Serikali ya Tanzania haipo tayari kutekeleza malengo ya milenia yanayotaka kufikia mwaka 2015 kupunguza vifo vya mama na mtoto kufikia asilimia 75 kati ya vizazi hai 100,000.
Hali hiyo inajidhihilisha kutokana na uhaba mkubwa wa maji na miundombinu kadhaa katika sehemu za kutolea uduma za afya likiwemo tatizo la umeme ambapo kutokana na mfumo wa serikali kuamua kutumia Luku hospitali nyingi wanapata shida hasa wakati wa upasuaji(Oparation) huku wakihofia unit kuisha maana ukinunua umeme mwingi na hata makato wakati wa kununua tena yanakuwa makubwa zaidi na bajeti hazitoshi.
Katika hospitali ya Manyamanyama Wilayani Bunda mkoani Mara wataalam akiwemo muuguzi mkuu wa hospitali hiyo Adelaida Masige anasema kuwa ni vema serikali ikabadili mfumo huo wa Luku katika hospitali zinazotoa huduma za upasuaji.
Kwa upande wa vyumba vya kulaza wagonjwa ni vidogo kwa mfano ni katika hospitali ya Butiama ambako chumba chenye dirisha moja kina vitanda kumi na hewa ni ndogo kintumika na wagonjwa wenye magonjwa tofauti.
Katikawodi ya watoto Butiama wanalazwa watoto wanne wanne katika kitanda kimoja ambapo wakiwa na wazaazi wao wanalazwa watu nane hivyo wengine kulazimika kulala sakafuni.
Wanawake wajawazito wanalazimika kutumia choo cha nje kilichopo umbali wa mita thelathini hali ambayo ni hatari na wanaweza kujifungulia chooni huku wengi wakiwa na upungufu wa damu.
Katika zahanati ya Bunda zahanati hiyo chumba cha kuchomea sindano hakina dirisha hali ambayo inatakiwa miundombinu ya zahanati hiyo irekebishwe haraka.
Katika kituo cha afya cha Ikizu wilayani humo familia mbili za watumishi hazina choo wala bafu kutokana na choo walichokuwa wakitumia kubomoka hivyo kulazimika kuchangia choo na wagonjwa wanaolazwa katika kituo hicho cha afya na kinatumika na wagonjwa wa nje.
Vifaa tiba
Kuna uhaba mkubwa wa vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya katika mkoa wa Mbeya na Mara vikiwemo vya kusaidia wajawazito wakati wa kujifungua zikiwemo Suction Machine, Musk bag, sindano za kuchoma kwenye mapaja ili kumsaidia mama baada ya kujifungua ili kutoa kondo la nyuma, glovu na dawa zenyewe.
Kwa mfano katika hospitali ya Butiama, madaktari wanalazimika kuwatoa kondo la nyuma akina mama baada ya kujifngua kwa njia za zamani kwa kuvaa glovu kwa kuunganisha kisha kuwaingiza mikono ukeni nah ii inaonesha ni jinsi gani hawajapata mafunzo ya kisasa ya kutumia sindano.
‘’Tunalazimika kufanya hivyo kuunganisha glovu ili kutoa kondo la nyuma la mama aliyejifungua kutokana na kutokuwa na glovu maalum ambazo ni ndefu zinazofaa kutumika na kutokuwa na sindano za kuwachoma kwenye mapaja ili kondo la nyuma litoke lenyewe’’ anasema kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Joseph Musagafa.