetu alikuja akaniambia kuna mtu ametumbukia chooni. Baada ya hapo nikajifunga kamba kiunoni na nikatumbukia kwenye shimo hilo na kuanza kumtafuta kwa kugusa gusa na fimbo, ndipo nikakutana naye na nikamshika na kumbemba huku wenzangu wakinivuta kisha kumtoa nje".
 
Mkuu wa shule hiyo aliyetajwa kwa kwa jina moja Kahema na Ofisa Elimu Sekondari wa wilaya ya Sengerema, Venance Mwizarubi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku msemaji wa Mganga mkuu wa hospitali Teule ya wilaya ya Sengerema, aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Muguta naye alikiri kupokea mwili wa mwanafunzi huyo akiwa amefariki dunia.

3 Comments
  • Inaniuma sana kupokea taarifa hizi maana mi ni mmoja kati ya marafiki wa marehemu huyo na jina lake aliitwa Euniace Kagiti nilimamaliza kidato cha sita shuleni hapo mwaka uliopita na nilikuwa nikiishi naya katika chumba kimoja katika bweni la Kibasila.        JAMANI WATANZANIA TAHADHARI BAADA YA HATARI HAITAKIWA SI BURE SASA TUTAISHA HEBU TUFUNGUKENI.

  • kifo ndo kitu knachotisha zaidi hata ya jela maana afalikipo mtu huwa hawezi kurudi kwa hiyo tujaribuni kuchukua tahadhari kabla kifo hakijamkuta mtu mfano huyo dogo Euniace amepoteza maisha yake kwa uzembe wa shule na board yake kushindwa kurekebisha vyoo na matokeo sasa ndo hayo

         Sasa hapa utakuta baada ya hatari ndo jitihada let us not allow naive awareness in our life tutakwisha sasa.

  • Inasikitisha kusoma taarifa ya kumpoteza mmoja wa mwanafuzi ambaye huenda kesho angekuwa waziri wa Elimu.

    Nawapa pole wanafunzi wenzake walioguswa na msiba huu pamoja na jumuiya yote ya watanzania wanaofuatilia mambo ya elimu.

    Mimi nilikuwa kati ya wanafunzi wa kwanza kwanza kusoma katika Shule hii nzuri ya Sengerema kabla haijawa High school.

    Ni katika shule nzuri zilizojengwa kwa utaalamu mzuri na kuwepo na vyoo vya ndani vya kuvuta kwa kipindi chote hadi nilipomaliza masomo mwaka 1979

    Wizara ya elimu iliona ni bora kufanya shule hii kuwa High school labda kwavile ilikuwa mahali pazuri pa kusomea bila kuangalia mahitaji ya muhimu kama ongezeko la watu katika wilaya ya Sengerema na kuathiri mfumo wa maji au kuwepo na maji kidogo na kulazimu kujenga vyoo vya shimo.

    Ujenzi wa vyoo vya shimo siyo jambo geni lakini unahitaji utaalamu mkubwa wa kufunika choo hicho kwa zege kali na nondo kubwa.

    Haiingii akilini shule hiyo kuwa na vyoo vya shimo vya kutumia mbao na vilivyokaguliwa na afisa Elimu wa Wilaya, Mkoa na wizara Elimu pia. Ni uzembe kama uliofanyika kule Dar es salaam na kibali cha ujenzi wa ghorofa 10 kikajenga ghorofa 16 na kuanguka na kuuwa watu 16.

    Mafundi waliojenga choo hiki, mwenye choo ambaye ni Mkuu wa shule, afisa elimu Wilaya, Mkoa na wizara ya elimu ni kati ya watu ambao wanatakiwa wajibu maswali haya na wakishindwa wajiuzulu na kuchukuliwa hatua kali kama wajenzi wa ghorofa hilo wanavyochukuliwa hatua.

    Familia ya mfiwa ni lazima ifidiwe kwa kujua kuwa huyu aliyekufa angekuja kutoa mchango mkubwa serikalini.

    Naomba vyombo vya dola visiishie kuangalia tuu vitoe onyo kali na vyoo vyote vya shimo vifungwe na kama hakuna tena vyoo vya kuvuta maji shule ifungwe na hii iwe fundisho kwa shule nyingine.

    Tunataka Tanzania tuwe na elimu bora na mazingira mazuri ya kusomea  kama tuliyoipata kipindi hicho na siyo acha tu bora elimu kwa mazingira yoyote.

    Tuna mali asili nyingi sasa kama gesi fedha zitokanazo na gesi hii ziweke mazingira mazuri ya mahali pa kusomea ikiwa ni pamoja na vyoo ya kuvuta  kama ni uhaba wa maji kwenye eneo jengeni kisima cha kupampu na matanki juu tumieni maji kwa kuweka vyoo vya kuvuta.

    Waziri wa elimu shart uliangalie hili vinginevyo basi siyo vibaya nawe ukajiuzulu kwa kushindwa kulisimamia

    Mungu ibariki Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *