Lugha kikwazo cha kufikisha elimu ya uzazi wa mpango Butiama

Stella Mwaikusa

Muuguzi mkunga wa Hospitali ya wilaya ya Butiama Neema Mchuruza,  anasema pamoja na mambo mengine ya mila na desturi zilizopo katika wilaya hiyo, lugha ya Kiswahili  ni tatizo lingine linalokwamisha kampeni za uzazi wa mpango.

Anasema wamekuwa na utaratibu wa kwenda vijiji ambavyo havina zahanati, kwa ajili ya  kutoa chanjo kwa watoto pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango, lakini wamegundua kwamba akinamama wengi hawaelewi lugha ya Kiswahili na kujikuta wakiondoka bila kujua kilichozungumzwa.

Anasema kutokana na hali hiyo, akinamama wengi wamejikuta wakiendelea kuzaa watoto wengi kutokana na kukosa  elimu kamili kuhusu njia za uzazi wa mpango, kwani wengine hupata maelezo kutoka kwa wenzao ambayo si sahihi na kuifanya kazi ya kuhamasisha matumizi ya njia za uzazi wa mpango kuwa ngumu.

NESI

Neema Mchuruza wa kwanza kushoto akiwa na wahudumu wa hospitali ya Butiama

Gati matuki mkazi wa kijiji cha Siloli Simba, anakubaliana na muuguzi kwamba, hata yeye hawaelewi wahudumu wanapofika katika kijiji anachoishi, kwa kile alichodai wanaongea Kiswahili cha ndani na kigumu hivyo amejikuta hafahamu mambo mengi likiwemo la uzazi wa mpango, kwani mpaka sasa ana watoto saba lakini hajui kabisa namna ya kujikinga na ujauzito.

Neema anasema wanatafuta namna ya kuwatumia wahudumua wanaoelewa lugha ya mahali Fulani kwenda huko kuelimisha juu ya elimu ya uzazi wa mpango, au kuwa na mtu anayetafsiri ili kuhakikisha elimu ya uzazi wa mpango inafikishwa kwani, bado wilaya ya Butiama iko nyuma  ukilinganisha na wilaya zingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *