Lowassa: “Kuna ugonjwa wa kutokutoa maamuzi”; akwepa kuzungumzia ufisadi

Jamii Africa
Lowassa

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, hatimaye amezungumza bungeni miaka mitatu na miezi karibu mitatu tangu kujiuzulu kwake kufuatia kashfa iliyolitikisa taifa ya Richmond.

Bw. Lowassa ambaye baada ya kashfa ile alijaribu pole pole kurudi katika mijadala ya taifa kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari alikuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake na wakosoaji wake kuzungumza tena Bungeni na hasa swali kubwa ni jambo gani ambalo angeamua kurudi nalo katika hadhara ya mijadala ya kisiasa nchini.

Bw. Lowassa mmoja wa wanasiasa wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na ambaye anaushawishi mkubwani ndani ya Chama cha Mapinduzi aliamua kuvunja ukimya wake Bungeni akitoa mchango wake kufuatia hotuba ya makadirio ya ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda. WM Pinda aliridhi mikoba na cheo chake baada ya anguko la Lowassa.

Pamoja na kutoa sifa mbalimbali za mafanikio ya serikali ya chama chake Bw. Lowassa aliamua kurusha mashambulizi ya wazi ambayo baadhi ya watu wamechukulia kama mashambulizi yasiyo na utata ya viongozi walioko madarakani. Bw. Lowassa alitumia muda kushambulia utendaji serikali akisema kuwa watendaji serikalini wamekuwa wazito kufanya maamuzi magumu kwa kuhofia kulaumiwa. Hata hivyo hakutoa mfano wa maamuzi magumu ambayo yameshindwa kuchukuliwa kwa hofu ya kulaumiwa.

Kabla kuelekeza mashambulizi hayo, Lowassa alieleza kwa majigambo ya mwanasiasa kuwa yeye alikuwa ni kati ya wabunge walioshinda kwa asilimia kubwa ya kura, akishika nafasi ya nne mbele ya wabunge watatu wa CCM. Katika mchango wake kwenye hotuba hiyo ya bajeti ya Waziri Mkuu, alieleza kuibuka ugonjwa wa kuogopa kufanya maamuzi serikalini na kusisitiza kuwa ni bora kuamua kwa makosa kuliko kutoamua kabisa.

Hata hivyo, wakati akieleza kuwa serikali imekuwa ikikabiliwa na ugonjwa wa kushindwa kufanya maamuzi hakuwa tayari kueleza ugonjwa huo umeanza baada ya yeye kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond au hata wakati huo akiwa katika wadhifa huo. Pamoja na kuzungumzia suala hilo la uthubutu wa kufanya maamuzi Bw. Lowassa alizungumzia pia haja ya kufanya mabadiliko katika ofisi ya Waziri Mkuu akitoa wito kuwa ofisi hiyo ina majukumu mengi sana na kutokana na wingi wake imekuwa haifanyi vizuri. Alitoa pendekezo la kuondoa ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

“Ofisi hii ni kubwa sana, kuna Maafa, Uratibu, Bunge, Uwezeshaji, Uwekezaji na Tamisemi. Tamisemi yenyewe pia imegawanyika katika mambo mengi sana. Nashauri Serikali itafakari kuigawa Ofisi ya Waziri Mkuu ili Tamisemi iwe yenye kujitegemea. Kwa kuwa sehemu katika Ofisi ya Waziri Mkuu inashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, haina budi kupunguziwa mzigo” alisema Bw. Lowassa.

Kutokana na kauli hiyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na hasa siasa za ndani ya CCM wanaeleza kuwa ndani ya mchango wa Lowassa bungeni, kwa sehemu kubwa amejielekeza kujibu mapigo ya uamuzi wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kumtaka yeye na wenzake, Rostam Aziz na Andrew Chenge kuachia nyadhifa zao kwenye chama hicho kutokana mwenendo wao unaokipunguzia umaarufu chama hicho mbele ya jamii.

Wachambuzi hao wanahusisha mchango huo wa Lowassa na mwelekeo wa maamuzi ya CCM kwa kugusa baadhi ya hoja zake hasa pale alipobainisha kuwa kwenye Jimbo la Monduli, CCM imepata kura nyingi za urais na yeye kati kura za ubunge amezoa nyingi kiasi kushika nafasi ya nne kitaifa kati ya wabunge wa CCM.

Kwa mujibu wa wachambuzi hao, bado inaaminika kuwa mtazamo wake huo kwamba amekuwa akikibeba CCM kwenye Jimbo lake unatajwa kukinzana na ule wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama ambaye hivi karibuni mbele ya wabunge wa CCM alisisitiza kuwa hakuna mtu maarufu kuliko chama hicho na kwamba chama kitazidi kujijenga kama taasisi wakati wote.

“Tumesikia ujumbe wake ambao tunaamini unalenga kukosoa uamuzi wa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao kama ilivyoamuliwa na NEC, lakini kigezo pekee cha kwamba mwenendo wao umekuwa ukigharimu chama unatazamwa kitaifa na si katika eneo moja dogo, kwa sababu mwenendo wa viongozi wa kitaifa unagusa taswira ya chama kitaifa.

“Kule kwake (Monduli) au Igunga na hata Bariadi inawezekana mbinu fulani kufanikisha ushindi ili baadaye kuunda hoja Fulani mahsusi ya kujijenga zaidi kisiasa, lakini ukweli halisi kutoka kwenye jamii kitaifa, inaibua mtazamo tofauti kabisa na huo. Utakumbuka hata wakati anajiuzulu uwaziri mkuu, nchi nzima ilishangilia lakini kule Monduli waliandaliwa magari na watu maalumu kwa ajili ya kumpokea kishujaa. Ujanja huu ndiyo CCM hauupi nafasi tena, tunataka kuwa realistic na si kubuni mbinu za ujanja ujanja,” alisema mmoja wa viongozi wa sasa wa CCM.

Baadhi ya wananchi waliotoa michango yao mbalimbali katika mitandao ya kijamii wameonekana kuvutiwa na kauli ya Lowassa juu ya ukosefu wa ujasiri wa maamuzi wakipongeza uamuzi wake kusema kile ambacho baadhi ya watu katika jamii wanaamini kuwa ni tatizo. “kanifurahisha sana pale aliposema watu wanaogopa kutoa maamuz, hope message sent” amesema Sam Kabugo kwenye mtandao wa Facebook.

Wananchi wengine hata hivyo wamechukulia uamuzi wa Lowassa kuzungumza kwa kuimwagia sifa CCM akiyapa shavu mafanikio ya miaka 50 ambayo “kila mtu anajua, na dunia inajua” kuwa ni mbinu ya kujaribu kutafuta huruma ndani ya CCM lakini wakati huo huo kuzungumzia kwake suala la uamuzi kuwa ni kujiandaa kwa maamuzi yanayokuja hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.

Hata hivyo tetesi ambazo FikraPevu haijaweza kuzithibitisha zimedai kuwa masaa machache kabla ya hotuba yake kulikuwa na kampeni ya chini kwa chini ya kupata support (washangiliaji) kutoka kwa baadhi ya wabunge hasa kutoka viti maalum na wale wa Zanzibar. Hata hivyo haijajulikana hasahasa matokeo ya kurudi kwake katika mijadala ya siasa kuna maana gani kwani hakugusia moja kwa moja tatizo kubwa zaidi ambalo linakabili taifa, yaani ufisadi.

Waandishi Wetu, Dodoma

7 Comments
  • huo ndo ujio mpya wa EL. Anataka serikal ichukue uamuz mgumu wa kuwafukuza mapacha watatu il waifumue serkal vzuri. Anajua kuwa JK ni muoga na ndo maana kasema hvyo.. Pia ameonesha kutojal utaifa kwan ye yuko radh taifa lpate hasara il kukwepa lawama… Nadhan JK AMEPATA SHOCK ALVYOCKIA KAUL YA EL..

  • Inabidi Lowassa nae afanye maamuzi magumu, sio swala la kuwashutum serikali pekee. Yeye mwenyewe mwana ccm harafu anadai kuwa kunaugonjwa wa kutokutoa maamuzi, Asiwe chichidodo. kama vipi atoke kwenye hiyo system ndo tutamuamini

  • jana nilimsikiliza vizuri sana jaajabu nikasikia akimkandia jk,kwakushindwa kuwajibika vizuri kwakutoa maamuzi yaharaka katika serekali yaje,,kweli huyu mtu anajisafishia njia ya kuwa Rais 2015.

  • Dkt.Toure asema lowassa kamfanyia hujuma kura za maoni kwani,pia kushinda kwake kwa kura 37,000 dhidi ya zake 300 ni uwongo kwani idadi ya watu hao 37,000 ni sawasawa na wapiga kura wote hadi wazee monduli ndiyo 37,000,ukiangalia wapo wapiga kura kati ya hao wameenda mikoa mingine kama arusha na Dar-es-saalam n.k kutafuta maisha na haiwezekani kwa watu wote kupiga kura.Swali ni lini wamasai wote hao walirudikwa wakati kupiga kura?Ukweli Lowassa anadhibitisha kuwa hata “makosa yake hayaja fanyiwa maamuzi mazito”.
    NI huyu huyu Lowassa aliye shinikiza NSSF kutoa billion 10 ajili ya kufufua kiwanda cha GENERAL TYRE EAst Afrika L.T.D.Arusha kwa Barua ya tarehe 15/7/2007 namba Na Pm/1/567/40 zaidi ya Billion4 zikapotea na hazikufanyia kazi iliyo kusudiwa anasema Shellukindo.
    Sasa Lowassa anachofanya nikuonesha serikali ya kikwete imewekwa mfukoni mwa wabadhilifu na wahujumu uchumi wachache lakini uongozi unaogopa.Na nikweli kabisa hata ukiangalia majibu ya Mkurugenzi Dkt.Hosea wa TAKUKURU dhidi ya yule jasusi wa marekani kuwa “Bwana mkubwa amesema tuwaheshimu viongozi waliopita asinge penda kuona kesi zao zinapelekwa mahakamani’WIKILEAKS ndiyo iliyo dhiirisha uwoga wa MAAMUZI magumu katika serikali ya CCM ni kweli “kunauogonjwa wa kutoa maamuzi”Sasa hapo tusitegemee maendeleo yenye usawa wala kushuka kwa garama za maisha na gepu la maskini dhidi ya matajiri kushuka kama maamuzi muhimu kwa ukombozi hayatakuwa yakifanyika.

  • Lowassa being an MP had all the democratic right to speak within the confines of the law.He is known as a person who does not chew his words and always calls a spade a spade!We hope our leaders will borrow a leaf from what he said in Parliament in order to speed up development of our people.

  • Lowassa as a Brand was Battered by Efforts to End Darkness Urgently? Return this Brand Sooner than Later.

    It’s alarming to observe how politics can mess up the country and reduce it to nothingness. Its difficult to establish how long Tanzanians will continue be forced to engage in small talk, unproductive political bickering while politicians abuse the country, ruin the economy, jeopardise the future of the nation and simply render the otherwise high potential nation, hopeless.

    My theory has always been that all politicians are corrupt to certain extents and equally I subscribe to the notion that pities the game not the player, for as far as I know, very few politicians can stand up and claim virtuousness as far as their discharge of service is concerned. In the Holy Bible there is a verse which warns us of a tendency to always see the “stick” in our brother’s eyes but never a “log” in our own. This verse seems extensively relevant to politicians especially in Africa who continue to distract Tanzanians by drawing attention to their fight for interests.
    It’s hard to understand why our media gets so engrossed into politics at the expense of key national agenda. But well since that seems to be the only item attracting readership I beg to start, only today by delving into the subject just a bit.

    One politician who seems to baffle me, and may be many more people, is Edward Lowassa, the Monduli MP and former PM, who I consider a battered brand. If a famous brand is battered more often than not, repercussions are harsh and restoration of confidence and “public” allegiance to the brand tends to be expensive, and often ends in disappointment. In the business world we all know the cost incurred by likes of Dell Computers when they recalled millions of flawed laptop batteries, and the case of Toyota recalling hundred of thousands of faulty vehicles. A key question here is whether the faults were purely “technical” or some were extra technical. Any how those are efforts to reclaim the confidence in the brand. It’s pricey. I am trying to draw an analogy of reversing a tainted leadership image resulting from both technical and extra technical loopholes. Like the business world the political world is competitive and the game can get harsh allowing room for extra technical strategies to survive. However business is sober and driven by logic and basic premises of life because it touches an individual’s “today” more directly. Politics is slightly different – it’s less “human” and is more for “tomorrow”. If a highly needed brand of cars is tainted once it will easily return back – if it ever disappears. Looks like Edward Lowassa has “really” not gone away as a brand and continues to prove like a much needed brand for “today”.

    The honourable MP was forced to resign from Premiership by his political adversaries because of what the MP rightly describes as ability to “make a decision than not”. Yet after the PM was asked to resign the decisions remain “unmade” five years down the line. We can not continue to let politicians fight for interests ruin our businesses, our lives, our future. We are now in total darkness in Tanzania, yet we don’t see who can even make a bad decision. Its time we realise that Lowassa is a true victim of extra technical loopholes in the game and revert to hating the game and not the players all the time. If we continue to be distracted from the “ball” we will soon become a hermit state and a real laughing stock in the region – we already are.

    James Kizito – Kariakoo, Dar es Salaam Tanzania:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *