Kishapu: Wanafunzi Magalata huponea njaa shuleni

Kulwa Magwa

WANAFUNZI wa shule ya msingi Magalata, wilayani Kishapu, wameendelea kuhudhuria vizuri shuleni tangu utaratibu wa kutoa huduma ya chakula ulipoanza.

Utaratibu wa kutoa huduma hiyo ulianza miaka mitatu iliyopo ambapo unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa ushirikiano na Mpango wa Chakula wa Kimataifa (WFP).

uji-shuleni

uji-shuleni2

Wakinywa-uji

Wanafunzi wa Shule ya msingi Magalata, wakifurahia kifungua kinywa cha uji wanaogawiwa shuleni hapo

Kwa mujibu wa Kaimu mwalimu mkuu wa shule hiyo, Cyprian Mabele, tangu utaratibu huo ulipoanza, mahudhurio ya wanafunzi yameongezeka na kuwatia moyo walimu.

Mabele alisema, chakula hicho kimekuwa kikisababisha wanafunzi hao kuhudhuria kwa wingi shuleni, ikizingatiwa kwamba katika miaka ya hivi karibuni, familia nyingi zimekumbwa na upungufu wa chakula.

“Watoto wanakuwa wengi sana maana wanajua wakija watakunywa uji asubuhi na kula makande mchana, tofauti na wakikaa makwao ambapo wakati mwingine hata hicho chakula wanaweza wasikipate,”anasema mwalimu huyo.

Kutokana na utaratibu huo kusaidia mahudhurio ya wanafunzi, wanaiomba serikali iendelee kuwakumbatia wafadhili hao ili waendelee kusaidia mpango huo.

Mwaka jana, shule hiyo ilifaulisha wanafunzi wanane kati ya 32 wa darasa la saba, ambapo mwaka uliotangulia wanafunzi sita ndio waliokwenda sekondari.

Kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi 386 ambapo mwaka huu imeandikisha wanafunzi 49 katika matarajio ya kuandikisha watoto 60, huku ikiwa na walimu 10. Hata hivyo shule hiyo ina upungufu wa vyumba vinne vya madarasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *