Trump ashangaa kuanza zoezi la kuhesabu upya kura, amtaka Hillary Clinton kukubali amemshinda

Jamii Africa

Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump ametoa tuhuma kuwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 8 mwaka huu mamilioni ya watu ambao hawakustahili walipiga kura. Trump amedai kuwa angeshinda kwa kishindo zaidi iwapo wapiga kura wasiostahili hawangepiga kura.

Ametoa kauli hiyo kufuatia aliyekuwa Mgombea wa chama cha Green, mwanamama Dkt. Jill Stein kuanzisha mchakato wa kuhesabiwa kura upya katika Jimbo la Wisconsin.  

636071360936144661-xxx-jillstein-4

Aliyekuwa Mgombea wa Chama cha Green aliyeanzisha zoezi la kuhesabu upya kura

Mwanamama Jill Stein amependekeza pia kuhesabiwa upya kwa kura katika majimbo muhimu yenye wajumbe wengi(Electoral College) ya Michigan na Pennsylvania akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika zoezi la kuhesabu kura.

Wiki iliyopita wataalamu wa TEHAMA nchini humo walidai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika Majimbo hayo matatu na kupendekeza kambi ya mgombea Hillary Clinton iitishe upya zoezi la kuhesabu upya kura katika majimb hayo.

Rais Mteule Trump ametoa kauli za kushangaa zoezi la kuhesabu upya kura likiungwa mkono na Hillary Clinton akidai kuwa yeye ndie Rais aliyeshinda na kwamba juhudi za kuonyesha kuwa hakushinda kihalali halitafanikiwa na upotezaji wa fedha bure.

Hillary Clinton aliyempita kwa zaidi ya kura milioni mbili katika kura za jumla(Popular Vote) Rais Mteule Trump, ameunga mkono zoezi la kuhesabu upya kura katika majimbo hayo matatu muhimu.

Aliyekuwa Meneja wa Kampeni wa Trump, Bi Kellyanne Conway amemtaka Rais Mteule Trump kufikiria uwezekano wa kumfungulia mashtaka Hillary Clinton kutokana na kashfa ya kutumia anuani yake binafsi ya barua pepe alipokuwa waziri wa mambo ya nje.

Rais Mteule Trump alishinda Uchaguzi kwa kupata  kura za wajumbe 290 huku Hillary  Clinton akipata kura za wajumbe 232, lakini Clinton akipata kura za jumla milioni 64.2 na Donald Trump akipata kura za jumla 62.2 ikiwa ni takribani tofauti ya kura milioni 2.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *