Pinda ‘aelemewa’ mgogoro wa nani achinje nyama

Sitta Tumma

SAKATA la nani achinje nyama kati ya Waislamu na Wakristo bado linaonekana kuwa bichi, ambapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja nyama yaendelee, hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.

Kufuatia hali hiyo, Pinda ameagiza kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kwamba kazi hiyo ifanyike haraka iwezekanavyo, na kisha ripoti yake iwasilishwe Serikalini kwa hatua zaidi za kimaamuzi.

Waziri Pinda ameyasema hayo muda mfupi uliopita leo, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, kuhusiana na kikao chake cha pamoja na viongozi wa Kikristo na Kiislamu, kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la Mwanza, kwa lengo la kutatua mgogoro wa kidini unaoonekana kuota mizizi.

Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda, imekuja siku chache baada ya kutokea mapigano makali baina ya wafuasi wa dini ya Kiislamu na Wakiristo kuzuka huko Buseresere-Katoro katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, ambapo mchingaji mmoja aliuawa kwa kuchinjwa huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya.

Aidha, Pinda alikemea vikali vurugu za kidini zilizotokea mkoani Geita, na kuwataka viongozi wa madhehebu yote ya dini kuheshimiana, kujenga mshikamano na kutohasimiana, kwani wao ni watu muhimu sana katika maendeleo na utulivu wa nchi.

12 Comments
  • kwa hiyo tutaishi kwa mazoea mpaka lini?hatakwenye mambo ya hatari hayo waziri mkuu ameona bora watu wazoee kuuana hata katiba ameiweka pembeni anasema mazoea ili watu waendelee kuuana simuelewi pinda ana ajenda gani na wakristu wa nchi hii

  • Hawa viongozi wa nchi hii tumewachoka yaani hali mpaka inafikia hivi wao wanafanya siasa badala ya matendo, tume au kamat inaundwa ya nini wakati wahusika wako waazi na kweli tumechoka wakitaka huko wanakochinja awepo shehe na mchungaji ili nyama ipate baraka za wote.  haya na huko Zanziba je pia wanaunda tume,

  • sasa hawa mwisho hata kuku au mbuzi nyumbani mwetu watatulipisha hela watuchinjie ukichinja wanakuua

  • Kama kunaushahidi wowote kupitia Bibilia unao turuhusu kuchinja basi uwekwe wazi mimi binafsi sijauona kwani tumeambiwa tu kiingiacho si najisi bali kitokacho

    • cha msingi ni kuainisha kwenye katiba mpya uhuru wa kuabugu ikiainisha vipengele vipi katika kuabudu. vinginevyo tutaleta vurugu. wakipewa mamlaka ya kuchinja wataweza kuchinja kila nyumba?

  • Ni jambo la kushangaza sana, kwani kuna tatizo gani mtu akichinja ng'ombe wake na watu wakaja kununua kitoweo? nani aliyekuamrisha wewe uchinje mimi ndio nile, jamani hii Amani mnaiona kwetu hamjui thamani yake, hakutakua na kwenda hata huko msikitini mnakokwenda, wala makanisani vurugu zikienea. na ni vile wakristo wana misingi imara ya imani yao, vinginevyo nchii hii ingeshakumbwa na vurugu, uvumilivu una mwisho wake, kabla hatujafika huko tunaomba waislam muelewe kuwa nchi hii haina dini bali watu wake, mnapodhani mnayo haki ya kufanya mtakalo itatupeleka pabaya, labda kama mmechoshwa na hii amani, watu wameoleana kila ukoo una mkristo na muislam, sasa sijui hata mnataka nini?

    Mbona wakristo hawajawahi kupiga au kudhuru mtu katika mihadhara ya kikashifu ukristo, miaka zaidi ya 10 tangu walipoanza, hakuna mkristo anayehangaika kubishana wala kufanya chochote, kwanini hamtumii huo muda na nguvu hiyo kukipekua zaidi kitabu kitakatifu cha kurani na hadithi za mtume? kwa miaka yote hiyo ni waamini wangapi wangeshajua hadithi hizo na mafundisho yake mema?

    Jamani tunawaomba mbadilike, ukristo tanzania hii hauwezi kwisha kwa aina yoyote ya vitisho, ukatili wala mauaji, wakrito walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo, mnapoteza muda tu. kuna mambo mengi ya msingi kwa nguvu hiyo mnayotumia ingesaidia sana, kama kuanzisha shule, madrasa, shunguli za ufundi, useremala, uvuvi na ukulima bora kuliko kuhangaika na jambo ambalo wao wenyewe wanaelewa hawawezi kumaliza. hakuna kitu kigumu kumbadilisha mtu imani yake.

    Wakristo wanawapenda na ndio maana wamekua wakiwavumilia kila mara, msitumie mwanya huo kudhani hawawezi kurudisha uovu, ingawa wamefundishwa hivyo, kwamba wanawaombea tu hata muue, lakini serikali za vijiji, mikoa na taifa inategemea nchii hii itakuja kuishi watu wa dini moja, la hasha ni ndoto tu haitakaa itokee kabisa. haya ndio maoni yangu

  • Chui akinyeshewa utadhani ni paka lakini utakapomrushia jiwe japo mara moja mbili tatu, na akagundua we ni mbaya wake, ama zako mama zake. Sasa waislamu wasidhani wakristo hawawezi kunoa visu na mapanga ni kwamba wanajaribu kuvumilia mengi kutokana na imani yao imara, maana imani ya kikristo hairuhusu kuua la hasha.

    Sasa siku watakapopata mwongozo wa huyo wanayemwamini ya kuwa ni vyema kulipiza kisasi, hapatatosha nchi hii. Hao viongozi goigoi  wasioweza kutoa maamuzi magumu kama Pinda waache waendelee kupiga rhumba.

    Mbona pakinuka waislamu wengi watarudi ukristo. Waislamu waache ushamba, wasome wafanye maendeleo. Kawaida ni kama sheria lakini si sheria, kama wakristo walikubali kuchinjiwa nyama na waislamu miaka ya nyuma, sasa hawataki, kwa sababu hao waislamu wakiruhusiwa kuchukua hilo jukumu la kuchiknja wataweza kuchinja kila nyuma za waislamu wenyewe na wakristo? Kwa sababu kuchinja si machinjioni tu hata majumbani tunachinja. kuna maeneo ya vijiji ambayo mtu anajichinjia ng'ombe wake na kuuza nyama kwa wanakijiji wenzake, sasa ni mpaka ng'ombe wake achinjiwe na muislamu? Nani kasema? Thubutu yenu nyie waislamu.

  • Amani ya Mwenyezimungu iwe juu yenu kwa wanaohusika,Kwani tatizo liko wapi? Waislamu wanaimani zao na Wakiristo wana imani zao,kila mmoja na dini yake,kila mmoja afuate maamrisho ya dini yake,kama watu wana maelekezo ya namna ya kuchinja katika dini yao basi wayatumie,kwani kuna ubaya, laa kama hakuna maelekezo basi watu watizame wenzao wanafanya vipi ,sio vibaya kuiiga.

  • Kwa kweli kama Waziri Mkuu ana muda wa kuingilia mjadala kama huu wa kitoto…. basi ndio maana hata maswala zenye Kipaumbele zaidi yana achwa pembeni.

    Kwa mfano wa vitu ambavyo Mh. Pinda Angejiingiza kwa nguvu zaidi ni utekelezaji wa sera za ajiria kwa vijana, afya, na elimu…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *