Mlundikano wa wanafunzi darasani

Albano Midelo

TATIZO la mlundikano wa wanafunzi darasani hapa nchini imekuwa ni moja ya mambo ambayo yanachangia kushusha kiwango cha elimu,wanafunzi hawa wanasoma katika shule ya msingi Mkili kata ya Ngumbo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, shule hii inakabiliwa na tatizo hili karibu kila darasa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo John Ntaga anasema kwa wastani kila darasa lina wanafunzi zaidi ya 75 hali ambayo inasababisha wanafunzi kuwa wengi. Shule hiyo ina wanafunzi 500 ambao wapo katika mikondo 14. Shule ina upungufu wa walimu na vyumba vya kusomea.

Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Mkili mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma ambao wanakaa dawati moja watoto kati ya watano hadi sita tofauti na utaratibu ambao unataka dawati moja kukaa wanafunzi wawili hadi watatu.Hali hii inachangia kususha taaluma katika shule hiyo.

1 Comment
  • Mimi jina langu sultan nilimaliza darasa la saba shule nyasa nzega mwaka wanafinzi 1975 mwaka huo tulikuwa 30 katika darasa moja, kwa ukweli ninasikitika sana kusikia habari ya kuwa darasa moja lina wanafunzi 75.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *