Nchi za Afrika zashauriwa kuboresha miundombinu kuvutia wawekezaji sekta ya madini

Jamii Africa
Mineworkers work deep underground at Harmony Gold Mine's Cooke shaft near Johannesburg, September 22, 2005.

Licha ya bara la Afrika kumiliki hazina kubwa ya madini, inachangia asilimia 8 tu madini yote yanayotengenezwa duniani.

Inakadiriwa kuwa asilimia 30 ya madini yote yanayochimbwa duniani yanatoka Afrika ambayo kwa sehemu kubwa ni dhahabu, almasi, shaba na tanzanite.

Kulingana na Jalida la NewsDay la nchini Zimbabwe limesema kikwazo cha uzalishaji wa madini ni kukosekana kwa teknolojia na mtaji wa kuendesha shughuli hizo barani Afrika. 

Madini yanayochimbwa husafirisha yakiwa katika hali ya malighafi kwenda nchi za nje zenye teknolojia ya kisasa ambapo hurudishwa tena Afrika yakiwa yamechakatwa kwa ajili ya kutafuta soko.

Licha ya teknolojia duni, bado wawekezaji wameendelea kuingia maeneo mbalimbali ya Afrika kutafuta soko na kuchimba madini. Hali hiyo inachagizwa na Sera za kimataifa ambazo zinahimiza uwekezaji wa mitaji katika nchi za Afrika ambazo zinakabiliwa na umaskini.

Uwekezaji huo unawazuia wawekezaji wa ndani kutumia rasilimali zao za asili na matokeo yake kukosekana kwa ushindani katika sekta hiyo ambayo inawafaidisha wawekezaji kutoka mataifa makubwa duniani.

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2030 inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 50 zitawekezwa katika miradi ya uchimbaji madini na kuzalisha faida itakahowanufaisha wawekezaji ikiwa hatua hazitachukuliwa kudhibiti soko.

Afrika imechangia kukuwa kwa makampuni makubwa ya madini duniani yakiwemo Anglo American, BHP-Billiton, Anglo Gold Ashanti na Acacia ambayo yamewekeza mitaji katika nchi za Afrika ikiwemo Afrika Kusini, Tanzania, Zimbabwe, Nabimia, Botswana.

Ni muhimu kufahamu kuwa ziko baadhi ya nchi kama Botswana yenye sera na sheria nzuri za madini inafaidika na madini iliuonauo ambapo kwa sasa inaongoza duniani kwa mauzo na uzalishaji wa  almasi.
Ongezeko la thamani na faida

Madini yanayochimbwa Afrika husafirishwa katika mfumo wa malighafi. Ili kunufaika na rasilimali hiyo muhimu, Afrika imetakiwa kutatua vikwazo vinavyozuia sekta hiyo kukuwa na kustawi.

Mabadiliko ya kisera na sheria ambayo yatasaidia kupata faida ya uchimbaji na kodi ya ongezeko la thamani. Lakini jambo hili linahitaji teknolojia ya kisasa na ujuzi kutoka kwenye soko lenye nguvu ili kuboresha bidhaa zitokanazo na madini.

Maboresho ya bidhaa za madini zinazosafirishwa  nje ya Afrika kutasaidia kuzalisha mapato ya ziada ambayo yatatumika katika sekta nyingine za uchumi. Pia kutengeneza ajira kwa vijana na kuboresha huduma za kijamii.
Hatua iliyochukua Tanzania

Serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Magufuli imefanikiwa kutunga sheria ya kusimamia Rasilimali Asilia ya mwaka 2017 ambayo Tanzania inakuwa mmiliki wa rasilimali zote ikiwemo madini.

Hatua hiyo inakuja baada ya kubainika ukiukwaji mkubwa wa sheria katika sekta ya madini ambao unaikosesha serikali mapato. 

Tanzania ambayo ni mzalishaji mkubwa wa Tanzanite na dhahabu imekuwa ikipata mrabaha wa asilimia 3 katika madini yanayochimbwa nchini.

Pia rais Magufuli alizuia usafirishaji wa mchanga wa dhahabu kwenda nje ya nchi na kuagiza Wizara ya madini kujenga mtambo utakaokuwa unahusika kuchenjua madini ya dhahabu ili kuongeza mapato serikalini.

Agizo hill linafuatia kukamatwa kwa makontena ya mchanga wa dhahabu katika bandari ya Dar es Salaam yakipelekwa nje bila kulipiwa kodi.

Pia omeendelea na majadiliano na kampuni ya Barrick Gold mining ambayo ina miliki migodi ya dhahabu namna nzuri ya kufaidika na madini haliyopo nchini.

Hata hivyo, nchi za Afrika zimeshauriwa kuboresha miundombinu ya reli, barabara, bandari na usafiri wa nga ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi kugundua na kuchimba madini yatakayolinufaisha bara hilo linalokabiliwa na umaskini. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *