Pres. Kikwete’s “Maisha bora kwa kila Mtanzania”

Salome Gregory

Reflecting on President Kikwete's promise – maisha bora kwa kila Mtanzania or a better life for every Tanzanian, see the photos and your comments are welcomed!

Hali ngumu vijijini
Five years already and it doesn't appear to have brought any difference to the lives of these two boys, whom I spotted following proceedings to mark the Day of the African Child at Chanzulu village

Hali ngumu vijijini, bibi kizee Loi

Hali ngumu vijijini, Tanzania
The two photos above show an old woman called Loi, in front of and in her house in Ibwaga Village. She has lost her sight with age, and lives with her daughter who is deaf. They normally depend on farming for their livelihood but last year their farm was among many others that were destroyed by the December floods in Kongwa District. At the time photograph was taken they had stock of only ten kilos of ”uwere” left.

Hali ngumu vijijini, Tanzania

Hali ngumu vijijini, Tanzania
Above, Ekilia Ngonyani, 46 is a single mother raising five children alone. She is also suffering from an unestablished condition that has caused her stomach to swell up and has been for the past 16 years. She cannot afford to go to a 'big hospital' as advised by the doctor in her village. For a living she walks 14 kilometres thrice a week to buy vegetables in a village called Tubugwe and only gets Sh2000 in profit for her trouble.
Hali ngumu vijijini, Tanzania
Theresa with her four grandchildren, having lunch of boiled 'uwere,' the family can only afford to eat two meals a day.
Maisha ya vijijini Tanzania 2010
A young boy Village walks more than 20 kilometres in one week to collect firewood.
114 Comments
  • …OMG!!!! Hizi picha zimenisikitisha kwa kweli, hadi unborn child wangu nimesikia kameruka tumboni.Hizi picha 7 hapo juu ni mfano tu, kuna watu wengi wanaishi kimaskini sana hapa TZ.Hizi hapa ni baadhi tu zinaonyesha jinsi hii nchi ilivyo kwenye dimbwi la umasikini………uhuru miaka 40 lakini bado sanaaaaaa tena sana tu maana pesa zote za mapato ya nchi, pesa za misaada zinazotolewa kuwasaidia watu kama hao kwenye picha zote zinaishia mikononi kwa mafisadi.Eeeeeeeeee Mungu baba saidia Tanzania.

  • Hawa wote hapa juu ni vigumu sana kwao kuparticipate katika kubadilisha mfumo mzima tulionao katika nchi hii. Lakini tunaosoma hapa na kuona picha hizi tuna nafasi kubwa ya kuchangia mabadiliko na kuwafanya watu wa aina hii wafaidi angalau sehemu fulani ya matunda ya uhuru. Kushiriki katika uchaguzi ili kuondoa uozo uliopo ni sehemu ya mchango wako. Shiriki

  • Hii ni Bora ni bora maisha tu. Kubwa, pongezi kwa mwenye wazo la kutafuta na kuziweka hapa hizi picha. Keep ze faya burning.

    Development is indeed a nightmare. PRS, PSRP came and passed, then MKUKUTA (NSGRP) which was later on christened MKUKUTA I, has just been here, and left these fellows and many more hapa hapa (pale pale walipo ndipo walipokuwa – oh God watakapokuwa – wakijaaliwa kuwepo); the song is still on, MKUKUTA II, and this time LOUDER. Mkuu wa kaya has just put it very clearly – ‘ANAJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA MIAKA MITANO INAYOISHA.ee Mungu samehe sisi.

  • Maisha bora kwa kila mtanzania” ni kauli mbiu tu aliitunga consultant wakati wa kuandaa ilani ya chama.si dhamira halisikama ambavyo inatakiwa kuwa ndo maana hakuna utekelezaji na wala haoni tofauti, laiti kama presidaa angefungua mtandao na kuziona picha hizi !labda dhamira ingemsuta

  • kwa tunaotoka vijijini, haya ndio maisha ya kawaiada ya kila siku, inasikitisha pale wanafunzi wanapopata elimu na kukataa kurudi katika maeneo waliyotoka, wote wanabanana dsm,insikitisha sana hasa yule mama mwenye…..

  • Pole Pretty kwa kumsumbua mtoto amehisi ugumu wa Nchi hii hata kabla ya kuzaliwa. Hali halisi huku ni mbaya sana kuielezea ni ngumu sana, tena sana

  • Asante Manyanda kwa maoni yako, ni kweli ingekuwa vema kama Muheshimiwa angeona hali halisi kupitia picha hizi.

  • Tobaaaaaa! Ee Mungu turehemu Tanzania! Mara nyingi tunajigamba Tz ni nchi ya amani. Mnasoma comment hii nisikieni…”Hakuna amani kwa watu waovu”. Mateso wanayopata watu kama hawa kilio chao kinafika hadi mbingu zinashuhudia…Je waweza kuonesha tofauti kati ya maisha ya kabla ya uhuru na haya wanaoishi watu hawa? Mnaotafuta udiwani, ubunge, na uraisi mwaka huu naomba niwaulize..mtawafanyia nini wapiga kura hawa? Au ni mwendelezo wa Chukua Chako Mapema? Na hata ukichukua utakipeleka wapi? Nimeumia moyoni hasa juu ya wamama hawa ambo wote ni wagonjwa! Ee Mola turehemu!

  • “Better life for every Tanzanian” Really? I think it is supposed to be “better life for few Tanzanian”. It is so hard to look at those pictures,seeing people suffering while others “few” have good time. Traveling everywhere without any good reason through GOVERNMENT funds. And still people will give the same people another chance to “milk” us again.
    He has done nothing in this country; now I know why “the late father of nation” didn’t want him to run for presidency. Because he knew he was not a leadership material. God Bless Tanzania.

  • Manyanda, nakuunga mkono, wasomi na walioona mbele hawarudi vijijini kwao kutia changamoto ya maendeleo. Na wala tusitegemee sana Serikali, maendeleo ya kweli yanaletwa na watu wenyewe!

  • ”Maendeleo yataletwa na watu” I remember this saying by Mwalimu from my young age. I also remember the saying ”Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne; watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora”. In all cases, Watu comes first.

    Yes, the president must fulfill the promises that he made during campaign ya uchaguzi, lakini ‘we’ and I mean all Tanzanians, are all responsible for the continuous suffering and only ‘we’ can make a better life for ourselves and others.

  • Kwa kweli inasikitisha mno,hebu ona leo matumizi ya viongozi wetu wakisafiri nje according to waziri wao wa mambo ya nje,matokeo ya safari zote hizo ni 1 ya kumi,kweli nchi haiwezi hii,ameshindwa kabisa sijui anangangania nini?

  • wamoja ni wamoj na wambili ni wambili. hizo kauli mbiu ni siasa tu ya kutafutia kura za wananchi lakini kuhusu maendeleo ni kitendawili.

  • Kila wakati mimi kuona Roman Abramovich katika TV, kwa ujumla kuangalia Chelsea yeye daima ni amevaa nini inaonekana kuwa nafuu plastiki kuangalia macho. Siwezi kuamini kwamba kuangalia ni nafuu, lakini mimi kwa kweli kuona kuona huo katika duka la jumla na online $ 40 tu sijui ya bidhaa lakini siwezi kuona kuwa macho katika place.Just wengine katika hilo. Online shop.I hawezi kuwa yeye kununuliwa tu katika shop.lol a online

  • KWAKELI SALOME UME INESHA DUNIA JINSI GANI TUNAVYO ACHANA NDANI YA NCHI MOJA TENA YA WATU WALIO HURU NA SAWA KAMA TULIVYO LISHWA NAMWALIMU .LAHAULA!HATA NASI AKINA KALIMANZILA KAMA ULAYA KIKWETE KWELI PICHA HIZO ANA ZIONA? SIAMINI KAMA ANA ONA SASA HIYO NDO NINI.

  • Tanzania is not one country, there are many Tanzanias. Powerful stuff Salome Gregory!

  • Sawa ni masikitiko kwa binadamu kuishi maisha kama haya tuliyoona, ni sawa kwamba hizo picha ni sehemu tu ya watanzania wenye matatizo na pengine haya tuyaonayo ni matatizo madogo zaidi ya yale makubwa ambayo hatujaoneshwa, ni ukweli usiopingika kwamba serikali inawajibika kuhakikisha raia wake ambao ipo kwa ajili yao wanahudumiwa katika nyanja tofauti.

    Hoja yangu hapa ni kwamba, pamoja na kwamba kuna nchi matajiri sana duniani lakini ndani ya nchi zao bado kuna watu wenye maisha magumu kuliko hata haya tuliyoyaona (huu si msamaha kwa serikali yetu kutowajali wananchi wake), na maanisha kwamba pamoja na serikali kuwa na jukumu la kuhakikisha watu wake wanaishi maisha mazuri haiwezi kufanya hivyo kwa kila raia wake hata kama serikali hiyo ina uwezo kiasi gani.

    Serikali si chombo unachoweza kukishika au kukitumia kifanye kitu/kazi, hata mimi na wewe ni serikali, kwa hiyo badala ya kuendelea kulalamikia serikali kama vile ni chombo kilichowekwa sehemu fulani nadhani sasa watanzania pamoja na kwamba utandawazi umetufanya wabinafsi, kwa yeyote awaye na uwezo kidogo wa aina yoyote amsaidie mwenzake asiyekuwa na uwezo. Huhitaji kuwa milionea ili usaidie, saidia tu kwa uwezo wako kwani wahenga walisema kutoa ni moyo na wala si utajiri. Tukilalamikia serikali ndugu zetu wanazidi kupata shida. Popote tuonapo binadamu mwenzetu anashida na tuna uwezo kidogo tumsaidie na dude hili (serikali) litaongezea tulipoanza.

    Tanzania itajengwa na wenye mioyo thabiti.

  • masikini tukiomba msaada wa kusoma tunanyimwa mikopo wanapewa watoto wa wakubwa wanaenda kufanya utumbo vyuoni then wazazi wao wanawapeleka nchi za mbali nako uko wanafanya utumbo lakini mngewasomesha masikini wangesoma kwa shida na kufaulu vizuri kikwete anajinufaisha na familia yake si kwa watanzania nasema kwamba Mungu atakuja kuwaazibu mafisadi wote wanaojali maslahi yao si ya watanzania wote sipendi iki kitu kabisa kutunyanyasa sisi ni watu kama wengine ao mafisadi wangefilisiwa mali zote wasomeshwe masikini ujumbe huu kikwete na watu wake wapate isiishie hapa sipendi Mungu atawaazibu wao wanakula na kumwaga chakula watu wengine wanalala na njaa awajui watakula nini na watalala wapi kama nguo umechoka pelekeni kwa yatima pia ombaomba wegine wana miguu 2 na mikono 2 lakini wanaomba mitaani wachapwe viboko wafanya kazi kwa jasho wapate hela pia wadada wa siku hizi mavazi yao ya kuonyesha maziwa nguo fupi za ajabu wangekuwa wanazomewa au kupigwa wangeacha wanakuwa vituko barabarani sipendi uarabuni nguo za ajabu unapigwa mawe nataka tanzania iwe hivyo kwani ukivaa suruali au sketi chini ya magoti upendezi UKIMWI autaisha mavazi yabadilike jamani mnatutia aibu wadada na heshima zetu tunavaa vizuri na wanaume wa mana tunapata kuliko kujizalilisha wanaume ao wadada wakivaa kiajabu muwazomee ili waache shepu mbaya bado unavaa kiajabu

  • babu yetu nyerere angekuwepo ufisadi usingekuwepo inaniuma sana kwa sisi ambao tumefiwa na mzazi mmoja kabaki mmoja mikopo atupewi kazi mnatunyima vyeti vizuri tunavyo acheni undugu kwenye upande wa ajila serikalini hata sector binafsi kikwete na jopo lake wapate hii sms rushwa za ngono narushwa za pesa na kazi upati sio fresh kula pesa ya halali sio ya wizi wakikamatwa amna kuachiwa wafilisiwe

  • Jamani hivimbune wa hapo ni nani?? hebu mwenyekiti wa mtaa peleka hilo jina au mpeleke jamani??wabunge wetu wanapesa kibao za kununulia kura za maoni na kuhonga majeneza hususan wakati wa uchaguzi inakuwaje kilio cha huyu mama jitumbo kisisikilizwe na mtu wa karibu namna hiyo labbda kaishiwa kdogo basi amsindikize aende kwa mzee JK nadhani hawezi kukosa hata lau 100000 ya daktari

  • siku ccm ikitoka madarakani ndipo maisha bora yatakuja hata hivyo tusilaumu tulijitakia kumpigikura

  • salome kwakeli we acha tu dunia ya tanzania inakwisha kwa sasa na hatujui mstakabli wa maisha yetu yanaenda wapi. na inchi hii imekaliwa na wachache wenye fedha kwa sisi maskini tutazidi kuisha na kuangamia siku hadi siku.

  • There are similar situations in many ares all over tz especially villages….maisha bora is to himself, his family , his friends like rostam, lowasa, hosea and his relatives and all other blind ccm followers who are just there to blow vuvuzela by any how…..now he is traping us with kilino kwanza…….too much lying…ahadi just for getting our kuras

  • kwanini katika kampeni wapinzani wasitumie vielelezo kama hivi kwenye kampeni ili kuonyesha kama kweli serikali yao imrshindwa kusaidia raia wake …

  • Ni ngumu kuelezea,inatia uchungu sana kuwa kuna watu hapa tanzania wanaishi kama wapo peponi na wengine wapo motoni hata kabla hawajafa na hii yote ni kwa kuwa wanaotutawala wametunyima elimu ili tusitambue haki zetu na kupigania. wanachotaka wao sisi tuombe haki zetu. NINAAMINI KUOMBA HAKI YAKO NI LAANA. Haki inapiganiwa.Mungu yupo na siku inakuja haya yote yatawekwa hadharani kama ushahidi wa kupigania haki zetu.

  • Hao hao wanakijiji ndio wachagua rangi ya njano na kijani ili kudumisha Amani na utulivu, nashindwa kusikitika, amani gani wanayo katika hali kama hiyo, utulivu uliopo unawasaidiaje watu kama kawa ambo hatya mlo mmoja ni kitendawili tega, tega ni kutege? hivi tumekubwa na jinamizi gani ambalo hata halituruhusu kufikiria hata kidogo? tunahitaji nabii gani wakutueleza kua chama tawala sio jibu la watanzania wa leo? Mungu atuponye na pepo hili la ujinga

  • jamani haya mambo yanatia uchungu ,huruma na hasira kali..hawa ni ndugu zetu na ambao ukiwaona hapo wamekwama kabisaa kimaisha…lakini wapo watu wanaibia nchi hii manillioni na wako mitaani wanakula nchi bila tatizo..AMKENI SASA..ITS TIME FOR CHANGE

  • Naamini wakati wa mabadiliko ni sasa. Nguvu tunayo mikononi mwetu. Tutazame hali halisi kisha tuamue. Asante wasomaji kwa maoni yenu.

  • Kipimo kizuri cha kwanza kwa Mtawala (Kiongozi) yeyote ni uwezo wa kutambua na kuteua watu wenye uwezo wa kutekeleza “vision” ya utawala wake. Kushindwa katika hili kunamwondolea Mtawala (Kiongozi) sifa ya kuwa kiongozi bora. Ni dhahiri kuwa wateule wa Kiongozi wetu wa Taifa wameshindwa kumsaidia na hivyo kuendelea kuwakumbatia kwa miaka 5 kunapelekea jamii kutilia shaka uwezo wake wa kuteua. Mungu Ibariki Tanzania

  • MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WANANCHI WAKE;kwa nyie wagombea litazameni hili maana inafika mahali ambapo tunaona ni bora tusingepata uhuru.maana wakoloni na uchache wao WALIWEZA KUFIKA HADI VIJIJINI.NYIE WABUNGE NA MA V8 & VX MNASHINDWA KUWAFIKIA WANANCHI WENU.MUNGU AWASAMEHE:

  • Watanzania tunahitaji kuondokana na mawazo mgando.Nimezifurahia sana comments za hapo juu lakini kinachotakiwa ni kwenda vijijini kuwaelimisha wanavijiji ambao bado hawajui hata maana ya maendeleo hususani mambo ya uchaguzi.Tusiwe wavivu wa kufikiri.

  • Tena anakuja kwa kasi zaidi nguvu zaidi na nyingine zaidi nyingi tu ILI TUENDELEE KUKOMA ZAIDI. tusipokaa vizuri tutateseka tena miaka mingine. TUMTOE JAMANI.

  • Jamani ukweli ndo huu, hakuna maisha bora na wala hatuko kwenye njia ya kuelekea huko, Kama asilimia ya budget inayokwenda kwenye garama za uendeshaji wa siri-kali haitakua adjusted na kiasi cha kutosha kuelekezwa kwenye kuinua maisha basi tujue ndo tunaangamia. Maneno matupu hayatutoshi! WATANZANIA TUAMKE!!

  • kila kitu wataahidi lakini mjinga ni yule anayechagua kwa sababu Tanzania tunaijua na viongozi tuna wajua tuwe makini tuache kuwa limbukeni hii Tanzania ni yetu tuijenge wenyewe sio mafisadi muda wao umeisha tubadilikie CHOOSE THINGS AT RIGTH TIME AND CORRECT PLACE

  • Without patriotism and avoiding egotism, the slogan cannot be met.Should we wait for the beautiful ones to be born in Africa particularly Tanzania? I think not instead let us wake up and join hands for the better future.

  • Hapa kwetu hatuna viongozi wenye uchungu na wananchi hasa wazawa,kama viongozi hao wangalikuwepo,umaskini kama huu haungekuwapo.kama huamini hilo angalia ni akina nani wanapewa mikopo,popote

  • Tunahitaji Mpango Mkakati Unaotekelezeka. Mambo ya ujumlajumla hatuyawezi. Umasikini bado ni janga la Kitaifa. wachache wanafaidi matunda ya Uhuru asilimia zaidi ya 90 ya watanzania ni Masikini wa Kipato.

  • Salome jibu ni kuachana na utumwa wa CCM ambao ni magwiji wa kutoa misamaha ya kodi ya Tshs bilioni 700 kila kwa mwaka kwa wawekezaji feki wa madini ambao wanahamisha malighafi za Nchi kiulaini na huku wakituachia mashimo. Chagua na hamasisha Chadema wakamate Nchi nao tuone watatupeleka wapi. Vinginevyo hivi vilio na kusaga meno kutaongezeka maradufu.

  • Napenda niongezee pointi za Pretty, Benson, Adam, jk na ndugu zangu wote walio changia kabla yangu. Kwanza pretty dua yako ipokelewe na mungu akubari mtoto mwema. jk, umemesema pointi nzuri. Lakini, hizi picha zina legend, ambayo mtu anaweza kufika. Kama hii blog inachapisha vitu vya uongo sijui. Nadhani pointi ya kutaka kujua how far are we on the poverty alleviation process. Jibu ni dhahiri tuko mbalisana, na sio tu Tanzania Nchi zote Africa, Ingawa zingine zinajongea mwendo wa kobe. Inawekana sio sisiem ya kulaum. Waafrika hatuthamini ubunifu. Majibu yako mbele yetu, lakini tunayapuuza. Hii mikakati yote ya tukukuru etc. ni kua watu wanajitahidi. Tatizo, ukiwa na plani hawakusikilizi mpaka baba yako awe mzee flani. Kwanza ningependa kujua viongozi wote what is their plan of action after they take office with a bit of time left? I have an answer to this. but i want to know who is going to use business effectively to fight poverty. kunawatu wali conjured the wajasirimali. kwanza inamaana gani? na lengo lake ni nini?

  • Damn you all supporters of foolishness and stupidity like “Maisha Bora Kwa Kila MTZ”, b’se inaonesha maisha bora yako airport anakoshinda huyu mjomba kila siku, maisha bora kwa mafisadi yanawezekana chini ya Ari “mpya zaidi” ya JK!!

  • I dont think only citizens can contribute to their development,they need some one to lead them that is (leaders).thats why we need to choose the leaders who seems so comitted to people and not(blaa blaa)and about (MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA)thats a dream kwa viongoz wa serikali ya CCM .Thats why they didnt attach those words this time.thanks

  • Matatizo ya management tanzania sio ya sisiem tu, ya watu wote, kwani hata kwa mfano chama kingine kiongoze, nadhani wafanya kazi ndio watakua hahawa, wafanya biashara ndio watakua hawahawa. Nadhani tuzalisheni kihalali zaidi. na uwe uwekano upo. aidha ni ccm au chadema cuf, you name it. Nadhani ni wananchi ndio wawajibike kuleta maendeleo kama ni kumvoti mtu out be it kama kuacha aendelee be it. Ubadhirifu na uzembe kazini hicho lazima ipungue sana hasa kwa viongozi. Na hii ni kwa vyama vyote nadhani.

  • ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania inahitaji political commitiment ya kweli sio maneno tu ya kusherehesha jukwaa la msimu yaani miaka mitano; picha nzuri congrats inareflect maisha ya mtz wa kijijini mama ktk picha number nne si mjamzito ana matatizo ya kiafya yaweze kua ana cancer ya ovaries yaani ovarian tumour au portal hypertension inayotokana na kichocho cha tumbo( complication) au matatizo ya maini yaani liver cirrhosis je tiba wapi je ushauri wa kitaalamu wapi haya ndo madhala ya siasa na hawa jamaa brabra hawawezi kuhachia donge la utawala maana walishatengeneza mfumo wa kuwalinda kuhakikisha wanatawala daima ntaendelea, i have to go, nachefuka

  • Maisha bora ingewezekana kama tu watu wangekuwa na hofu ya Mungu. Kwa hali halisi ya uongozi tulionao sijui, labda waachane na dhambi ya wizi hapo itawezekana. Damu ya Yesu ikabadili mtazamo wa viongozi wetu na iwapo roho ya huruma kwa wanaoishi katika mazingira mazito. Hizo fedha mnazolimbikiza na hayo magari mbinguni hamtaruhusiwa kuingia nayo wala kaburini hayaruhusiwi

  • inasikitisha, binafsi nimeogopa hata kutazama hizo picha. hivi kweli hawa ni watz wenzetu? hao wakuu wa mikoa/wilaya/mbunge/diwani wa maeneo hayo wanafanya nini?

  • Jamani hapa ndipo tunapoona umuhimu wa mabadiliko kesho ni siku ya uchaguzi mkuu je tutaendelea kuwachagua hawa viongozi wabinafsi mpaka lini?inasikitisha kuona baada ya miaka yote hii ya uhuru bado tunaishi maisha duni kupindukia.

  • The word “kila mtanzania” is so subjective but it doesnt limit any critical thinking on the slogan…I belive we can eradicate poverty only if our politicians would stop being selfish and become responsible for their actions and decissions.

  • Najisikia huzuni moyoni mwangu 7bu ya hawa ndugu zangu,naona ni jinsi gani baadhi ya viongozi hawaoni watanzania wanavyokufa bila ya wao(viongozi) kujisikia hata tone la uchungu.Natamani hata kufa nisione mambo haya.

  • Ili kuondokana na hali hii tubadili mfumo wa uendeshaji serikali. Machozi ya moyoni yananitoka kuona kuna watanzania wenzangu wanaishi maisha ya namna hiyo, wakati kuna sehemu anayo ishi kuna serikali kuanzia ngazi ya nyumba kumi, kata, tarafa, mbunge, wilaya nk nk. Ndg. Jenerali NAONA IMEFIKA HATUA TUKUBALI KULA NYASI ILI KATIBA MPYA iandikwe. katiba mpya itabadili mfumo ulioshindwa kutuletea maendeleo ya maana hasa vijijini. TULE NYASI LEO tupate pesa ya kutunga KATIBA MPYA ili tuondokane na usanii huu.

  • Tatizo letu sisi Watanzania tunachagua viongozi kama mtoto anadanganywa na pipi ili ameze dawa. Tunaendelea kuchagua viongozi ambao wameshakuwa madarakani na tukashuhudia wenyewe kwamba ahadi zilizowekwa zilikuwa danganya toto. Sasa tunadanganywa tena na tunadanganyika kama watoto na tunarudi palepale kwenye tulipotoka. Tunachagua kama vipofu na kulalamika kama vichaa hata mwezi haujaisha. Kwa nini tusifunguke akili?????

  • kweli inasikitisha sana, hizo picha zinatisha na zinanikumbusha mbali, niliwahi kutembelea sehemu za serengeti-Mgumu, kijiji cha machochwe nibaadhi ya maeneo ambayo wamebahatika kuwa karibu na national park lakini wanaishi maisha magumu sana. Hawana huduma za kijamii wakati sera zinasema jamii zilizopo adjucenrt to national parks wanastahili hizo huduma.Pia ukienda maeneo ya mpwapwa kijiji kama kisima ni kilometa chache kutoka dodoma mjini sehemu wanakokutana wabunge lakini wanaanchi wanakwenda zaidi ya km.12 kutafuta maji tena machafu lkn wkt huohuo utaona vibanda vya nyasi na matope*(TEMBE) vinapepea bendera za sisiem.Ukienda maeneo ya Tabora na Shinyanga ndo worse kabisa.Jamani tutajikomboa tu kwa kupeana elimu hasa ya uchaguzi kama walivyofanya baadhi ya wagombea kama mh.Slaa.Inafurahisha wanachi wengi wameshajua kwamba wanalipa kodi na kodi yao inapaswa kutumika kwenye utoaji wa huduma za kijamii

  • watu huwa wanadai maisha ya africa huwa ni magumu lakini si kuwa ni magumu tu bali hata viongozi wetu pia wanachangia kwa ugumu huwo.
    kwani south africa si ipo kwenye bara la africa mbona wenzetu serikali yao ina wajali tu.yaani mpaka sisi tunaoishi huku tuna waonea donge wanzetu.yaani ifikapo end of the month kwa mtoto tokea kuzaliwa mpaka 18years old na mtu mzima kuanzia 60years old mpaka kufa wanapokea mishahara yao kutoka kwaserikali kama wafakazi. na wagonjwa,
    viwete,vipofu wanapokea mshahara wa mana tu.
    sio lazima tufanane nao.lakini serikali yetu ingeamua hata kwa kuwasaidia watu wazima pamomoja na walemavu au wagonjwa ingepunguza kidogo aibu kwa nchi yetu ya tanzania.

    MUNGU ATUSAIDIE KATIKA KUUTOKOMEZA UMASKINI KATIKA TAIFA LETU…
    AAMIN.

  • These terrifying images tell a typical sorry state of affairs in rural areas…but, no this is too much, in this day and age,it is absolutely unacceptable. all of you who are responsible for this ugly mess-RESIGN immediately and repent for ur days are numbered!

  • Jamani maisha ni magumu kila kona haishikiki, labda wachache waliobahatika, lakini sisi watanzania wengi tunasota ile mbaya, kila kitu kimepanda bei,umeme ndo hivyo kama mimi mtengeneza barafu na mtaji wenyewe Mungu anajua, ki ujumla mpaka sasa sijaona maisha bora…natamani hata nikawe mkimbizi nchi nyingine labda nitapata haueni…khaaa!!!!!!!

  • Tatizo la kwetu watanzania ni kuwa hatujui haswa kinacho sababisha umaskini na kama tunajua hatujawa na uelewa wa kuki kabili.
    Kila mtu hujua umuhimu wa nishati iwe ni ktk mfumo wa gesi,petroli,umeme, au makaa ya mawe.
    Vitu hivi huweza hata kusababisha vita kutokana na umuhimu si tu kwa maendeleo ya nchi lakini kwa maisha tu ya kawaida ya siku hadi siku.
    Sasa je iweje tumvumilie waziri ambaye ameshindwa 1)Kutuepusha na mgao 2)Aliyeshindwa kutu onya juu ya mgao na badala yake kutudanganya eti umekwisha baada ya uchaguzi.
    Nayo Tanesco imeshashindwa kazi acha kampuni zingine zifue na kuuza umeme

  • After see those picture above till now I’m thinking who lead us to be partriotism people, If you want to love something don’t love it by all percent just think first then judge and if possible act like that in Tunisia and strick I like it but……..promisess like this are poisons to citizens who wats changes

  • After see those picture above till now I’m thinking who lead us to be partriotism people, If you want to love something don’t love it by all percent just think first then judge and if possible act like that in Tunisia and strick I like it but……..promisess like this are poisons to citizens who wants changes and if you don’t want changes better to stay beside and to leave those who what changes I vow from now never and again to loose direction to vote poiwsons leadership

  • These are just political lies and we should never entertain leaders like these who belive in mere words to fulfill their political ambitions.
    We should always deny to be prisoners of our own identity.

  • Kuna tanzania na tanganyika hizo picha ni tanganyika cyo tanzania.HIYO NI MIAKA 50 YA UHURU NA SHEREHE JUU NI KAMA MAIGIZO VILE ILA NI MAISHA YA WATANZANIA.INAUMIZA SANA…………

  • When someone tell you that Maisha bora kwa kila mtanzania know that is a killer. So be very carefully with him/her because he/she want to kill you. They have unimplemented plan. Now their un torelable let us join and disagree them.

  • YAAANI NI NGUMU KUZUIA MAUMIVU YA MOYO UNAPOTAZAMA WATU KAMA WEW WANAISH MAISHA YA NAMNA HII.TZ INA VIONGOZ WAUAJI NA HATA KM SHERIA ZINAWAKINGA KUWASHTAK AKIWEMO RAIS LAKIN MUNGU YUPO ATAWAHUKUMU TU,WAACHE KWAKIPINDI KIFUP HIKI WAISHI KAMA WAKO PEPON,LAKIN MUNGU WA WOTE ANALO JAWABU KWAJIL YAO NA RAIA WANAOTESEKA HVYO.KWELI KIKWETE NA SERIKAL YAKE WAMESHNDWA NA WAMEHARIB MPK VDG VILIVYOKUWEPO.TUAMKE TZ

  • ningefurahi kama ningeona upande mwingine wa maisha bora yaani kwa wale ambao wameyapata. hata hivyo kumiliki baiskeli siyo kitu kidogo mtu wa namna hiyo kipato chake ni cha wastani. na sasa tunatoka kwenye baiskeli tupo kwenye pikipiki hadi kijiji. tumesonga mbele kwa kiasi fulani na bado maisha bora yanashuka polepole yatawafikia

  • Your picture represent the reality of Poverty to most Tanzanian leaving in the villages.
    I was further shocked when you your writting was as if it is not known
    I will rather like to see that you written for people and leaders to trake action on peoples life under such missery.

  • Your text and photos show the reality of Poverty level to most Tanzanian leaving in the villages.

    I was further shocked when message/writting was publicity rather than seeking of remedy action people and leaders

  • siasa za nchi hii ni mbovu. hazina misingi ya uwajibikaji. nchi inaonekana mwenye nayo na kila anayepata uongozi anajinufaisha kwanza yeye, kiukweli wananchi wa kawaida hatutayapata haya maisha bora kama watu , hasa viongozi hawabadiliki. wanatukatisha tamaa sanaaa!

  • we cant judge only by pictures we stare on ryt now…and let us ask ourselves where does this good life starts??in the urban or rural??and how are we going to get this by waiting or working???let us start to work at ground level rather than waiting for our president.

  • inashangaza kuona maisha kama haya kwenye nchi yenye kila kitu,kam Tanzania. ili yote yaishe suluisho ni katba mpya itakayo ondoa matumizi mabaya ya fedha ya kununua magari ya kifahari wakati wenye NCHI yao wanatesaka kama ivi.jamani hi si haki bora kufa ukiwa shujaa kuliko kufa ukiwa mtumwa.katiba mpya KWA WATANZANIA WOTE.PAMOJA SANA

  • Maisha bora kwa kila mtanzania ni utani mtupu yani sawasawa na kusema kilimo kwanza wakati wakulima wakitumia zana duni za kilimo. Misemo mingine jamani angalau washirikishwe watalaam na siyo kuropoka tu.

    Kwakweli hali ya hizo picha inatisha, hayo ndiyo mambo ya chukua chako mapema.

  • nahisi kuchanganyikiwa…kwani hawa wananchi wenye halingumu kama hii hawana viongozi?viongozi wao wanawawakilisha vipi,wanawatumikia vipi?wabunge wa wananchi hawa ndowanaodai posho ziongezwe?kikwete alifika kweli kwa hawa wananchi na kuwaomba kula zao?kwanini waishi katika hali hii juu ya udongo wenye utajiri?NAZIDI KUICHUKIA SERIKALI YANGU YA SASA NA ZILIZOPITA KWASABABU HALI HII SIYO YA JANA WALA JUZI…MUNGU ALISHAIBARIKI TANZANIA

  • Assalam alehkum watz maisha bora kwa kila mtanzania inawezekana ila tatizo ni hao waliopewa majukumu kuishi maofisini kwenye viti vya kuzunguka wantamwona vipi huyu bibi wa kijijini ushauri wangu ni huu kwa mheshimiwa rais,waziri mkuu,mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,mkurugenzi wa mji…… waweke utamaduni wa kujulishana usalama wa watu wao kuazia ngazi ya chini kwani kwa kufanya hivyo basi watawafikia hata akina huyu bibi ,pia kwa wananchi wenzangu tuna jukumu la kuwahukumu wabunge,madiwani wetu….. kama hawatendi walivyo ahidi,inakuaje mbuge kachaguliwa wilaya ya kasulu au kiteto au same halafu yeye anaishi dar simuelewi na sitajaribu hata siku moja iliyobakia katika maisha yangu kumuelewa na nakuombeni wananchi wenzangu kufanya hivyo JK wafuatilie watu hawa kwa karibu

  • DAH kweli masha Tanzania bado kabisa we need much effort to building our nation

  • Subhannallah!Ewe Mollah tujaalie watanzania tuondokane na umasikini huu.

    Nasapoti wazo la viongozi kupata taarifa za maisha ya jamii inayomzunguka kuanzia Vijijini.

  • maendeleo hayaletwi na wananchi pekee ndio maana kuna kuchagua viongozi wa kuwaongoza wananchi kufikia maendeleo licha ya hivyo wananchi hawa wanalipa kodi.mafuta ya taa,kiberiti,sukari,pipi,kalamu,mswaki na vyote mwananchi wanavyotumia ameshalipa kodi.

    Hivyo maendeleo duni kama ya leo Tanzania yamesababishwa na viongozi wetu wabovu.Kiongozi anayefanya maamuzi mpaka wabunge hasa wa upinzani wafoke Bungeni na kutishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu ndipo afanye maamuzi huyu naye utasema kiongozi!Maovu yote yanayofanywa na viongozi hawa(Mawaziri) mh.anayajua,alipaswa kufanya maamuzi mapema hata kabla ya Wabunge hawajayajua haya kwani ye ndo mwenye mamlaka lakini kimya kimya kimya kimya.

    Kwa hali kama hii maendeleo Tanzania itabaki kuwa kwa viongozi na si kwa WANANCHI.

  • I think the better life 4 every tanzanian is converse. may BE this be better life 4 ever government leader.

    If U try TO BE kin enough when u look at the picture u can realize that this is the country we say democratic.while SOME of our fellow dying of hunger diseases unatended and human right are violated sick one have decided to die slowly every thing is now sold at high price.

    Did we elect trouble or what? where are u carry us to mr PRESDENT is this ur promise to us? if the vip is sick u here south africa!! india!! londo!! and how about that mother in the picture?ahe dont have even acsess to the hospital even if she get there dr are not there becsa of strike and if she lucky enough doctor happen to help her no drugs no medical equpments and the doctors are already demolarized by the KAMA KUNA DACTARI HAWEZI KUFANYA KAZI BILA MILLION TATU AACHE KAZIDO U CAN THINK TWICE IF THEY ALL SAY OK DO U THINK UR WOULD BE THERE.here is where we are and we are here because of our choice we made.

    It’s not too late we can change our ideals to elect person WHO is able to lead us, and political party TUNAZOSHABIKIA. WE CAN CHANGE THE WAY WE ARE THE POWER IS WITHIN OURSELVES TUACHE UCHAMA TUANGALIE UWEZO

  • kama ahadi tumesha ahidiwa sana but atuoni utekelezaji so what2 do! mi naona aina maana kuongozwa na viongozi ambao wana jali maslai yao bila kuangalia damu ya mpiga kula inavyo mwagika msabani.

  • just wano say u guys you have a good presso.He is putting the right policies in place,the rest is for Tanzanians to grab the opportunities n capitalize on them for your own betterment.

  • uongozi kwanza ni kipaji,kama huna kipaji cha kuongoza,hata ukienda shule,utajifunza kusimamia,kukemea,na kuchekacheka hovyo.

  • Well travelling on a bycicle is not new neither sign of poverty, well a lady in that mud house and the other with ascites if be, are in a condition needing assistance, but somehow managing to make a living in difficulty.

    My comment on this is if the President's promise on the better life for every Tanzanian, meant seeing non of those, then that was a utopia (daydream), otherwise, I think meant to pave way to this end where every Tanzanian will see light of not starving, having access to health services (not treatment of diseases only) and a shelter as that is what we call basic needs (food, shelter, education and care). Then I can assure you that the policies developed like the MMAM in the health sector, shule za Kata in education and Kilimo kwanza in agriculture, are all geard towards this end. We are not going to realise this now (very recent) but think of it in a near future that kila mwana kijiji have gone up to form 4 and in a neighbourhood a facility providing health services is available.

    Is it not something?

    We do not have that capacity of running to success, but we are going towards it, not at a snail speed but at a certain speed, mazuri hayahitaji haraka. Badala ya kuangalia hiyo mifano pekee, angalia pia maeneo yenye mafanikio. Hata hivyo sina maana kuwa hatuhitaji kuwa mbele zaidi, lakini uwezo wa kukimbia ndio bado mdogo.

    GESI YA MTWARA basi itukomboe, ila taabu ni hiyo wa Mtwara hawataki iwakomboe wengine ila wao tu, na wanasema mambo bado, haya yetu macho

  • nakubaliana na wanaotaka mageuzi sijui yapi, na kuona kuna nini huko mbele, lakini mimi bado naamini kuwa Kiongozi mzuri bado atatoka CCM hata kama ni baada ya ku-defect, maana hiyo kwa sasa inayo bank ya viongozi wazuri, na tatizo labda hatujawa-tap. waingereza walisema ni mvaa/mwenye kiatu anayejuwa palipo msumari unaochoma, waswahili wakasema ZIMWI LIKUJUALO …. na pia usilolijua ni usiku wa …. alamsiki

  • kiukweli wanatia huruma sana maisha bora kwa kila mtanzania ni yapi hayo mbona hatuyaoni? zaidi ya kuangamizwa tu, ebu muangalie na upande wa pili tu siyo unakura raha uko nasi mnatuacha tunatesekani bora kijana kuliko mzee kama huyo sasa inakuaje anasikitisha sana jamani anahitaji msaada.

  • Mimi sijui kweli,hawa viongozi wetu wana maanisha nini!jamani watu wanateseka tuache utani

  • Hivi hawa viongozi wetu ni vibofu au viziwi kweli hawaoni au kusikia  haya maisha ya wananchi wao utawaona wakati wa kampeni wakigawa t shirt na kanga. Lakini Mungu anaona. Jamani tugeuke pamoja na umaskini wetu

  • kwa mtazamo wangu, tukiishi kwa ahadi za hawa viongozi wetu tutapoteza maisha ya watanzania wenzetu ni vyema tukaludisha mioyo yetu ya zamani ya kusaidiana japo kwa kidogo mungu anacho tubariki

  • Hii nchi inamwitaji Mungu wa kweli so wapendwa tuamke kutoka usingizi tumwite Mungu coz yeye c dhalimu utatusikia na kuiponya nchi yetu kwani haki huinua taifa na haki haiwezi kupatikana pasipo maombi,ni hayo tu wapendwa kwa leo.

  • Kama mafisadi watabanwa, na tuchague viongozi wenye uchungu na nchi yetu, huruma kwa wenye shida na wanaomwogopa Mungu, ndipo maisha yatakuwa BORA kwa Mtanzania. Nia ya Mh. Rais Kikwete ni njema, lakini watekelezaji ndio tatizo. Naye anakuwa mzito sana kuwachukulia hatua, kwa sababu ambazo mimi sizijui. Sababu ufisadi mwingine uko wazi mno, hata raia wa kawaida tu anauona.

  • Hakuna cha "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania", Ni maneno matupu tu yasiyokuwa na vitendo ndani yake ili kwamba aonekane ana huruma sana na ni mtu mwema kwa walengwa, kumbe si lolote si chochote. Gia tu ya kutaka kupata kura ili iwe rahisi kuingia madarakani.

  • dah! sooo sad!!!

    Ila kweli mtu kama huyu ambaye hata uhakika wa menu ya kueleweka hana serikali inamfikiria kweli??

  • maisha bora kwa kila bado ni ndoto hasa kwa watanzania wa taabaka l achini.maisha bora yatawezekana tu endapo rasilimali za nchi zitaachwa kwa watanzania wote na endapo tu mikataba mibovu itrekebishwa.MUNGU Ibariki tanzania

  • Maisha bora bado ni ndoto hasa kwa watanzania wa tabaka lla chini na badala yake Mmaisha yamekuwa bora kwa wale tu walioko tabaka la juu.JE NINI KIFANYIKE?

  • ni kweli mheshimiwa aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania lakini mambo mawili yamekinzana maana yeye amekuwa na moyo wa dhati kabisa wa kubadilisha maisha ya watanzania lakini wasaidizi wake waliopewa dhamana ya kusimamia ndo wamekuwa watumwa na mateja wa kuangalia maisha yao binafsi kwanza na ya watanzania wengine baadae hivyo inamuwia ngumu kukamilisha ahadi hiyo maana hawezi kusimama pekeyake kilicho athirika ni mioyo ya wapewa dhamana wanahitaji chakula cha moyo ambacho ni kufuata vitabu na maagizo ya mungu tu maana kama ni vikao na auditing vimefanyika saaana ila mabadiliko hakuna hivyo turudi katika kitabu cha mungu ugonjwa wa moyo utatibika

     

  • Watanzania sisi wachawi wenyewe wa maendeleo yetu….

    Tulipigwa chenga la macho, jamaa alitwambia maisha bora kwa kila mtanzania, lakn hatukumkalisha chini aeleze anamaanisha nini? Namna gani na nani? Lini na wapi? Tuliishia tu kucherekea theoretical kama kawaida yetu, na kukumbatia vitenge, kofia na kununuliwa pombe….tutaendelea kulizwa na kulizana because we don ask questions…and we hate reflections…

    hahahhahhahaha Tanzania….

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *