WAFANYAKAZI wanne wa hospitali ya mkoa wa Kagera wakiwemo wafamasia wawili wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuiba dawa za wagonjwa zenye thamani ya shilingi 480.000.
Kaimu kamanda wa polisi Vitus Mlolele ameieleza Fikrapevu kuwa watuhumiwa hao walitiwa mbaloni May 31,wakiwa wameishaiba makopo thelathini ya dawa aina ya cotramoxazole na septrin yakiwa njiani kusafirishwa nje ya hospitali.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Peter Joseph9 (29) na Japhet Anthony (25) wote wakazi wa eneo la Kashai mjini Bukoba na kuwa walikuwa wakijihusisha na shughuli za usafi hospitlaini hapo.
Wengine ni Alexander Ndyamukama (53)na Rukahia Lushaka (27) wote ni wafamasia katika hospitali ya mkoa na wanadaiwa kumiliki maduka ya kuuza madawa baridi ya binadamu.
Aidha kamanda Vitus Mlolele ameeleza kuwa mfamasia mwingine aliyemtaja kwa jina la Willison Kazaura bado anasakwa na polisi baada ya kutoroka na kuwa anahusika katika wizi wa dawa hizo.
Pia amesema uchunguzi bado unaendelea na kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Shame, shame, shame…
There is a need to differentiate between pharmacist and Assistants. Rushaka is not even a pharmaceutical staff she is a Lab Tech.
Jamani wahudumu siyo wafamasia.
Hii aibu kwa wafanyakazi wote wenye tabia za udokozi, kwani mbona ni wengi na wanamiliki Phamacy, Mungu tusaidie!!