WAUGUZI wawili, akiwemo muuguzi mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Mbeya (Mbalizi Ifisi), Sikitu Mbilinyi, wameacha kazi ghafla.
FikraPevu ina taarifa kuwa wameacha kazi wakati kukiwa na tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla kuwachunguza watumishi wanaodaiwa kutumia vyeti ambavyo siyo vyao au bandia (feki).
Muuguzi mwingine ambaye ameamua kuacha kazi ni Beatrice Mbilinyi ambaye ni mke wa Muuguzi Mkuu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, aliamua kuunda Tume hiyo Januari 10, mwaka huu, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wauguzi ambao hawakuwa na vyeti kuwa walifukuzwa kazi, huku baadhi ya wenzao wakibakishwa, licha ya kuwa na vyeti bandia vya taaluma hiyo.
Mbali na malalamiko hayo, Makalla alikabidhiwa majina ya wanaotuhumiwa ambayo FikraPevu imepata orodha yake.
Baadhi ya majina aliyopewa mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na jina la Naomi Jackson, Memory Nsemwa, Modester Kasebele, Anna Mwahalende, Rehema China, Zaina Ngove, Rehema Paza, Angel Mwakagenda, Tusekelege Tuntufye, Juliana Ackim, Tumpe Ackim, Prisca Michael, Hawa wa Mapokezi, Maria Mwambene, Tabu Kumwenda na Mwajabu Issa.
Wauguzi; Sikitu Mbilinyi na mkewe, Beatrice, ambao wote wameacha kazi ghafla
FikraPevu iliwasiliana na Muuguzi Mkuu, Sikitu Mbilinyi ili kujua sababu zilizosababisha kuacha kazi huku kukiwa na taarifa kuwa sababu moja wapo ni hasira zitokanazo na kudhalilishwa kuwa naye ni mmoja ambaye hatumii jina lake halisi.
"Ni kweli nimeacha kazi, lakini kwa hiari yangu mwenyewe na mke wangu leo (Jana), nilimtuma kwenda kuchukua barua kwa aliyekuwa mwajiri wangu,” Mbilinyi aliiambia FikraPevu.
Alithibitisha pia kuwa hata mkewe Beatrice Mbilinyi ameamua kuacha kazi ili waungane katika kufanya biashara.
"Mimi sihusiki na tuhuma zozote pale hospitalini, bali nimeamua kuacha kazi maana nina watoto wanne, wawili wapo chuo kikuu nawalipia hivyo nimeona nifanye biashara na mke wangu naamini atanisaidia kusimamia ninaposafiri wala si mtu mwingine" aliongeza Mbilinyi wakati akiongea na FikraPevu.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Emmanuel Mbwile alipoulizwa kuhusu sababu kuu ya wauguzi hao kuacha kazi alisema yeye siyo msemaji, bali msemaji ni Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo ya Kanisa la Uinjilisti Tanzania, Mchungaji Tito Nduka, ambao ndiyo wamiliki wa hospitali hiyo.
Mchungaji Nduka alithibitisha kupokea barua yake ya kuacha kazi na kwamba baada ya kupokea barua yake walimpa likizo ya malipo.
FikraPevu ilibaini kuwa sakata la kufukuzana katika hospitali hiyo lilianza Novemba 15, 2016 kwa kubandika majina pendekezwa katika ubao wa matangazo huku baadhi ya watu wakiachwa. Watu walioitwa kuonana na uongozi wa hospitali hiyo walikuwa 36 ambao majina yao tumeyabaini.
Watu hao ni pamoja na Aneth Mwanamtwa, Atuganile Mwasaga, Angela Mwakagenda, Upendo Kajange, Neema Mpangala, Netto Mwasongole, Esther Mwasalwiba, Lilian Kaduma, Rebecca Mwashala, Anna Mulukeghe, Faraja Sanga, Hawa Kalinga, Grace Kayombo, Prisca Lucas na Amina Ngumbilo.
Wengine ni Boniface Robert, Bosco Christopher, Boniface Robert, Tabia Mwakaje, Upendo mwakatika, Atuganile Mwanjala na Edna Kasebele.
Wengine ni Faustina Masuwa, Tunaye Kusiluka, Nasibu Janiwelo, Hawa Mwakijengele, Daud KMwasomola, Faraja Sanga, Helena John, Flora Sanga, Subby Mwanjala, Jesaya Katembo, Memory Nsema, Ulimbalisya Mtafya, Robert Mpalala, Gwamaka Kinyali na Rose Mwantebela.