Washika mipini mnawahisha mazishi ya CCM kabla ya 2015

Jamii Africa

BADO najiuliza kwa nini “washika mipini” (Spika, Majaji, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri, n.k) kwa maksudi wanachukua maamuzi ya kusiliba kaburi la ccm? Hakuna hata mmoja anajifunza kutokana na makosa yake ya awali au ya mtangulizi wake!

Mbunge waa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye alifukuzwa ndani ya ukumbi wa Bunge Jumanne Juni 19, 2012

Tuliona la Dr. Slaa na EPA Bungeni mwaka 2007, CDM wakashinda kesi Mahakam ya Wananchi na bado wanazidi kuvuna riba ya makosa yalitokana na udhaifu wa Bunge la wakati ule. Ikaja mwaka 2008 Zitto akafukuzwa Ubunge, wimbi la ushindi wa kuungwa mkono na wananchi likaendelea kusimama upande cha CDM. Bunge jipya 2011 tumewabeza CDM na Katiba, leo hii tunafakamia matapishi yetu tukiwa chooni kwa wapinzani. Juzi juzi tu Jaji wa Mahakama katika kesi ya Uchaguzi wa Arusha, kwa kufikiri amefanya kazi ya kusifiwa na chama, kaleta balaa uraiani kwa kumuacha Godbless Lema alande lande nchi nzima. Sasa badala ya watu wa Arusha wavue magamba, nchi nzima hata watoto wanavaa magwanda. Bado tu hatujajifunza wala kuwafunza au kuwaeleza watoa maamuzi kwamba; chonde chonde kujipendekeza kwenu kwa nia ya kuinusuru Chama Tawala, serikali na Taasisi zake (Bunge, Uraisi, Mahakam) havisaidii bali ndo vinamwaga petrol kwenye tanuru la kuni kavu za zinazoiteketeza serikali! Wananchi wa Tanzania ya leo, si wa Tanganyika ya Mwaka 1947! Wana maamuzi rohoni mwao tayari kwa kiama cha serikali yao hapo mwaka 2015.

Ukiyatazama haya yote huwezi kuja na uamamuzi kama wa leo juu ya JJ Mnyika. Watoa maamuzi wa serikali yetu ya ccm lazima wajue kuwa hawa CDM  wakati mwingine wanachezea sharubu za simba maksudi kwa sababu wanajua Simba mwenyewe ni wa plastiki. Na akibahatika kuwa na betri yenye chaji inayomwezesha kuunguruma basi ni furaha zaidi Maana watoto wa wana CDM wanafaidi muungurumo wake!

Hivi kuna upya gani katika neno *“UDHAIFU”* lililosemwa na Mnyika leo Bungeni? Mbona watu wengi sana ikiwemo viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa wamelisema na kulirudia neno hili na wakilihusisha na Taasisi ile ile (Rais Kikwete) bila kuchukuliwa hatua yoyote?

Juzi Prof. Lipumba kasema wazi *Rais JK *ni *dhaifu* na kaenda mbali zaidi kumsifia Mkapa na utawala wake. Mh. Sitta akiwa Spika aliwahi kusema “kiutu uzima” kuwa *“wewe rais umekuwa mpole mno” *Hapa kwa wenye kung’amua Sitta alitumia uungwana tu kukwepa kutumia neno DHAIFU. Angeweza kusema *“wewe rais umekuwa DHAIFU mno*”. Pia mwandishi Kondo Tutindaga – katika MwanaHalisi ya tarehe 01 June 2011 iliyobeba kichwa cha mada “ Ni ubaya wa Lowassa au udhaifu wa JK?” alitumia neno “UDHAIFU” kama kisifa cha Rais JK si chini ya mara 15. Upya uko wapi mpaka huyo Spika anampa Mnyika kupiga penalti kwenye goli lisilo na golikipa?!

Hapa chini ni baadhi ya waandishi wachache tu miongoni mwa Watanzania lukuki walisema hadharani UDHAIFU wa Rais Kikwete

—Quote—
Kondo Tutindaga
………..Hali ya nchi kwa sasa ni tete kisiasa, kiuchumi na hata kijamii.  Wale wanaojipendekeza kwa Rais Kikwete ni wepesi kumshauri kuwa  anayesababisha haya ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na  wengine wanamwambia sababu ni mapacha watatu. *Hakuna anayemwambia rais  kuwa udhaifu wake ndicho chanzo cha utete wa taifa*…………
—End Quote—

—Quote—
Pasco
Nimemkumbuka Nyerere, angekuwepo, tusingefika hapa!. Tukiwaambia *JK is a  weak president,* watu hawataki kukubali!. Hao masheikh wa kukundi cha  Uamsho, wanakuwa tolerated under pretex ya religious tolerance hivyo  kutenda vitendo vya jinai ya uhaini kwa muda mrefu na kuachwa hivi hivi  wakiangaluwa!. Lakini wafuasi wao walipofanya jinai ya violence, ndipo  wakakamatwa!. *Kwa huu udhaifu wa JK,* sasa sio tena CCM itamfia mikononi
—End Quote—

—Quote—
Kondo Tutindaga
….. Lakini upo upande wa pili unaowakilishwa na udhaifu wa Kikwete kama Rais na mwenyekiti wa chama chetu. Rais na *mwenyekiti mwenye udhaifu wa kiuongozi* husababisha makundi ya watu wanaojipendekeza kwake au kujituma kufanya mambo ambayo yeye angefanya……..

…….Kwamba, *udhaifu wa Kikwete* ambao wakati mwingine unaitwa “uungwana wake” kwa vile unatendwa na mkuu wa nchi, ndio unaosababisha makada wachinjane, wauane, wakamiane, wasingiziane, na hatimaye waangamizane kisiasa……..

*………Udhaifu wa Kikwete* umelifikisha taifa mahali pagumu sana. Ili kurekebisha hali hii, gharama kubwa kisiasa na kiuchumi itatumika. Rais kwa hofu na aibu ya kusemwa sana na watu, anaweza kuzinduka na kuchukua hatua kwa jazba na hasira na kufanya makosa yanayoweza kuligharimu taifa kwa muda mrefu……….
—End Quote—

—Quote—
*Saed Kubenea
MwanaHalisi 30 November 2011
Kikwete, Lowassa hapatoshi*

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kauli ya Lowassa ambayo ilitolewa mbele ya viongozi wake wakuu, akiwamo rais mstaafu, *Benjamin Mkapa, ililenga kuonyesha udhaifu wa Kikwete ndani ya CCM *kwa kuasisi falsafa ya kujivua gamba na kuikimbiza moja kwa moja kwenye CC na NEC, kinyume cha taratibu na kanuni za chama chake.
—End Quote—

Imeandikwa na Omutwale wa JamiiForums

19 Comments
  • nimefurahishwa sana na uwazi wa mnyika na ningesikitishwa sana kama angefuta kauli yake cha kwanza anaposema sifuti kauli yangu mimi mbele ya luninga nilikuwa napiga makofi kama vile nipo bungeni.Hivi huyu si yule aliyesema hajui kwanini TANZANIA ni masikini angekuwa mwanafunzi angefeli kama sijakosea sana hili swali lipo kwenye geography form two sasa wa university anapokosea tusemeje?

  • tatizo ccm na serikali yake wanadhani hutujui kipi ni kipi, mfano nmeshuhudia mara nyingi spika anashabikia wabunge wa chama chake hasa katika hoja za mipasho..sasa unategemea nn hpo, eti huyo ni spika wa bunge la jamuhuri ya Tanzania

  • Nimefurahishwa sana msimamo wa Mnyika alionyesha bungeni watanzania muda wa kuogopa umekwisha.

  • Nasikitika jinsi binadam tulivyo na uchu wa madalaka,hii yote ni kuwafurahisha wakuu wa nchi na kulinda vyeo vyao .Hapa wangejifunza wapi wanachemka, na kujirekebisha.wajui ipo siku watakuwa uraiani watatendewa km wanavyotenda.kila kitu kina mwisho

  • Hakika hili si jambo jema na wala halina tija kwa Taifa hili!! Kitu cha msingi ni Spika wetu pamoja na wasaidizi wake kufanyia kazi ushauri wa Mhe, Mbowe, kwani unaweza kuwasaidia kuendesha Bunge kwa manufaa ya Taifa hili. TAFAKALI.

  • CCM wanapaswa kufahamu kuwa watanzania wa sasa sio wale waliozoea kuwaburuza, watake wasitake watatuachia nchi yetu kwa gharama yoyote na hii falsafa ya kutuimbisha wimbo wa umasikini haipo tena nchi yetu tajiri na rasilimali zetu zitunufaishe wenyewe vijana tumeamka kazi wanayo!

  • yes wada chama tawala hawataki kukubali ukweli wanafikiri watanzania tunawapenda kumbe hakuna watakiona 2015 general election kiufupi ccm hawajui maana ya utawala na nyakati.

  • Ban people,kill people but revolutionary ideas never die.ccm mjiandae kuwa chama cha upinzani 2015

  • mabadiliko ya kweli hayaji kiustaarabu hasa kulinganishwa na ccm. ni lazima kwanza mabaya yao yote yaanikwe mwisho wazikwe kwa aibu. na huu ndo mwisho wao. cdm wote na watanzania makini, walala hoi wanyonge, tusikubali kurudi nyuma tukamwacha mwizi akazidi kuuza uhai wetu na watoto wetu.

  • Ikiwa mtu mweusi akiambiwa wewe ni mweusi alafu wapambe wakadakia na kusema siyo mweusi alafu na yeye mwenyewe akajifariji kuwa kumbe yeye siyo mweusi haiwezi kubadili ukweli. cha msingi tufunguke ufahamu wote hata hao chukua chako ili tudhamilie mabadiliko ya kweli kunako 2015

  • Kuna usemi usemao kwamba ukweli unauma na hii ndio iliyomfanya ndugai kumtoa nje mnyika lakini, nashukuru sana kwamba mnyika hakufuta kauli, hii ni kukiamini alicho kisema kwamba ni sahihi.

  • Hivi ccm wanapokusema hivi kweli huumii au kusikia mbona hata siku moja hujiteei .Inawezekana wanachosema kina ukweli ndani yake .Hebu na wewe zinduka useme

  • kwani hamjui sikio la kufa halisikii dawa!hakika ccm inaelekea ukingoni,mtupe fursa tuchukue nchi.CHADEMA!

  • mie si mwanasiasa lakn mwisho wa reli abiria hupiga kelele kuashiria wamefika na wamechoshwa na mtikisiko wa treni ktk reli ni hayo tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

  • CCM wakiambiwa ukweli wanadai ati vijana wadogo hawana adabu,nidhamu na maadili yenye kutumia maneno ya hekima kama hayo,lakini wanakwenda mbali kwa kuwahita wahongo,wakati wakikosa hoja za kujitetea kwa umma.Mwandishi fulani riwaya wa hapa nchinikutoka huko maeneo ya Kanda ya ziwa, katika riwaya yake fulani ina kichwa “UWIKE USIWIKE KUTAKUCHA”,Ipo siku si mbali sana aliye juu ataanguka ukweli utasimama kwa njia hizi hizi,za kusema na kudai haki na ukweli wanabezwa.Wako wapi Machiefs,familia zao tuapiga debe pamoja Nasi,hawakuwaza kama siku moja watashuka, waliotuuza sokoni?,Waarabu?,Waingereza?.Kila jambo lina mwisho.Mapambano ya kubadilishana fikra yanasong mbele kama mzaha vile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *