Wakurugenzi wa Halmashauri za Misungwi, Sengerema kupanda ‘kizimbani’

Jamii Africa

karibu misungwiKUFUATIA kuwepo kwa tuhuma nzito za ubadhilifu wa fedha za miradimbali mbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, imeelezwa kwamba, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Xavier Tilweselekwa ameshushwa cheo.

Mbali na madai hayo ya kushushwa cheo, taarifa nyingine zinadai kwamba Mkurugenzi huyo kesho Jumatatu huenda akafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya tuhuma hizo za ubadhilifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri yake hiyo.

Aidha, inadaiwa kwamba, mbali na Mkurugenzi huyo wa Misungwi kudaiwa kukalia ‘kaa la moto’, tuhuma kama hizo zinasadikiwa kumkumba pia Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani hapa, Erika Musika.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo hazijathibitisha na upande wowote, zinadai kwamba, Wakurugenzi hao wapo kwenye hatihati kukumbana na mkono wa sheria, kutokana na halmashauri zao kudaiwa kutumia vibaya fedha za maendeleo zilizokuwa zikitolewa na Serikali.

FikraPevu imewahi kuandika habari za tuhuma za ubadhilifu huo wa fedha unaodaiwa kufanywa na halmashauri hizo mbili za Misungwi na
Sengerema.

Baada ya safu hii kufichua tuhuma hizo nzito, vyombo vya dola ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, vlianza kuwahoji mmoja baada ya mwingine watuhumiwa wa ufisadi huo, na baadaye FikraPevu ikapata taarifa kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujitu tuhuma zinazowakabili.

Kufuatia hali hiyo, hivi karibuni, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ametoa ripoti ya ukaguzi wake, ambapo halmashauri
ya wilaya ya Misungwi imepata hati chafu.

Wakati Misungwi wakipata hati hiyo chafu, halmashauri ya wilaya ya Sengerema ni miongoni mwa halmashauri zinazotuhumiwa kutumia
vibaya fedha hizo za umma.

Kufuatia taarifa hizo za kutaka kufikishwa mahakamani, ikiwa ni pamoja na kushushwa vyeo vyao, inadaiwa kwamba, siku ya Ijumaa wiki hii
Maofisa wa Usalama walizuru katika ofisi ya Mkurugenzi wa Misungwi, kisha kukutana na mtumishi huyo wa umma.

Taarifa zilizolifikia FikraPevu jioni ya leo kutoka wilayani Misungwi zinadai kwamba, maofisa Usalama hao walienda kumkabidhi rasmi barua ya kushushwa cheo Mkurugenzi huyo, Tilweselekwa.

“Ijumaa Maofisa wa Idara ya Usalama walikuja kisha kukutana na Mkurugenzi ofisini. Tunadhani walimletea na kumkabidhi rasmi barua ya kushushwa cheo.

“Unajua, mlishambuliwa sana kwa maneno mlipokuwa mkiandika habari za tuhuma hizi za ufisadi Misungwi. Lakini yamefika wapi?.

“Ukweli daima haufichiki. Tunawashukuru sana waandishi wa habari kwa kufichua ukweli na Jumatatu tumesikia huyu DED anaweza kufikishwa mahakamani”, kilisema chanzo chetu cha habari kutoka wilayani Misungwi na Mwanza.

Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – FikraPevu, Mwanza

5 Comments
  • Kweli mtu anapatikana na tuhuma halafu anashushwa cheo????

    Ama kweli Wahenga hawajakosea usemi huu:

    Kikulacho hakika kipo nguoni mwako.

  • Mla, Mla Leo Mla jana sijui kala nini, Ni kweli wewe Missungwi kuna ubadhilifu wa Chapaa hizo za dola lakini, Mimi naamini unasulubiwa kutokana na kuwa Mtu mwenye dhamana na hasa ikizingatiw wewe ndiye Mhasibu mkuu wa Halmashauri, lakini kama m2 anaye muamini Mungu endelea kuomba Bila kukoma, Mwisho wa siku tutawajua wale waliokuwa wakienda kupata Bata kwa pesa ya Umma halafu mwisho wa siku wewe umefanywa kuwa Kilongola, yaani KONDOO WA KAFARA.
    MUNGU YU NAWE JIPE MOYO UTASHINDA

  • Machozi anayolia mtanzania leo, majibu yake yataonekana kesho, najua wachache mtanielewa kwa hili lakini ukweli ni kwamba adhabu itakayotolewa na wapiga kura wa Missungwi nikiwemo mimi, itashangaza ulimwengu.

    Ikumbukwe kwamba mh, Charles Kitwanga alikuwa mbunge wa pili kuwa kati ya wabunge walioshinda kwa kura nyingi zaid katika uchaguzi 2010, hivyo matarajio ya wananchi yalikuwa makubwa sana, all in all, Bernad POLYCARP anafanya nn?, Mkurugenzi anafanya nini? au ndo janja ya nyani, nashukuru kwa taarifa hii imenifanya nifumbue macho, mwezi wa saba nadhan ntakuwa huko, tutafanya mkutano wa hadhara kuwafumbua macho wananchi kwa yote yanayotendeka halmashauri, tunaomba uzidi kutupasha yanayojiri

  • Xavier Tilweselekwa:
    Mimi nashawishika kukupa pole kwa yanayokukuta kwani si mamlaka yangu kusema unatuhumiwa maana mamlaka hayo sina. Hata hivyo, imani yangu ni kwamba yanayokukuta hayana tofauti na yaliyomkuta ‘Mchapakazi’ Lowassa – uwajibikaji. Lakini ukweli utabaki kuwa pale pale, Misungwi uliyoikuta 2008 si Misungwi unayoiacha 2011. Wenye macho tunaona. Labda upole wako ndio umesababisha hawa mchwa wakatafuna hadi koti lako. Bwana awe nawe ktk kuueleza umma ukweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *