Shughuli za kiuchumi kwa Vijana wa Wilaya ya Kisarawe na changamoto zao

Belinda Habibu

Kama ilivyo kwa vijana wengine hapa nchini, wale wa wilaya ya Kisarawe wanajihusisha na shughuli mbalimbali.

Wilaya hii imejaliwa vitega uchumi vingi kama maliasili nyingi ( misitu, ufugaji wa nyuki, madini ya kaolin, kokoto, na mazao ya chakula na biashara.

Kwa kutumia rasilimali hizi, vijana wamegawanyika katika utendaji wa kutumia rasilimali hizo,wengine wakulima,wafugaji,wachimbaji madini, mafundi na waendeshaji wa vyombo vya usafiri kama pikipiki ( boda boda).

Noel Daniel Udulele ni mmojawapo wa kijana katika wilaya hii, anasema alipata mafunzo yake ya ufundi selemala katika chuo cha VETA jijini Dar es salaam, na alipohitimu alijiajiri mwenyewe.

Ameongeza kazi yake ina ugumu kidogo kwa sababu ya upatikanaji wa mbao sio rahisi kwa sasa na hasa kwa miti migumu na kumlazimu kutumia iliyo laini ambapo wateja wengi hawaipendi sana.

Akizungumzia changamoto nyingine inayomkabili alisema ni mtaji wa kuweza kupanua ofisi yake,na kuongeza unajua suala hili linawauumiza vijana wengi,na ukisema uende benki nao wanamasharti mengi na kuwa kikwazo

Kijana mwingine aliyejulikana kwa jina la Mikidadi Shukuru ambaye ni mchimbaji wa kaolin katika machimbo ya Dongo jasi wilayani humo alisema kazi wanayoifanya ina ugumu kutokana na kipato kinachopatikana baada ya uchimbaji.

Alisema kwanza vifaa vyao vya uchimbaji ni duni wanatumia sululu, chepe na viroba, inayowachukua muda mrefu kupata madini hayo na wanauza kwa lori sh.70, kwa kuwa anachimba na wenzake wakigawana wanapata hela ya kula tu na si ya kujiendeleza zaidi.

Vijana hawa hawafahamu kuwa halmashauri yao ina kiasi cha fedha katika bajeti yake kinachoweza kuwawezesha kimtaji.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hii Yona Maki alisema katika pato la halmashauri asilimia 10 ya pato lote linakwenda kwa wanawake na vijana.
Ameongeza kuhusu uchimbaji wa kaolin ni lazima uwekwe katika kipaombele cha halmashauri, kwani inatoa ajira kwa wakazi wa hapa na hasa vijana.

Mkurugenzi huyo ameongeza ili waweze kuwezeshwa kimtaji vijana lazima wawe katika kikundi cha watu 10 na kuendelea.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *