Tatizo la sasa katika sekta ya afya, haliwezi kupatiwa ufumbuzi wa kuduma hata kama watawekwa pale Wizarani, the best Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kutoka nchi za jumuiya ya madola. Hii ni kwa sababu we always fail to make the right diagnosis, na badala yake kuachia suala hili lijiendesha katika mazingira ya ‘siasa huru’.
Nia yangu ni kutoa maoni yangu kuhusu kiini cha tatizo hili, lakini kubwa zaidi, tusaidiane jinsi gani ya kulikabili sasa na kwa siku za usoni.
Katika Tanzania, Sekta ya afya inajenga na a 3 Tier System:
1. Basic Clinics, Dispensaries = First Level
2. District Hospitals = Second Level
3. Referral Hospitals and Specialty = Third Level. (e.g. of Referral Hospitals = Muhimbili, KCMC, Bugando, Mbeya) and Speciality (e.g. Specialities = Taasisi ya Moyo, Kansa etc).
Moja ya matatizo yaliyopo under this arrangement
Pamoja na kwamba 75% ya mahitaji ya wananchi ya afya (health needs) yapo katika first level (i.e. basic clinics and dispensaries), huku asilimia 25% tu ya health needs zikiwa katika higherlevel i.e. referral hospitals and specialty, katika kupanga bajeti za wizara ya afya na ustawi wa jamii kila mwaka, serikali huwa haitengi fedha kwa kufuatana na mahitaji haya. Badala yake, asilimia 75% of Resources (madawa, vifaa, mishahara, posho, education and training etc) huwa zinapelekewa kwenye level ya juu (referral hospitals na Specialties). Jambo hili ni la kushangza kidogo kwa sababu kuu ifuatayo:
Katika kila siku ya mwenyezi mungu, outpatient diseases in Tanzania (magonjwa yasiyohitaji mgonjwa kulazwa zaidi ya kuonana tu na daktari kisha kurudi nyumbani), ni yafuatayo:
Malaria; Acute Respiratory Infection ; Numonia ; Kuhara; Eye infection; Skin Infection; Anaemia; na UTI = 2%. Magonjwa ya kulala hayapo mengi kama yake ya kutohitaji kulala na haya ni pamoja na complicated malaria (ambayo huwa sio nyingi sana). Complicated malaria accounts for about 70% ya magonjwa yote yanayohitaji mgonjwa kulala. Mengine katika the remaining 30% ni TB, Ukimwi, na kuhara.
Hoja ya msingi hapa ni kwamba asilimia 90% ya magonjwa yote Tanzania yanaweza kupatiwa tiba katika vituo vya afya (dispensaries and clinics), iwapo vitapatiwa tu wataalam wa kawaida, vifaa basic tu vya diagnosis, na madawa. Lakini kutokana na serikali kutojali eneo hili in terms of budget and resources allocation, matokeo yake ni wataalam wengi kurundikana kwenye higher levels of the 3 tier health system, na kupelekea uwepo wa hali ya – too much manpower chasing too few resources.
Kwanini Serikali inaendekeza jambo hili?
Sijui, lakini ningekuwa Waziri wa Afya ningeweza kutetea kwa hoja zifuatazo:
· Kuna umuhimu wa serikali to train train wataalaum ili waende kupata watu wa kutosha kwenda kutoa huduma at the lower levels i.e. district hospitals, and clinics and dispensaries, ndio maana kila mwaka tunatenga fedha nyingi sana kwa ajili ya zoezi hili.
· Pili, Tanzania hakuna Health Insurance Market yenye kuweza kuwasaidia walio wengi, kwani walio wengi cannot insure themselves against the risk of serious illnesses, injury and the consequent need for very expensive treatment. Kwahiyo kuna umuhimu wa serikali kutenga fedha nyingi kwenye level ya juu (Referral hospitals and specialty hospitals – moyo, saratani, n.k), kuliko level za chini, kutokana na kutokuwepo kwa health insurance market kwa maskini.
Lakini majibu haya yanazaa maswali mengine. Kwa mfano:
1. Suala la kwanza – pamoja na resources nyingi kwenda to higher level, kwanini magonjwa yote makubwa uhitaji serikai kupeleka wagonjwa India na kwingineko. Fedha zinazotengwa kila mwaka hazitoshi kuzuia hili?
2. Suala la pili ni juu ya mahitaji ya fedha nyingi kwa serikali to train wataalaum wanaohitajika mikoani/wilayani/vijijini. Pamoja na fedha za walipa kodi kutengwa kwa wingi sana kila mwaka kwa ajili ya zoezi hili, kwanini Tanzania bado inabakia kuwa moja ya nchi yenye the highest ratio ya population per doctor. Requirement ya World Health Organization (WHO) ni kwamba, kila daktari anatakiwa ahudumie watu wasiozidi 10,000 (elf kumi). Lakini sasahivi, hali ipo vipi Tanzania?
Kwa hali ya Sasa, kwa wastani (national in Tanzania) ni karibia watu 64,000 per doctor. Na kuna mikoa ambayo hali ni mbaya sana, kwa mfano:
· Mkoa wa Mara = 167, 000 people per doctor.
· Kigoma kwa Mheshimiwa Zitto na Kafulila, 308, 000 people Per Doctor.
· Mwanza = 144, 000 per doctor
· Rukwa kwa Mh. Pinda = 121, 000 people Per doctor
· Tabora kwa Mh. Sitta = 121, 000 people per doctor.
Inakuwaje hakuna uwiano wa wingi wa fedha zinazotengwa kila mwaka kwa ajili ya zoezi hili, hazina uwiano na takwimu hizi za afya kitaifa? Ni mikoa michache sana yenye ahueni katika hili, nayo ni:
· Arusha = 22,000 people per doctor
· Pwani = 32, 000 people per doctor
· Morogoro = 56,000 people per doctor
· Dar-es-salaam = 24,000 people per doctor
· Ruvuma = 57,000 people per doctor.
3. Suala la tatu: Katika Tanzania ya leo, karibia 50% (nusu) ya hospitali zote ni za NGOs, huku nusu iliyobakia ni mchanganyiko wa serikali na sekta binafsi. Na hali hii imekuwa hivi miaka nenda miaka rudi. Kwanini hali hii haibadiliki kulingana na fedha nyingi za walipa kodi kutengwa kwa ajili ya bajeti ya wizara ya afya miaka nenda miaka rudi?
4. Suala la nne: Katika Tanzania ya leo, karibia 25% ya clinics na dispensaries ni za NGOs, huku zilizobakia zikiwa ni za serikali. Nyingi ya hizi zipo vijijini. Lakini kama tulivyokwisha ona, ni asilimia 25% tu ya bajeti ya serikali ndio uelekezwa kwenye mahitaji ya vijijini ambako asilimia 70% ya watanzania ndio wanaishi. Ndio maana, kwa ujumla, Clinics na Dispensaries zote Tanzania zilizo chini ya serikali hazina wataalam wa kutosha, vifaa, wala madawa. Matokeo yake ni kwamba, asilimia 70% ya Watanzania wanategemea huduma za afya zinazotolewa na NGOs, Waganga wa Kienyeji, huku wengine wengi wakiamua kupotezea tu magonjwa mengi na kumwachia mungu awaongoze.
5. Na suala la mwisho: Madaktari wengi wanaosomeshwa na fedha za walipa kodi hutumia muda mwingi sana kutoa huduma za afya katika hospitali binafsi, kuliko kule walipoajiriwa na serikali. Je, ni nini kinawasukuma kufanya hivi? Ni mishahara midogo au kuna sababu nyingine?
Makala haya yameandikwa na Mchambuzi (JF Member)
so why do we have doctors who have completed schools and not at work? holy cow!
ni muda wa viongozi kuchukua hatua. takwimu alizotoa mchambuzi wanazo na uwezo wa kuzifanyia kazi wanao. suala ni kwamba tunapata viowasiojua mipango.
MADAKITARI mesomeshwa na hela za wananchi; hebu kuweni wazalendo kutoa huduma kwao
nawashangaa madaktari, wanajali maslahi yao tuu, wamesahau kama bila team yote ya afya watafanya kazi peke yao,
Nadhani hakuna mtu anayestahili kushabikia mgomo huu kwani unagusa maisha ya watu ila Serikali yapaswa kuwa na utamaduni wa kuchukua hatua za makusudi mapema katika kutatua matatizo ya madaktari pale tu wanapotoa madai yao na si kusubili tarehe ya mgomo ifike ndio watoe tamko
Nadhani madaktari wamejiona kuwa ni miungu wadogo wanataka sisi wavuja jasho tunaoishi kwa shida tuwaabudu. Serikali ichukue hatua kazi maulimboka wote wawajibike. ulimboka amepelekwa muhimbili anatibiwa na nani hali yeye amesisitiza mgomo hii inaonesha mgomo huu hauna ubinadamu. heri madaktari wa mkoloni walikuwa na huruma kuliko hawa watoto wazawa. wafungiwe kila kitu hata kutoka nje. miaka 3 watakaoajiriwa wapewe masharti hawataki wakae tujue sasa hatuna madaktari wazalendo ila wataka maslahi bila huruma na utii.
kweli ni uzuni sana! kuona watu wanapata tabu huku kodi zao zinatumika! serikali inabid ijue umuhim katika sekta zote pia ichukue tahadhari mapema kabla ya maafa tuache siasa kwenye mambo muhim ili tujenge nchi bora ni maoni ya kadinali painter
madaktali mishahara inatosha.wabunge ipungue ,vifaa vya hospitalini pamoja na ufisadi na mipango mibaya nchi bado kipato ni kidogo asiyeelewa ni mbishi tu kukiri ukweli safi muhimu vinunuliwe madaktali warudishwe kazini nchi inakwenda uchochezi wa kisiasa ndo noma tz.
Mchambuz ameonesha hali halisi ya sekta ya afya nchini Tanzania Madaktari wanajiona wafalme au LULU katikati ya changarawe lakini hawakumbuki hao wavuja jasho na wamama wajawazito wanaoteseka ndio waliotoa KODI mpaka wao wakafika hapo.Nyie wakina ULIMBOKA hivi DOCTOR aliemsaidia MAMA yako wakati unazaliwa angegoma ungezaliwa ww hai au ungekua haujulikani angalieni utu na maandiko ya mungu yanawaasa nini na sio kutaka maslahi ya makumbwa ili mkale Bata LEADERS
Kweli kangara ulilosema nipo pamoja nawe!
nawashauri wavumilie mpango wa budget ya mwaka 2014/2015 kwani subira ndo jambo la msingi kwani Elimu walionayo wamepewa na ALLAH MWENYEZI MUNGU MUOGOPENI MUNGU