Tarehe 15 Desemba 2016, Dk Mwele Malecela, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI) alitangaza hadharani kuwa kuna virusi vya Zika nchini Tanzania.
“Zika ipo nchini mwetu, na kati ya watu 533 waliofanyiwa uchunguzi 15.6% walikutwa wameathiriwa na virusi vya Zika” Dk Mwele alinukuliwa akiwaaambia waandishi wa habari.
Dk Mwele aliweka bayana kuwa uchunguzi huo ulifanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki Bugando kilichopo Mwanza, Kaskazini mwa Tanzania na huko watoto 80 waliochunguzwa 35 sawa na 43% walionekana kuwa na virusi vya Zika.
Uchunguzi huo ulikusudia kufahamu kama virusi vya Zika vipo nchini mwetu na kama vinaleta athari hadi kupelekea watoto kuzaliwa wakiwa na ulemavu”. Dk Mwele aliliambia gazeti la Kiingereza la Daily News.
Kauli hizi ziliweza kuonekana kupingana na hoja za awali zilizotolewa na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, ambaye Februari 16 mwaka 2016, alitangaza kwamba Zika haijaingia nchini mwetu.
Siku moja baada Dk Mwele kueleza hayo, Waziri wa afya alijitokeza na kukanusha akisema hakukuwa na ushahidi wa kutosheleza kwamba virusi vya Zika vipo nchini.
“Hakuna uthibitisho kwamba kuna virusi vya Zika nchini hadi sasa” alisema Mwalimu kwa mujibu wa shirika la utangazaji la China – Xinhua. “Virus vya Zika ni ni tatizo linalopaswa kutangazwa kimataifa, ambapo hali hiyo ikibainika ni lazima ithibitishwe na shirika la afya duniani (WHO) kwa kushirikiana na ofisi ya mganga mkuu wa serikali wan chi husika.
Aliongeza kwamba “Nawahakikishia watu kwamba hadi sasa uwepo wa ugonjwa wa Zika haujathibitishwa”
Kufuatia kutokukubaliana hadharani kati ya Waziri wa Afya na Dk Mwele, Mkuu huyo wa Taasisi ya utafiti alitenguliwa kazini.
Swali lililobaki, je kuna Zika Tanzania au hakuna? Kwa nchi ambayo kiwango cha uzazi kipo takribani watoto watano kwa kila mama , madai ya uwepo wa virusi vya Zika kuwepo Tanzania yanapaswa kuangaliwa.
PesaCheck wamefanya Utafiti na kubaini kuwa utafiti wa Dk Mwele, ulikuwa wa kweli, na kwa upande mwingine ilikuwa sawa kwa Waziri wa Afya kutamka kuwa hakuna ugonjwa wa Zika nchini Tanzania kwa sababu
Shirika la Afya duniani (WHO) linasema kuwa mwanadamu wa kwanza kupatikana na virus vya zika aliishi kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1952, na ugunduzi huo ulilipofanywa ulisaidia kupatikana kwa chanjo za Zika katika nchi hizo.
Kwa nyongeza ni kwanza, Februari mwaka 2016, tathimini ya athari iliyofanywa na Shirika la Afya kwa nchi za Afrika, Tanzania ipo katika kiwango cha kati cha kupatikana na athari za uwepo wa virusi vya Zika. Nchi hizo ndizo zinazotarajiwa kupewa kipaumbele katika masuala ya kliniki na udhibiti wa malaria