Nassari aanza kuibana serikali; Wenje, Kafulila, Kigwangala nao wamo

Jamii Africa

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige amejikuta katika wakati mgumu, baada ya Wabunge kadhaa akiwamo mbunge mpya wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kumbana kuhusiana na Serikali ikiwemo Wizara yake kushindwa kuzalisha ajira nyingi kwa vijana, badala yake Serikali hiyo imebaki kuwa ombaomba mkubwa duniani.

Wabunge wa vyama vyote ikiwamo Chama cha Mapinduzi (CCM), Chadema na wa NCCR-Mageuzi walikuwa mwiba kwa Waziri Maige, wote wakiilaumu serikali kwa kushindwa kuzalisha ajira zakutosha kwa wananchi wake.

Mbali na kibano hicho cha Wabunge, Waziri Maige alishindwa kueleza sababu za Serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Elimu na sasa Waziri wa Kilimo, Jumanne Maghembe kuhusiana na kupiga marufuku masomo ya kilimo kwa Shule za Sekondari nchini.
Hali hiyo ilimkumba Waziri Maige wakati wa mdahalo wa kuhusu ajira kwa vijana nchini, ulioandaliwa na wanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho.

Mbunge wa kwanza kuirushia kombora Serikali na Waziri Maige ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mdahalo huo, alikuwa ni mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje (Chadema), ambaye alihoji sababu ya Rais Jakaya Kikwete kuwaahidi Watanzania kwamba atazalisha ajira milioni moja mara atakapoingia Ikulu kama kiongozi mkuu wa nchi, ahadi ambayo alidai imeota ‘mbawa’.

Mbunge Wenje ambaye alikuwa miongoni mwa watoa mada wakuu, alianza kwa kusema kwamba, takribani vijana 800,000 wanaoingia katika soko la ajira hapa nchini kwa kila mwaka, kati yao vijana wasiozidi 100,000 ndiyo wanaopata ajira rasmi, huku vijana wengine 700,000 wanabaki hawana ajira kabisa.

Pichani ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), akizungumza kwenye kongamano la ajira lililoandaliwa na wasomi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma. (Picha na Sitta Tumma).

Alisema, hali hiyo inatokana na Serikali kuwa na sera mbovu pamoja na mikakati yake kutozingatiwa, hivyo jambo hilo linazidi kupanua pengoi kubwa la vijana kutokuwa na ajira, jambo linalozalisha mtazamo hasi ndani na nje ya Tanzania.

“Taarifa za kiutafiti zinaonesha kwamba, kati ya vijana 800,000 wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka, kati ya hao vijana 700,000 wanakosa fursa za ajira hapa Tanzania.

“Hili ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu hii. Waziri Maige upo hapa naomba unisikilize vizuri…ahadi kama zilizotolewa na boss wako Rais Kikwete hazijasaidia chochote!. Tunahitaji ujasiri mkubwa katika kuondoa tatizo hili”, alisema Wenje ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Hata hivyo, Wenje ambaye karibu muda wote alikuwa akishangiliwa na wasomi wa chuo hicho cha Mipango Dodoma, alikwenda mbali zaidi na kusema kwamba, sera za ubinafsishaji viwanda na mashirika ya umma zilizoasisiwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa zinaipeleka nchi shimoni, kwani viwanda vingi vimekufa, hivyo Watanzania wengi kukosa ajira.

Alisema, bila kuwepo kwa njia mbadala Tanzania itaendelea kuonekana inarudi nyuma katika maendeleo yake, badala ya kupiga hatua kubwa kusonga mbele kimaendeleo, na kwamba inakera sana kuona raia wa kutoka nje ya nchi wakija kufanya kazi hapa nchini na kulipwa fedha nyingi kuliko fursa hizo kupewa Watanzania.

Naye Mbunge wa Nzega Mkoani Tabora, Dk. Hamis Kigwangala (CCM), aliiponda Serikali kwa kile alichosema kwamba imeonekana kuwa bingwa wa kuandaa na kubuni mikakati isiyotekelezeka na kuleta tija kwa wananchi.

“Tanzania ni mabingwa wa kuandika na kuandaa mikakati ambayo utekelezwaji wake ni sawa na ziro. Kati ya vijana 760,000 wanaoingia kwenye soko la ajira, ni vijana 40,000 tu wanaopata ajira, wengine hawa wanakosa ajira”, alisema Dk. Kigwangala kisha kushangiliwa na umati mkubwa wa wasomi uliokuwa umejaa kwenye ukumbi wa chuo hicho.

Aidha aliipongeza Serikali kwa kuwa na mfumo mzuri wa elimu unaowaandaa vijana wengi kuingia katika soko la ajira, na kwamba kwa sasa taifa linapaswa kuondokana na sera ya kuzalisha wasomi wa digrii wasio na uwezo wa kufanya kazi, huku akitolea nchi ya China ambayo inawasomi lakini wenye uwezo wa kusimamia na kufanyakazi bora na yenye kiwango cha Kimataifa.

Alipendekeza Watanzania hasa wenye akili timamu wawekeze kwenye sekta ya kilimo, ili kuweza kujiajiri wenyewe na hatimaye kujikwamua na lindi la umasikini wa vipato linalosababishwa na mawazo ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.

Kwa upande wake, mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageui), alisema: “Ripoti ya Mkukuta inasema vijana 650,000 hadi 750,000 wanaingia kwenye soko la ajira, lakini wanaopata ajira ni wachache ikilinganishwa na hitaji lenyewe!”.

Kwa mujibu wa mbunge Kafulila Tanzania ni nchi ya 20 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa kasi, lakini Tanzania pia ni nchi ya 20 duniani kuwa nchi masikini, na ni nchi ya tatu kuwa ombaomba duniani ukiachilia mbali nchi ya Iraki ambayo uchumi wake umeathiriwa sana na vita.

Alisema: “Tanzania inazo ekari milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, lakini toka uhuru hadi sasa zinazolimwa ni ekari 400,000 tu. Najiuliza hivi Serikali inafanya kazi gani?. Je tukiingia kwenye soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki Watanzania tutaishije?”.

Naye mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), mbunge wa Iringa mjini, mchungaji Peter Msigwa (Chadema), waliishambulia Serikali kwa kubeza jitihada zake ambazo walidai hazijawasaidia Watanzania, huku mbunge Nassari akieleza kushangazwa na uwezo wa kiutendaji wa Waziri Maghembe ambaye huko nyuma akiwa waziri wa Elimu alipiga marufuku masomo ya kilimo shuleni.

Akijibu hoja za wabunge hao, Waziri wa Maliasili na Utalii, Maige alikiri Serikali kukabiliwa na changamoto kubwa, hasa katika suala zima la ajira, na kusema Serikali ya CCM ni sikivu hivyo itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zote zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na kupanua soko la ajira.

“Kimsingi zipo changamoto nyingi zinazoikabili Serikali. Lakini naamini mikakati inayobuniwa katika kutatua adha zilizopo zitafanikiwa. Na nzuri zaidi Serikali yetu hii ni sikivu, itaendelea kutatua matatizo yaliyopo”, alisema Waziri Maige huku wasomi waliokuwa wamejaa kwenye ukumbi huo wakisikika wakiguna kuashiria kutilia mashaka kilichosema na Waziri huyo.

Habari hii imeandaliwa na Sitta Tumma – FikraPevu, Dodoma.Wabunge wa vyama vyote ikiwamo Chama cha Mapinduzi (CCM), Chadema na wa NCCR-Mageuzi walikuwa mwiba kwa Waziri Maige, wote wakiilaumu serikali kwa kushindwa kuzalisha ajira zakutosha kwa wananchi wake.

Habari hii imeandaliwa na Sitta Tumma – FikraPevu, Dodoma.

2 Comments
  • watanzania sasa wamejua kinacho endelea kuwa ni ubazilifu mkubwa wa lasimali zao na si kuwaletea maendeleo wala ajila ni kazi kwao kuamua kwani haingii akili kuwa na ajila hewa unalipa mishahara watumishi hewa na kuna vijana wasomi hawana ajila wanatangatanga mitaani bila aajila huduma za afya zimezolota dawa hamna msd wanalipwa kwa kuwa na dawa zilizopita wakati wake watanzania saa ya ukombozi ndiyo sasa wanafunzi vyuo vikuu hawana mikopo helal zinalika reli,barabara hamna gharama ya maisha imepanda maisha ni magumu sana watanzania wamekata tamaa wanasubiri miujiza

  • kama tanzania ndio ivoi kweli kuna haja kubwa ya wa2wote 2weke itikadi ze2 mbali na kuwa ki2 kimoja kuokoa maisha ya mtanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *