Auawa kwa kuchinjwa na kuachanishwa kichwa na kiwiliwili; muuaji atembea na kichwa mtaani!

Sitta Tumma

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mkazi mmoja wa mtaa wa Bugarika jijini Mwanza, Malimi Mathias ameuawa kikatili kwa kuchinjwa kisha kuachanishwa kichwa na kiwiliwili.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 6-8 mchana, baada ya mtuhumiwa wa mauaji hayo aitwaye Bahati Vincent kumchinja kinyama Mathiasi na baadaye kuanza kutembea  mitaani na kichwa cha marehemu.

Duru za habari kutoka eneo la tukio na ndani ya Jeshi la Polisi makao makuu mkoani Mwanza, zinaeleza kwamba chanzo cha mauaji hayo ya kinyama ni deni la pombe aina ya gongo ambalo marehemu Mathias alikuwa akidaiwa na Vincent.

Taarifa zisizokuwa na shaka yoyote ambazo pia zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ernest Mangu zinasema kwamba wawili hao walikuwa wakidaiana deni la pombe hiyo ya kienyeji, na siku ya tukio Vincent alichukuwa panga kisha kwenda kumchinja Mathias.

RPC Mangu amekaririwa akisema, baada ya mtuhumiwa Vincent kutenda unyama huo, wananchi wenye hasira kali walimkimbiza kisha kumkamata na kumpiga hadi kumuua na yeye!.

7 Comments
  • jaman utu wetu upo wapi kila kukicha mara mia ya jana ee mwnyezi mungu tusaidie na mungu amsamehe huyo aliyetenda unyama huo

  • Huenda ni mwendawazimu! kitendo cha yeye kuuwawa kitasabisha kupata ukweli. Japo deni ndilo linaloonekani ni sababu. Au alitumiwa na Mganga. kunaweza kukawa na mambo mengi yaliyo jificha na yengeweza kujulukana kupitia yeye aliye uwawa.

  • Ktk hili Watanzania bado tuko ktk mazingira magumu kwani mtuhumiwa angehojiwa na kujibu chanzo cha kumuua mwenzie….

    TUSIJICHUKULIE SHERIA MKONONI.

  • tumuogope mwenyezi mungu m2 unatoa uhai wa mwenzio then unatembea na kichwa chake ama kweli dunia imekwisha ndugu zangu kila m2 na imani yake tumludi mwenyezi mungu huko ndio kimbilio letu 

  • Tutambueni tupo siku za mwisho km maneno ya Mungu yanavyosema…Ee mwenyezi Mungu uturehemu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *