Majambazi yashambulia ndege ya dhahabu Geita, mmoja auwawa

Jamii Africa

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha nzito za kivita, wamevamia Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), na kuiteka ndege ndogo iliyokuwa imebeba dhahabu kutoka mgodini hapo, kwa ajili ya kuikisafirisha kwenda nje ya nchi.

Tukio hilo limetokea hii leo majira ya saa 5:55 asubuhi, katika uwanja wa ndege wa mgodi huo uliopo umbali wa kilomita 5 kutoka katikati ya mji wa Geita, na kwamba majambazi hayo yaliyodaiwa kujifunika nyuso zao, yaliishambulia ndege hiyo kwa risasi za moto, kwa lengo la kutaka kupora dhahabu hizo zenye mabilioni ya fedha.

Habari kutoka eneo la tukio zilizoifikia FikraPevu, zinaeleza kwamba, wakati majambazi hayo yakiimiminia ndege hiyo risasi, huku yakifyatua ovyo risasi nyingine hewani, askari polisi Wilaya ya Geita walifanikiwa kufika eneo hilo haraka, kisha kuanza kupambana na watu hao kwa risasi za moto, kabla majambazi hayo hayajakimbia na kuliua jambazi moja.

Katika majibizano hayo ya risasi, askari polisi walifanikiwa kuliua jambazi moja baada ya kulimiminia risasi kifuani, na kwamba kabla ya jambazi hilo kuuawa na polisi lilikuwa limejeruhiwa vibaya na mmoja wa walinzi wa mgodi huo ambaye ni raia wa nchini Afrika Kusinia.

Dhahabu iliyonusurika kuporwa na majambazi hao inadaiwa kuwa ilikuwa ni zaidi ya kilo 1,000, ambapo ilikuwa imegawanywa katika maboksi 16 huku kila boksi moja likiwa na matofali manne ya dhahabu, na kwamba kila tofari moja linadaiwa lilikuwa na ujazo wa kilo 25.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio na kuthibitishwa na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la polisi wilayani humo, zimeeleza kwamba, uchunguzi wa awali umeonesha kuwa majambazi hayo yapatao wanne walivamia mgodi huo kwa kuingilia geti kuu la kuingilia kwenye uwanja huo wa ndege wa mgodi wa GGM kabla ya kuiteka ndege hiyo.

Pichani: Wakazi wa Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, wakiangalia mwili wa mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi (jina hajafahamika), akiwa ni mmoja wa watu wanne waliyovamia mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), akiwa amekufa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika jaribio hilo la kutka kupora dhahabu jana.

 

“Ilikuwa kama sinema vile, maana majamaa (majambazi), yalikuwa yanarusha risasi nyingi kwa kuishambulia ndege hiyo iliyokuwa ikipakia dhahabu. Baadaye polisi walipofika walipambana nayo kwa risasi za ana kwa ana na jambazi moja tumeliua”, alisema afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la polisi wilaya ya Geita kwa njia ya simu.

Imeelezwa kuwa majambazi hayo yakiwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, bunduki aina ya SMG, pamoja na Bastola, walianza kuishambulia ndege hiyo yenye nambazi za usajili SH-TZX iliyokuwa ikipakia dhahabu kutoka kwenye gari maalum iliyokuwa imebeba dhahabu hiyo kwa kuirushia risasi nyingi mfululizo.

“Inadaiwa kwamba, baadhi ya walinzi wa mgodi huo waliokuwa katika eneo la tukio wakihakikisha usalama wa mali iliyokuwa ikisafirishwa, wengi wao walilazimika kutimua mbio baada ya majambazi hayo kuanza kutoa mashambulizi ya risasi, na kwamba katika walinzi hao alibaki mzungu mmoja raia wa Afrika Kusini ambaye ni mfanyakazi wa mgodi huo aliyekuwa na bastola ambaye alianza kupambana na majambazi hayo kwa kuyarushia risasi.

Inadaiwa kuwa wakati mzungu huyo akijibizana kwa risasi na majambazi hayo, mmoja wa majambazi hayo alijikuta akiishiwa risasi na kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi kwenye mkono wa kulia na kulazimika kukimbia kuokoa maisha yake, na baada ya muda mfupi askari polisi walifika na kuanza kupambana na majambazi hayo.

Hata hivyo imebainishwa kuwa baada ya askari kufika majambazi watatu yaliamua kukimbilia kwenye msitu mkubwa unaozunguka mgodi huo, ambapo jambazi moja lililokuwa limejeruhiwa na Mzungu huyo kushindwa kuhimili vishindo vya askari polisi kabla ya kuuawa.

“Wakati polisi wanafika eneo la tukio, majambazi matatu yalitimua mbio msituni. Lakini mmoja aliyekuwa amejeruhiwa alibaki akirushiana risasi na polisi, na baadaye alitwangwa risasi akafa papo hapo. Hili ni tukio la kwanza katika mgodi huu”, alisema ofisa mwingine wa jeshi la polisi kwa sharti la kutotajwa jina kwa vile siyo msemaji.

Jambazi aliyeuawa bado hajatambuliwa jina, na alikutwa na basotola moja aina ya Chenese yenye namba za usajili 0048467, ikiwa na risasi sita, bunduki moja aina ya SMG yenye namba za usajili za Uganda UA.89381997, Mabomu manne ya kutupa kwa mkono, Magazini 4 pamoja na risasi 60 ambazo hazijatumika, huku akiwa amevalia nguo za kawaida seti nne ndani na ile ya tano (juu), ikiwa ni sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ).

Hata hivyo imeelezwa kwamba, mfanyakazi mmoja wa mgodi huo ambaye ni raia wa Afrika ya Kusini aliyetambuliwa kwa jina la Engenas Van Der Schuffs, alijeruhiwa kwa risasi na majambazi hayo, baada ya kumpiga risasi kwenye mkono wake wa kulia na kumjeruhi vibaya.

Marubani wa Ndege iliyoshambuliwa yenye nambazi za usajili SH-TZX wametambuliwa kwa majina ya Meja Kondo Hamza pamoja na Hamdan Salehe, na kwa taarifa zilizopatikana kutoka Geita zinaeleza kwamba ndege hiyo imeshindwa kuondoka kwenye uwanja huo kutokana na moja ya mabawa yake kutobolewa kwa risasi na majambazi hayo.

Hilo ni tukio la kwanza mkoani Mwanza kwa majambazi kuteka mgodi na kuishambulia ndege kwa risasi, ikiachiliwa matukio mengine ya uhalifu ambayo yameonekana kuanza kurudi kwa kasi mkoani hapa.

Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – Mwanza

37 Comments
  • Inatisha kishenzi!!! lakini nadhani washikaji walifuata hiyo mikate 16 ambavyo ni zaidi ya kilo 25 , mimi sijui tutafika wapi?

  • jamaa inaonekana ni mwanajeshi kamili hapo ndo unaweza kutofautisha kati ya walinzi wetu na wa njee ndo maana makampuni ya nje yanapenda kuja na walinzi wao

  • Hao wabongo waliotimua hawafai kusindikiza mali za mabilioni ya fedha. waendelee kulinda mafuta tu.

  • Duh,

    Kwa kweli inatisha, nauliza na huo msitu walikokimbilia majambazi hakuna police aliwafuata? I see, GGM inaitaji ulinzi kuimarishwa zaidi lazima kuna internal hand in this, lazima kuna mtu anawapa majambazi ratiba za kazi mgodini.

  • IVI CC TULIO GEITA TUNAONA, IVI MGODI UNAWANUFAISHAJE WANANCHI WA GEITA? VUMBI HAMNA BARABARA,AFYA OVYO SHULE NDO WANANCHI BINAFSI WANAFUNFUA,NJOONI MUONE JAMANI UKU KWENE UTAJIRI KULIVYO OVYOOO.

    AO MAJAMBAZI INAWEZEKANA WANAHASIRA NA MGODI,

    IMAGINE WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WOOOOTE WAMEPIGWA MARUFUKU, WATAKULA WAPIII,MI NADHANI HAO SIO MAJAMBAZI NI WANANCHI WENYE HASIRA KALI.. ANGALIENI MAISHA BORA TULIOAHIDIWA JAMANI…

  • Hiyo yote ni dalili za mgao usiokuwa wa haki wa rasilimali zetu, na hali haitakuwa nzuri kama hoja za wananchi walio wengi hazitaheshimiwa katika mgao wa keki ya Taifa. TUTAFAKARI !!

  • Si kitu kizuri kutokea lakini ukweli watu wamechoka kuona dhahabu inapandishwa ndege na kupelekwa nje ya nchi huku wananchi wakiachiwa mashimo. Wajuba sasa wanaamua kufanya kweli kama noma na iwe noma.

    Wajuba wangeshinda game wangeuaga kabisa umasikini, kilo 1000 ya dhahabu pesa yake si mchezo. DIE RICH OR DIE TRYING TO BE RICH.

  • nadhani hawa walitaka kupata riziki kwa nguvu ila basi tu tunaibiwa mali hizo zote tungekuwa tunachukua wenyewe.duh tungetajirika sana

  • mamilioni ya tsh inasemekana zaidi ya bilion 163,jamaa wangechukua wangeuaga umaskini na wangetoa ajira kwa wenzao maana wangejenga mahoteli na majumba ya ajira big up msichoke try it again one day must yes.askari
    watakufa maskini

  • umefika muda wa kufanya hvo.maana si halali mali zote ziende nje huku wananchi wanahangaika na shida kibao

  • mpaka majambazi wavamie ndiyo tujuwe kuwa kilo 1000 (boksi 16, kila moja lina tofali 4 za kilo 25 ni kilo 1600 wala si 1000!) zilikuwa zinasafiri siku hiyo!?, nani anatuwakilisha watanzania katika kusimamia na kuhakiki kiasi cha dhahabu inayopanda ndege kila siku hapo msituni?, kwanini iondokee huko msituni?..sisi wadanganyika tunafaidika vipi na hayo madini?…nani anayejua bei halisi huko inakoelekea hiyo dhahabu?… yaani mgeni anaingia jikoni anapika, na anapakuwa na kula huko huko jikoni, wenye nyumba tuko sebuleni tunasubiri ugali!…basi na mabenki yawekewe viwanja vya ndege ili pesa ipae kiusalama

  • kwanini wageni wanajipakulia tuu vyetu?, tupeni sababu ya kuwawekea uwanja huko huko migodini!.. kama migodi inawekewa viwanja ili dhahabu ipae huko huko kwa “sababu za kiusalama”… basi mabenki nayo yawe na viwanja vyao vya ndege…

  • Amakweli heri ya huyo aliye kufa akitaka mali isitoke tz wazawa hatuji kinachoendelea migodini wazungu wanakuja kuchimba wenyewe nakuondoka nazo sisi tunabaki kuwapungia mikono wakiwa namadini yetu kwenye ndege haoo.. kuijenga America kweli serikali ipo? nadhani hawani watu wenye uchungu na mali zetu.tz wananchi tunabaki kuona mashimo tu thamani ya madini wajua wazungu sisi tutachimba lini?.

  • Mi nashindwa kuelewa jamani, hii nchi inaenda wapi jamani…babu zetu wametuachia mali, tunawaachia wageni hivihivi!!! nakionea huruma kizazi kijacho…IKO WAPI SERIKALI YETU….UMEENDA WAPI UZALENDO WA ENZI ZA MWALIMU??? Nani alaumiwe hapa, MSOMI AU MWANANCHI WA KAWAIDA? Mi naona ni sisi wasomi tunaotia sign kuangamiza wanyonge!!

  • Mi nashindwa kuelewa jamani, hii nchi inaenda wapi jamani…babu zetu wametuachia mali, tunawaachia wageni hivihivi!!! nakionea huruma kizazi kijacho…IKO WAPI SERIKALI YETU….UMEENDA WAPI UZALENDO WA ENZI ZA MWALIMU??? Nani alaumiwe hapa, MSOMI AU MWANANCHI WA KAWAIDA? Mi naona ni sisi wasomi tunaotia sign kuangamiza wanyonge!!

  • Safi sana, mali yote hiyo ilikuwa inasafirishwa nje, sisi mlikuwa mnatuachaje?? safi sana kaka jambazi….RIP.

  • mtizamo wangu unaweza pingana na wengi sana, let us think cleary jamani, sitaki kutetea criminals but tunadhulumiwa sana tena sana ndo maana ni pekee yule mzungu

  • pole sn familia ya jambazi, mi nawaunga mkono kabisa 2mechokaa yan ss wakaz wa geita hatuthaminiwi barabar mbovu, maji hakuna hewa chafu matatizo 2

  • Chenge na karamagi waliosaini hii mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini yetu bado wanaendelea kutesa mjengoni kwa raha zao. Dr. SLAA akisema mnasema anavuruga amani na ana tamaa ya kwenda kuishi mgogoni. kulaaaleki natamani yaho madini yangehamia mkoani kilimanjaro tuone kama kuna mwisi angesogelea pale kuhomora .

  • Huyo jamaa muliemuua ni Msukuma,huwezi amini! anaitwa selemani daudi gata. mmemuua?
    alikuwa atali sana. ndie aliteka ndege mwaka 2002, ndie alieiba zaabu kule mara buhemba. ni mtu wa kazi kweli. police huyo si Mnyarwanda kama mlivyozani. ana makazi apaapa mjini Mwanza. angefnikiwa angebakiza noti yote umu nchini. angetumia pesa umu uchumi ungepanda.

  • Tanzania ni nchi kama sikosei ya tano duniani kwa kuzalisha dhahabu nimesema kama sikosei hata kama nikikosea nakumbuka amana hii marehemu Julius Kambarage Nyerere hakupenda kuigusa kwa sababu aliona nchi bado haijakomaa kuchimba madini hayo.

    Lakini baada ya kuondoka hali haikuendelea kama alivyotaka tuliona migodi mikubwa ikianzishwa kanda ya ziwa ukiwemo huu wa Barrac Gold Mines na machimbo mengine kama ya Gesi huko Songosongo na Mtwara

    Kama wataalamu wetu wangefanya mikataba mizuri na ya kueleka kwa watanzania nafikiri kusingekuwa na malalamiko yanayoonekana wazi hivi leo kuwa nchi yetu inahujumiwa bila kuwepo na usimamaizi thabiti wa madini hayo na gesi hiyo

    Nasema hivyo kwa kuunga mkono msemaji aliyepita anayeuliza je ni muuafaka kujenga kiwanja cha ndege eneo la mgodi. Jibu linaweza likawa ndiyo ikiwa kama hapo mgodini kuna maafisa wa mapato wanaohakikisha kila chembe ya dhahabu inayotoka hapo

    Aidha ni vvizuri mbali na TRA kuwepo na ofisi mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ni wajibu kwani kama mamlaka ya mapato watahakikisha na mkaguzi mkuu akaidhinisha basi ndege inaweza kuruka na madini hayo

    Lakini tumeona taarifa ya kukanganya kuwa box moja lina uzito wa kilo kadhaa na baada ya kupiga hesabu tunaona tofauti ya kilo 600 zaidi kati ya 1000 zilizooripotiwa

    Je kama gharama ya madini hayo kwa kilo 1000 ni bilion 163 nyongeza yake ambayo haikurekodiwa ni zaidi ya nusu ya bei hiyo ni zaidi billion 86

    Sasa kama hii ni trip moja je zinafanyika trip ngapi kwa wiki, mwezi mwaka na ni mabilion mangapi yanayochukuliwa bila kurekodiwa

    Mimi kwa ushauri wangu mheshimiwa Rais Kikwete alimpa mkaguzi mkuu majengo yake mwenyewe ili asiingiliwe kwenye kazi yake nafikiri sasa mheshimiwa Raisi mpatie meno ili aweze kufanya kazi ya kukagua migodi yote kwa kufanya suprise check kwenye makasha yaliyotayari kusafrishwa nje ya nchi.

    Nafikiri uliona kazi nzuri aliyofanya ndugu Ludovick Utoh kwenye taarifa ya ukaguzi iliyowalazimisha mawaziri na manaibu waziri kadhaa pamoja na wakurugenzi kuachia madaraka

    Aidha nashauri serikali kwa kushirikisha wanakijiji waliotoa eneo lao kujenga migodi hiyo wawe wanalipa royalt kwani madini hayo yanapatikana kwenye maeneo yao ,halmauri za wilaya na mkoa zidai fedha hizo ikulingana na thamani ya madini yanayochimbwa ili kujenga miji yao.

    Nazungumzia madini siyo dhahabu tu, hata chuma,bati, uranium, shaba ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mafuta na Gesi iliyopatikana huko Songosongo na Msimbati Mtwara nk

    Kwa kufanya hivyo kila mwananchi atakuwa ananufaika na pato la taifa na hakutakuwa na manununguniko wala mauaji yanayotokea kwani watu wanaona kama hawa wawekezaji wanajichukulia utajiri wa watanzania.

    Kama leo hii mwalimu Julius Nyerere angeamka huko aliko na kukuta haya angesema je

    “si niliwaambia”

    Mungu ibariki Tanzania

  • RIP brother life gumu na hukuwa na jinsi wakati mababilon wanakula dhahabu zetu na hii iwe ni fundisho for both 2 side of the Gvrnmnt and his peoples. so better on the other side street sweeper

  • Kama hali ndo hiyo,hayo ndo matunda ya mali za umma kama madini kushindwa kutokomeza umaskini mpaka sasa jobless inakosesha watu/vijana uvumilivu.lakini,hayo magwanda sijui wanapataje?

  • watu washavurugika nyie mnaenda kuuza nje mabilion alafu sisi tunasota tuuuuuuuuuu,msitutanie nyie!!!!!!!!!

  • aisereeee hi mbaya sana watu wanakufa kila siku ya mungu god may help us poa washikaji wangu mimi niko rwanda

     

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *