VIDEO: Ofisa wa TRA Arusha akichukua rushwa waziwazi!

Jamii Africa

Video hii imerekodiwa kutoka kwenye simu ya mkononi na inamuonyesha Ofisa wa TRA Arusha akipokea rushwa toka kwa mteja ili aweze kumhudumia.

Ofisa huyu yupo mapokezi (reception) na inadaiwa ni kawaida yake kupokea Rushwa na kuwa usipompa anadai kwa nguvu.

Wafanyakazi wa TRA na wakubwa zake inadaiwa wanajua kinachoendelea lakini hawachukui hatua.

Kuna utendaji mbovu, lugha chafu kwa wateja na za majivuno na mambo mengi yanayofanana na hayo.

Mamlaka husika zinaombwa kuingilia kati TRA Mapato, (karibu na Benki Kuu tawi la Arusha) ili raia wapate huduma bila vikwazo vya rushwa toka kwa maofisa kama huyu.

19 Comments
  • Haya ndo maisha halisi na watanzania kwa ujumla.hivyo watanzania wazalendo kuwa macho

  • Natamani kuona wahusika wakimchukulia hatua huyo Jamaa. Kusema kweli sehemu nyingi sana zimeharibika. Kinachonitesa kwenye akili yangu kila siku ni kwamba, UZALENDO Nchi hii maana yake ni nini? Kwani wengi wa Viongozi wetu walipitia haya mafunzo, ila sijui wamesahau!

  • Hatakama tukisema hafai wakati ndio uti wa mgongo wa nchi yetu bado watanzania tutaibiwa mali zetu na watu wachache na hatakama tukilalamika hakuna atakae tutetea chamsingi kila mmoja wetu achunge mzigo wake….!

  • Aibu ya watanzania, nchi itabarikiwaje wakati watu kama hawa wenye kipato chenye afadhali kuliko sekta nyingine wanakuwa namna hiï?

  • AIBU YA MWAKA 2013!

    EMBU NIULUZE SWALI MOJA , MPAKA WATEJA WANAAMUA KUFICHUA HALI HIYO JE HAMNA KAMATI YA MAADILI TRA KAMA ILIVYO AGIZA SERIKALI ? KAMA IPO NA WATU WANASEMA NI KAWAIDA YAKE , JE HAWAJAWAHI KUSIKIA ? TUSIONEANE AIBU JAMANI TULELEKEZANE KWA UPENDO … 

     WANANCHI TUNATAKA TUSIKIE MATOKEO YA AIBU HII . 

    • Wapo wengi sana wafanyakazi wa aina hyo karibu kwenye mashirika yote ya umma na hakuna hatua zozote wanazochukuliwa kwani hata hao viongozi wao nao ndio wala rushwa wakubwa sasa nani atamfuatilia na kumkataza mwenzie nchi ishakuwa pabaya sasa

  • Kusema kweli serikali yetu inabidi iwe makini na hawa watu, kwani ndio wanaoirudisha nchi yetu nyuma, kwanini tusiwe kama China?

  • Jamani Arusha Traffic police wamezidi sana. Sasa wameanza kutoza ushuru kila kona na kila barabara asubuhi mpaka jioni.

    Kisa wamepewa malengo kukusanya 13billioni.

    Mbaya zaidi nusu ya makusanyo ni zao mfukoni.

    Jamani tushikamane tutokomeze uonzo huu.

  • dooh…

    sasa tazama hiyo ni hali  halisi kila kona na kwenye huduma za jamii.

    Mwananchi anayehitaji huduma ikiwa ni haki yake anatozwa fedha, je na sisi watanzania ndio tunaelea hili swala la rushwa.

    wenzetu ulaya jamani wameelimika mtu akikuomba rushwa mlipue tu.

    Naudhika sana ikiwa nafahamu na kutetea haki za wanyonge, mimi ni mtumishi wa serikali ambae nimekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo viovu na vinavyopingana na taratibu kanuni na sheria za kazi.

    Msolo Pagazi

  • TAKUKURU wajibikeni hapa manake ushahidi umeshafika kwa umma tayari, sidhani kama kesi ndefu inahitajika hapa. #ChangeTanzania

  • Hatua za kisheria zichukuliwe haraka sana kwan tukisubir hadi Edward Hosea ambae kazi yake haitambui na analipwa mshahara usio na kazi….hii tabia ikomeshwe Rushwa rushwa rushwaaaaaaa…….

    Tuitokomeze rushwa kan kwa maana hyo kwa cku huyu mfanyakaaz anatoka na milion kwa hezsabu zaharaka haraka kwan ni wengi mno wanaenda kupata huduma hyo kwake…

  • kwakeli hali mi mbaya, huyo jamaa  inafaa awajibishwe ili asitishe huo mchezo, maana inaoneka ameozoea sana na ndio maana hana hata chembe ya woga, arobaini yake imefika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *